Hali ya Kunga cha Mbopo - Bunju ni mbaya sana!!

Mangi wa Rombo

Senior Member
Sep 25, 2014
172
104
Habari wana JF!

Nafahamu kumekuwa na ripoti nyingi za uharibifu wa miundombinu kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha, lakini leo ningependa nilete jukwaani hapa hali ya kiunga kati ya Mbopo na Bunju, kutoka kata ya Mabwepande, wilaya ya kinondoni.

Kwa sasa hakuna mawasiliano kabisa kufuatia kukatika kwa kiunga hichi kilichopo mbele kidogo baada ya mbopo center eneo maarufu "mabanda ya kuku"

Kibaya zaidi ni kwamba shule ya kata na zahanati zipo upande wa mbopo hivyo wagonjwa na watoto wanahatarisha maisha kwa kupita juu ya bomba la Dawasa kama inavyo onekana hapo kwenye video!
Juhudi za kupata hata daraja la muda la waenda kwa miguu zimegonga mwamba!

M-bunge wa jimbo la Kawe,Mh Josephat Gwajima amekuwa mwenye kukwepa kukutana na wananchi wa eneo hili, na amekuwa akitoa ahadi hewa bila utekelezaji! Hili ni jimbo ambalo yeye mwenyewe kupitia ukurasa wake wa Instagram alipost video ya Mh Makonda akitoa ahadi ya magreda 20 lakini mpaka leo hata greda moja halijaonekana.

Watoto wako hatarini, inapotokea wako shule na mvua ikanyesha bhasi wanakaa upande wa pili hadi maji yapungue kisha wanapita juu ya bomba!

Miaka 63 ya Uhuru bado kuna kata hapa Dar haina kiunganishi na watoto wanabebwa mabegani.
TARURA wanajua juu ya eneo hili ila hawajawahi kutoa majibu! Ofisi ya Mkuu wa Wilaya inayo taarifa!
Swali ni je, mnasubiri hadi mtu apoteze maisha au kuumia ndo mchukue hatua?

#Jamiiforums tusaidieni kupaza sauti

Kwa sasa hana shabiki Mbopo hata mmoja! Tangu majanga yatokee Mh Chalamila RC amekuwa karibu na wakaz wa huku kuliko yeye! Tulikaa na Chalamila hadi saa nne usiku tukijenga daraja la Panga Boy.. yeye hata kutokea hakutokea
 
Habari wana JF!

Nafahamu kumekuwa na ripoti nyingi za uharibifu wa miundombinu kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha, lakini leo ningependa nilete jukwaani hapa hali ya kiunga kati ya Mbopo na Bunju, kutoka kata ya Mabwepande, wilaya ya kinondoni.

Kwa sasa hakuna mawasiliano kabisa kufuatia kukatika kwa kiunga hichi kilichopo mbele kidogo baada ya mbopo center eneo maarufu "mabanda ya kuku"

Kibaya zaidi ni kwamba shule ya kata na zahanati zipo upande wa mbopo hivyo wagonjwa na watoto wanahatarisha maisha kwa kupita juu ya bomba la Dawasa kama inavyo onekana hapo kwenye video!
Juhudi za kupata hata daraja la muda la waenda kwa miguu zimegonga mwamba!

M-bunge wa jimbo la Kawe,Mh Josephat Gwajima amekuwa mwenye kukwepa kukutana na wananchi wa eneo hili, na amekuwa akitoa ahadi hewa bila utekelezaji! Hili ni jimbo ambalo yeye mwenyewe kupitia ukurasa wake wa Instagram alipost video ya Mh Makonda akitoa ahadi ya magreda 20 lakini mpaka leo hata greda moja halijaonekana.

Watoto wako hatarini, inapotokea wako shule na mvua ikanyesha bhasi wanakaa upande wa pili hadi maji yapungue kisha wanapita juu ya bomba!

Miaka 63 ya Uhuru bado kuna kata hapa Dar haina kiunganishi na watoto wanabebwa mabegani.
TARURA wanajua juu ya eneo hili ila hawajawahi kutoa majibu! Ofisi ya Mkuu wa Wilaya inayo taarifa!
Swali ni je, mnasubiri hadi mtu apoteze maisha au kuumia ndo mchukue hatua?

#Jamiiforums tusaidieni kupaza sauti
View attachment 2890938

View attachment 2890940
Gwajima hajishughulishi na matatizo ya Kawe kwa sababu kuu mbili hapo chini.

1. Ashajua kwamba mwaka 2025, chama chake hakitomchagua kugombea tena jimbo la Kawe. Kwani aliempitisha wakati ule ameshafariki.

2. Ikitokea akapita ki ujanja ujanja basi hakuna mwana Kawe ambae atapoteza muda wake kumchagua tena awe mbunge wa jimbo hilo any more. Kwani jimbo hili ni la wasomi na watu wanaojitambua sana. Hawawezi kufanya kosa baada ya kosa kwa kumchagua tena mtu wa kuja kutafuna mamilioni salary za bunge bila kusaidia changamoto za wananchi.
 
Mbunge wetu anawasaidia wananchi wote jimboni bila shida yeyote na mpaka Bungeni anasimama na kuongea juu ya jimboni kwetu || wananchi tunampenda sana anatusaidia.
 
Back
Top Bottom