JK ana hali mbaya sana ...

Mwakalinga Bujo

JF-Expert Member
Oct 22, 2008
2,720
1,435
Katika viongozi watakao weka historia mbaya nchini ,Rais huyu atakuwa wa kwanza.Nadhani washauri wake wameshindwa kusoma alama za nyakati.Yanayotokea Igunga ni chachu na picha ya mambo yatakavyakuwa tunakoelekea miaka ijayo hivi karibuni.
Kwa wanaofahamu falsafa ya Uongozi,kiongozi mkuu wa nchi (ambaye kwa Tanzania ni Rais).Viongozi hawa huchukuliwa kama ni watu wenye maono na karama za pekee kutoka kwa mwenyezi Mungu.Kiongozi mkuu wa nchi anapopita sehemu yoyote kama ilikuwa haina neema, itakuwa ni moja ya chachu na chanzo cha neema pindi atakapoondoka kutokana na matatizo atakayoelezwa na hatua madhubuti atakazo chukua kutatua kero/maswala mbalilimbali yanayogusa maendeleo ya eneo husika.

Yanayotokea kwa serikali ya mh. JK ni kutatua matatizo ya wanaomwanika hadharani kuwa yeye hana uwezo na karama ya kuwa kiongozi mkuu wa nchi (Vita hivi anapigana na wapinzani wake wa kisiasa ndani ya chama na nnje ya chama chake).Yapo mambo mengi ambayo kimsingi alitakiwa ayafumbie macho ili akimbilie kwa watetezi wake wamwisho ambao ni wananchi ( wapiga kura),kwa kusikiliza na kutatua kero zao.
Kiongozi ambaye hana umaarufu kwa wananchi wake siku zake za kukaa madarakani zinahesabika.Ni kitendo cha kustaabisha ukihesabu mambo yalimkumba Mh. Jk tokea ameingia madarakani,mfano kitendo cha msafara wake kupigwa mawe alipofanya ziara mkoani Mbeya.Matukio kama haya yanaweza yasipewe uzito kutokana na yanavyoripotiwa na vyombo vya habari.Ila ni kigezo kikubwa kwa kuangalia/kupima umaarufu wa kiongozi kwa wachambuzi /wafuatiliaji wa mambo.Kisiasa ni hatari sana kwa kustakabali wa kiongozi huyo.

Mambo mengine yanayodhihirisha kuwa kiongozi huyu amepoteza umaarufu ni kwenye mitandao ya kijamii.Mijadala mingi inayoendeshwa inakuwa inamkosoa na kumpinga wazi wazi kana kwamba sio Kiongozi wa nchi,mitandao ya kijaii ni muhimu kwa zama hizi kwani hutumika kama njia ya kuwasiliana baina ya mtu na mtu ,mtu na kundi ama kundi moja na kundi jingine.Nchi nyingine mitandao hii ya kijamii inatumiwa na viongozi kuwapasha habari wananchi na kutoa fursa ya kujadiliana/kushauriana maswala mbali mbali ya kijamii,kisiasa na kiuchumi.Kilichotokea tare 25/9/2011 wakati Rais alipoweka status na wachangiaji kuanza kuporomosha matusi ya wazi kuonyesha kuwa wamechoshwa na uongozi wake ni hatari sana.Kama watu unaowaongoza hawana imani na uongozi wako ni dhahiri unakosa/unapoteza sifa za kuwa kiongozi.

Yapo mengi yaliyotokea ila jingine ambalo litamtafuna sana Mh. Jk ni hili la hukumu ya leo -Tanesco iwalipe Dowans 94 bil. Tshs.Kweli Rais huyu hana washauri na hajaweza kusoma alama za nyakati ..Katika zama hizi za kiza /mgao mkali wa umeme,anaachia vyombo vilivyoko chini yake kufanya maamuzi bila kupima uzito wa jambo jenyewe.Anaamsha hisia za Watanzania kwa uchafu uliofanywa na watendaji wake!.Mbaya waliofanya uchafu huo wapo mtaani wanatembea na ma V8 kwa mbwembwe zote.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,519
6,084
jk ni tia maji tia maji yaani duniani hayupo ahera hayuoo basi tafrani tupu
 
Bigirita

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
15,866
7,161
Duniani hayupo, ahera hayupo??!
tia maji tia maji....yani mguu kwenye break na kwenye accelerator.....ukiachia mafuta gari inazima, silence haipo.
 
Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,046
Duniani hayupo, ahera hayupo??!
tia maji tia maji....yani mguu kwenye break na kwenye accelerator.....ukiachia mafuta gari inazima, silence haipo.
Dahhh kwa kweli ni full magumashi, akivaa suti alizohongwa na kijana wa kiarabu unaona kweli kiongozi tumepata kumbe hana lolote maskin ya mungu, ubabaishaji mtupu, kuwa na kiongoz wa hivi ni mzigo kwa taifa, yan 2015 ni kama karne kwa watanzania.
 
DASA

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,031
301
Katika viongozi watakao weka historia mbaya nchini ,Rais huyu atakuwa wa kwanza.Nadhani washauri wake wameshindwa kusoma alama za nyakati.Yanayotokea Igunga ni chachu na picha ya mambo yatakavyakuwa tunakoelekea miaka ijayo hivi karibuni.
Kwa wanaofahamu falsafa ya Uongozi,kiongozi mkuu wa nchi (ambaye kwa Tanzania ni Rais).Viongozi hawa huchukuliwa kama ni watu wenye maono na karama za pekee kutoka kwa mwenyezi Mungu.Kiongozi mkuu wa nchi anapopita sehemu yoyote kama ilikuwa haina neema, itakuwa ni moja ya chachu na chanzo cha neema pindi atakapoondoka kutokana na matatizo atakayoelezwa na hatua madhubuti atakazo chukua kutatua kero/maswala mbalilimbali yanayogusa maendeleo ya eneo husika.

Yanayotokea kwa serikali ya mh. JK ni kutatua matatizo ya wanaomwanika hadharani kuwa yeye hana uwezo na karama ya kuwa kiongozi mkuu wa nchi (Vita hivi anapigana na wapinzani wake wa kisiasa ndani ya chama na nnje ya chama chake).Yapo mambo mengi ambayo kimsingi alitakiwa ayafumbie macho ili akimbilie kwa watetezi wake wamwisho ambao ni wananchi ( wapiga kura),kwa kusikiliza na kutatua kero zao.
Kiongozi ambaye hana umaarufu kwa wananchi wake siku zake za kukaa madarakani zinahesabika.Ni kitendo cha kustaabisha ukihesabu mambo yalimkumba Mh. Jk tokea ameingia madarakani,mfano kitendo cha msafara wake kupigwa mawe alipofanya ziara mkoani Mbeya.Matukio kama haya yanaweza yasipewe uzito kutokana na yanavyoripotiwa na vyombo vya habari.Ila ni kigezo kikubwa kwa kuangalia/kupima umaarufu wa kiongozi kwa wachambuzi /wafuatiliaji wa mambo.Kisiasa ni hatari sana kwa kustakabali wa kiongozi huyo.

Mambo mengine yanayodhihirisha kuwa kiongozi huyu amepoteza umaarufu ni kwenye mitandao ya kijamii.Mijadala mingi inayoendeshwa inakuwa inamkosoa na kumpinga wazi wazi kana kwamba sio Kiongozi wa nchi,mitandao ya kijaii ni muhimu kwa zama hizi kwani hutumika kama njia ya kuwasiliana baina ya mtu na mtu ,mtu na kundi ama kundi moja na kundi jingine.Nchi nyingine mitandao hii ya kijamii inatumiwa na viongozi kuwapasha habari wananchi na kutoa fursa ya kujadiliana/kushauriana maswala mbali mbali ya kijamii,kisiasa na kiuchumi.Kilichotokea tare 25/9/2011 wakati Rais alipoweka status na wachangiaji kuanza kuporomosha matusi ya wazi kuonyesha kuwa wamechoshwa na uongozi wake ni hatari sana.Kama watu unaowaongoza hawana imani na uongozi wako ni dhahiri unakosa/unapoteza sifa za kuwa kiongozi.

Yapo mengi yaliyotokea ila jingine ambalo litamtafuna sana Mh. Jk ni hili la hukumu ya leo -Tanesco iwalipe Dowans 94 bil. Tshs.Kweli Rais huyu hana washauri na hajaweza kusoma alama za nyakati ..Katika zama hizi za kiza /mgao mkali wa umeme,anaachia vyombo vilivyoko chini yake kufanya maamuzi bila kupima uzito wa jambo jenyewe.Anaamsha hisia za Watanzania kwa uchafu uliofanywa na watendaji wake!.Mbaya waliofanya uchafu huo wapo mtaani wanatembea na ma V8 kwa mbwembwe zote.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.

JK hii Nchi imeshamshinda. AJIUZULU.
 
Chimunguru

JF-Expert Member
May 3, 2009
10,676
4,301
Kosa hili la kuchagua mtu asiye na uwezo lisirudiwe tena. hii imetokana na pesa chafu za Rostam na Lowasa wanamtandao waliohonga wajumbe wa CCM na kumweka huyu mtalii madarakani
 
Mbugi

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,489
256
Kosa hili la kuchagua mtu asiye na uwezo lisirudiwe tena. hii imetokana na pesa chafu za Rostam na Lowasa wanamtandao waliohonga wajumbe wa CCM na kumweka huyu mtalii madarakani

Nimejifunza jambo kwa JK. na nampongeza sana kwa ukomavu wa siasa, kwani pamoja na matusi, kashfa, maombi yote mabaya, na kutomtakia mema, ameendelea kuwa mvumilivu kisiasa sifa ambayo viongozi wengi duniani wameshindwa. chukua mfano tu wa vyama vingi ikiwemo vile tu ambavyo hata bado havijapewa dhamana kwa kiasi fulani inapofikia tu kiongozi kukosolewa anavyogeuka mbogo. angalia ya Mrema na mzee Tau, (TLP). Maamuzi zidi ya madiwani Arusha, na kwingineko ni baadhi tu ya ukosefu wa uvumilivu wa kisiasa.
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,580
25,244

ni kweli amekomaa kwani yeye hujui ana kichwa nazi!
 
jigoku

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,413
730
Ukomavu wake uko wapi?usitake kuudhi watu hapa,ukomavu wake uko wapi?hivi wewe uko Tz au uko nchi jirani,hii nchi huioni inavyokwenda?hivi uliwahi kuona wapi Raisi anawaambia wezi rudisheni pesa halafu basi inaishia hivyo?wangapi wako gerezani kwa wizi wa kuku?Hii nchi ilipofika hapa unatuambia kakomaa kisiasa,wewe!au umetumwa?au kibaraka wa Nape?please think twice,hakuna ukomavu wala uvumilivu.hayo ya madiwani chadema ndo tunachokihitaji,wame-violate katiba off they go.nyinyi mlituambia siku tisini magamba mtayavua mbona yamewashinda?au huko ndo kukomaa kisiasa?na kwa taarifa yako,ndani ya CCM hakuna mwenye uwezo wa kufukuza Lowasa na Chenge ambao ndo mmewatuhumu ni magamba,wakati sisi tunajua kuna magamba karibu chama chote.
Usiruduie tena kufikiri kwa kutumia masaburi,hakuna ukomavu wa kisiasa alionao Jei Kei.
 
uporoto01

JF-Expert Member
May 23, 2008
4,718
1,378
You are barking at the wrong tree,Kikwete hawezi kujiuzulu hilo halitatokea,hatasimama kwenye uchaguzi tena anamalizia miaka yake minne kama afya itamruhusu.Mapinduzi ya jeshi ni ndoto kwakuwa ni MWENZAO na wanajivunia mtu aliyepitia jeshini kuongoza nchi.Vyama vya siasa vijipange kuanzia muda huu;
1.kushinikiza tume huru ya uchaguzi,
2,kupatikana katiba mpya,
3.kujiimarisha nchi nzima mambo ya 'shuka hadi shuka'.
 
Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,039
Hata Gaddaf na Mubarack ni wanajeshi lkn wako wapi,ndugu jeshi aliwezi kushinda na popular democracy.Ila ya Tanzania yaweza kuwa kama ya Baharin and Syria.
 
CCM they have guns CHADEMA have PEOPLES POWER!
 
Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
3,840
628
Yapo mengi yaliyotokea ila jingine ambalo litamtafuna sana Mh. Jk ni hili la hukumu ya leo -Tanesco iwalipe Dowans 94 bil. Tshs.Kweli Rais huyu hana washauri na hajaweza kusoma alama za nyakati ..Katika zama hizi za kiza /mgao mkali wa umeme,anaachia vyombo vilivyoko chini yake kufanya maamuzi bila kupima uzito wa jambo jenyewe.Anaamsha hisia za Watanzania kwa uchafu uliofanywa na watendaji wake!.Mbaya waliofanya uchafu huo wapo mtaani wanatembea na ma V8 kwa mbwembwe zote.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.[/QUOTE]

Hapo kwenye red ni 94bil. plus gharama za kesi natakataka nyingine
ambapo ki uhalisia ni
111bil.tsh.

kinachoniuma ni mahakama iliweka masharti ya kuwa DOWANS
hawaruhusiwi kufanya chochote bila ruhusa ya mahakama ila
cha kushangaza wakajiuza kwa SYMBION bila ya ridhaa ya mahakama.
leo hii mahakama hiyo nayo inatoa hukumu dowans ilipwe mimi sielewi
na sipendi kutoamini kama hakuna rushwa au mkono wa mkulu!!
 
Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,177
3,326

[/QUOTE]

Hata mimi nashangaa sana, yaani umeme hatuna halafu tena tunaenda kulipa watu matapeli bila sababu ya msingi. Ningekuwa mimi nisingekubali kutoa fedha hizo hazina maana ni mzigo usiobebeka.
 
Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
35,318
35,438
miaka kumi hana hata kitu kimoja alichofanya cha kusimulia, hivi atawaeleza nini wajukuu zake miaka ijayo.
 
Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,703
142
Hapo kwenye red ni 94bil. plus gharama za kesi natakataka nyingine
ambapo ki uhalisia ni
111bil.tsh.

kinachoniuma ni mahakama iliweka masharti ya kuwa DOWANS
hawaruhusiwi kufanya chochote bila ruhusa ya mahakama ila
cha kushangaza wakajiuza kwa SYMBION bila ya ridhaa ya mahakama.
leo hii mahakama hiyo nayo inatoa hukumu dowans ilipwe mimi sielewi
na sipendi kutoamini kama hakuna rushwa au mkono wa mkulu!!

Hata mimi nashangaa sana, yaani umeme hatuna halafu tena tunaenda kulipa watu matapeli bila sababu ya msingi. Ningekuwa mimi nisingekubali kutoa fedha hizo hazina maana ni mzigo usiobebeka.[/QUOTE]

Watawala wa Tanzania ni demonic kiasi kwamba hawajali kabisa how we feel.They are sadists of the highest order.
 
Majala Kimolo

JF-Expert Member
Aug 3, 2007
342
39
Nimejifunza jambo kwa JK. na nampongeza sana kwa ukomavu wa siasa, kwani pamoja na matusi, kashfa, maombi yote mabaya, na kutomtakia mema, ameendelea kuwa mvumilivu kisiasa sifa ambayo viongozi wengi duniani wameshindwa. chukua mfano tu wa vyama vingi ikiwemo vile tu ambavyo hata bado havijapewa dhamana kwa kiasi fulani inapofikia tu kiongozi kukosolewa anavyogeuka mbogo. angalia ya Mrema na mzee Tau, (TLP). Maamuzi zidi ya madiwani Arusha, na kwingineko ni baadhi tu ya ukosefu wa uvumilivu wa kisiasa.
Mwagito pole, nafikiri hujui maana ya Siasa ndo maana ukadhani kupuuza kwake maoni ya wanaotaka tija ya uongozi wake basi ndo ukomavu. Siasa sio ulaghai au blahblah, siasa ni sayanzi na inaendeshwa kwa utafiti na uhakika wa ukisemacho. Tafsiri ya siasa ni sayansi ya uongo ndiyo iliyomfikisha hapo huyu jamaa, alidhani akishasema jukwaani baasi yamekwisha, kumbe ndo kalianzisha, alidhani unaweza kuwadanganya watu wote kwa muda wote, kumbe sivyo, aghlabu mambo yake yanawafanya watu wengi wajisikie wanyonge na ukiwa katika kipindi chake cha uongozi. Ni kweli jamaa ni muungwana, anakiri kuwa mambo yamemshinda ndo maana badala ya kukemea, analalamika. Sasa sijui anataka nani afanyie kazi kero
Leo hata sukari inataka kuwa bidhaa adimu, eti kakomaa kisiasa, mafuta na umeme ni kero. Kukomaa gani huku unakokusema mnyalukolo
Mpe pole shemejiyo, analo hilo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom