Mwakalinga Bujo
JF-Expert Member
- Oct 22, 2008
- 2,719
- 1,440
Katika viongozi watakao weka historia mbaya nchini ,Rais huyu atakuwa wa kwanza.Nadhani washauri wake wameshindwa kusoma alama za nyakati.Yanayotokea Igunga ni chachu na picha ya mambo yatakavyakuwa tunakoelekea miaka ijayo hivi karibuni.
Kwa wanaofahamu falsafa ya Uongozi,kiongozi mkuu wa nchi (ambaye kwa Tanzania ni Rais).Viongozi hawa huchukuliwa kama ni watu wenye maono na karama za pekee kutoka kwa mwenyezi Mungu.Kiongozi mkuu wa nchi anapopita sehemu yoyote kama ilikuwa haina neema, itakuwa ni moja ya chachu na chanzo cha neema pindi atakapoondoka kutokana na matatizo atakayoelezwa na hatua madhubuti atakazo chukua kutatua kero/maswala mbalilimbali yanayogusa maendeleo ya eneo husika.
Yanayotokea kwa serikali ya mh. JK ni kutatua matatizo ya wanaomwanika hadharani kuwa yeye hana uwezo na karama ya kuwa kiongozi mkuu wa nchi (Vita hivi anapigana na wapinzani wake wa kisiasa ndani ya chama na nnje ya chama chake).Yapo mambo mengi ambayo kimsingi alitakiwa ayafumbie macho ili akimbilie kwa watetezi wake wamwisho ambao ni wananchi ( wapiga kura),kwa kusikiliza na kutatua kero zao.
Kiongozi ambaye hana umaarufu kwa wananchi wake siku zake za kukaa madarakani zinahesabika.Ni kitendo cha kustaabisha ukihesabu mambo yalimkumba Mh. Jk tokea ameingia madarakani,mfano kitendo cha msafara wake kupigwa mawe alipofanya ziara mkoani Mbeya.Matukio kama haya yanaweza yasipewe uzito kutokana na yanavyoripotiwa na vyombo vya habari.Ila ni kigezo kikubwa kwa kuangalia/kupima umaarufu wa kiongozi kwa wachambuzi /wafuatiliaji wa mambo.Kisiasa ni hatari sana kwa kustakabali wa kiongozi huyo.
Mambo mengine yanayodhihirisha kuwa kiongozi huyu amepoteza umaarufu ni kwenye mitandao ya kijamii.Mijadala mingi inayoendeshwa inakuwa inamkosoa na kumpinga wazi wazi kana kwamba sio Kiongozi wa nchi,mitandao ya kijaii ni muhimu kwa zama hizi kwani hutumika kama njia ya kuwasiliana baina ya mtu na mtu ,mtu na kundi ama kundi moja na kundi jingine.Nchi nyingine mitandao hii ya kijamii inatumiwa na viongozi kuwapasha habari wananchi na kutoa fursa ya kujadiliana/kushauriana maswala mbali mbali ya kijamii,kisiasa na kiuchumi.Kilichotokea tare 25/9/2011 wakati Rais alipoweka status na wachangiaji kuanza kuporomosha matusi ya wazi kuonyesha kuwa wamechoshwa na uongozi wake ni hatari sana.Kama watu unaowaongoza hawana imani na uongozi wako ni dhahiri unakosa/unapoteza sifa za kuwa kiongozi.
Yapo mengi yaliyotokea ila jingine ambalo litamtafuna sana Mh. Jk ni hili la hukumu ya leo -Tanesco iwalipe Dowans 94 bil. Tshs.Kweli Rais huyu hana washauri na hajaweza kusoma alama za nyakati ..Katika zama hizi za kiza /mgao mkali wa umeme,anaachia vyombo vilivyoko chini yake kufanya maamuzi bila kupima uzito wa jambo jenyewe.Anaamsha hisia za Watanzania kwa uchafu uliofanywa na watendaji wake!.Mbaya waliofanya uchafu huo wapo mtaani wanatembea na ma V8 kwa mbwembwe zote.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.