Hali ya Vijijini ni mbaya sana

Abuu Dharr

JF-Expert Member
Dec 28, 2017
2,898
3,006
Bila kupoteza muda,hali ya amani katika Vijijini vyetu ni ya kusikitisha sana,Serikali wekeni umakini katika hili
Kuna tukio limetokea hivi karibuni,katika Kijiji cha Magoza kata ya Kuparang'anda.

Binti mlemavu wa masikio,macho na bubu,amebakwa mchana kweupe, ni hili la kubaka, ni jambo la kawaida sana Vijijini,na Hawana njia ya kutatua.

Kadhalika,jambo la kutiana mimba hususan kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi,imekuwa kawaida mno,adhabu anayopewa Mtia mimba,ni kupeleka kiroba cha sembe kilo Tano kila wiki.

Tatizo
Katika Vijiji vingi,hakuna vituo vya polisi,hakuna lolote lile ambalo wananchi wanaweza kukimbilia
Ifike Wakati, Serikali iweke angalau Kituo kimoja katika Kijiji au Kitongoji,kupunguza uhalifu na kuweka amani

Unaweza kusema
Serikali ipo Mjini tu, Kijijini hakuna Serikali
 
Bila kupoteza muda,hali ya amani katika Vijijini vyetu ni ya kusikitisha sana,Serikali wekeni umakini katika hili
Kuna tukio limetokea hivi karibuni,katika Kijiji cha Magoza kata ya Kuparang'anda,Binti mlemavu wa masikio,macho na bubu,amebakwa mchana kweupe,Ni hili la kubaka,ni jambo la kawaida sana Vijijini,na Hawana njia ya kutatua,
Kadhalika,jambo la kutiana mimba hususan kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi,imekuwa kawaida mno,adhabu anayopewa Mtia mimba,ni kupeleka kiroba cha sembe kilo Tano kila wiki....
Tatizo
Katika Vijiji vingi,hakuna vituo vya polisi,hakuna lolote lile ambalo wananchi wanaweza kukimbilia
Ifike Wakati,Serikali iweke angalau Kituo kimoja katika Kijiji au Kitongoji,kupunguza uhalifu na kuweka amani

Unaweza kusema
Serikali ipo Mjini tu,Kijijini hakuna Serikali
Halafu huko CCM imetamalaki sana
 
MKuuu kupeleka Kituo cha Polisi kwenye kijiji ni namna fulani ya kudumaza kijiji husika na kuvunja undugu na ushirikiano uliodumu toka Vijiji vya Ujamaa.
Askari wetu wanapenda kuonea Wanavijiji sana.
Watawabambika kesi watauza Mazao yao na Ng'ombe zao kulipa faini hewa.
Hata hizo Mimba watajigeuza Mahakama na kupokea hongo.
Kila ugomvi mdogo wananchi watakimbilia polisi na hatimaye Utengano utaongezeka.
Vijana watahama Kijiji kuepuka kukamatwa kwa kesi za hovyo hovyo ili askari wapate pesa chafu.
Anyway kituo cha Polisi Kijijini kwetu hapana tumeapa hatutaki pelekeni huko.
 
Back
Top Bottom