Rais Kikwete amteua Zitto kamati ya Madini

Nyani yaani umenifanya nicheke hadi machozi...

sasa nyinyi mnavyonishangaa mimi ninavyoshangaa, najikuta nazidi nawashangaa!!

Mkandara, tulichoshuhudia ndio kinachoitwa mazingaombwe ya Prof. Ndumba Nangae, goli kama la Maradona ndiyo hilo linaingia pole pole. Ndio maana nikashangaa watu wameamka kufurahia "Kikwete afanya Kweli".. n.k
 
Hongera JK kwa uamuzi huu wa kumweka Zitto hapo kama kweli ni kwania hasa na si kumpooza. Najua pia Bwana Kamugisha Mugisha jamaa ni kichwa ile mbaya, kwa ujumla kamati naona ni nzuri ila tatizo Tanzania huwa tunaunda makamati na matume lakini matokeo yake huwa hayafanyiwi kazi. Muhimu ni kufanyia kazi report za Tume hizi zinazoundwa na sio kuunda tuu tume riport ikitoka inakaa kwenye mashelve.
 
Jamani hii kamati haijaanza kazi na sijui itaanza kazi yake lini. Tupendekeze majina mawili au matatu ya watu ambao tungependa wawemo katika kamati hiyo na tufanye kampeni kupitia vyombo mbali mbali vya habari vya Tanzania waongezwe kwenye kamati hiyo ili ripoti watakayoitoa isiwe na usanii wa aina yotote na ikubalike na Watanzania wote. Mmoja wa watu wa kuongezwa ni Issa Shivji. Wakati wa kukaa kimya wakati rasilimali zetu zinawatajirisha wageni umeshapita.
 
Mmoja wa watu wa kuongezwa ni Issa Shivji. Wakati wa kukaa kimya wakati rasilimali zetu zinawatajirisha wageni umeshapita.

Mkuu Bubu,

Heshima mbele mkuu, kwenye hili I am with you 100%, na sasa hivi ninai-forward hii post yako kwa wahusika, maana this one is pure politics za bongo.
 
Mimi nitaanza na mwakilishi kutoka wizara ya Sheria. Maria Kejo ambaye ametajwa ndio mkuu wa ufuatiliaji upatanishi wa mikataba, ndiye yule yule alituletea IPTL. Alikuwa akifahamika kama Mary Ndosi au Maria Ndosi.

Mama Ndosi-Kejo, ameshatuhumiwa kuwa mshirika wa kusaini mikataba bomu kupitia ofisi ya Waziri wa sheria akishirikiana na aliyekuwa waziri wa sheria Andrew Chenge. Aidha, anatuhumiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Lowassa (refer to posings from BCS Times on IPTL).

Huyu Mama Ndosi-Kejo ndio kachangia kabisa kuimaliza hii kamati ya madini. Na ukiuliza sababu ya kumweka humo sijui watasema nini mtu anayehusika na IPTL na uchafu mwingine wote!
 
Thank you so much FMES, in fact when I was posting that para I had you in my mind but I did not want to put you on spot. Once again thank you so much for your decision.
 
Mmoja wa watu wa kuongezwa ni Issa Shivji. Wakati wa kukaa kimya wakati rasilimali zetu zinawatajirisha wageni umeshapita.

Mkuu Bubu,

Heshima mbele mkuu, kwenye hili I am with you 100%, na sasa hivi ninai-forward hii post yako kwa wahusika, maana this one is pure politics za bongo.

Mkuu FMES,

Heshima mbele mkuu. Hapa sijui nicheke au niseme nini ila hii ya kuforwad jina kwa wahusika inafurahisha!
 
Huyo mama yake Frank Ndosi aka KizzoGunz ni fisadi kubuhu la kibuzwagi lililokubuhu lisilo na huruma na haya.
 
Huyo mama yake Frank Ndosi aka KizzoGunz ni fisadi kubuhu la kibuzwagi lililokubuhu lisilo na huruma na haya.

Kwa kiswahili kizuri ni Buzwagist yaani ni specialist la masuala ya kibuzwagi......kamati ipo tainted, na ni ya kifisadi!!.
 
Sioni kama kuna sababu ya kuanza kuwa na wasi wasi. Kwanza lazima tumpongeze Kikwete kwa kwenda kinyume na Lowasa mwasisi wa kumfukuza zito kijinga bungeni.

Pili pamoja na kuchelewa kuona kunahaja ya kutoa majibu kwa watanzania baada ya kilio kikubwa.

Swala la kwamba wanakamati wengine wanaweza kuwa na walakini sioni kama kuna shida hapa. Pamoja na kufanya kazi na wenzake(Zito) tayari wao (Chadema) wameshafanya utafiti mkubwa wa mikataba yetu ya madini inavyosainiwa kienyeji na kiwizi hiyo inamfanya Zito kuwa na kazi rahisi ya kwenda kuwakilisha kwenye kamati.

Vilevile kamati inachunguza mikataba kama ilifuata sheria za madini na kauli za raisi, hivyo hata kama huyo dada alishirikiana na Karamag ina kuwa rahisi kumuuliza jinsi walivyooandaa wizi wao kwenye hiyo mikataba waliosaini kwani kwa mtu makini ni rahisi sana kuona utumbo na ni vigumu sana kuficha uchafu.

Kazi iliopo ni jukumu la wanakamati kuamua kuisaidia nchi au kubeba walarushwa na mafisadi. Kila mmoja akifanya kazi yake vizuri tutapata majibu safi.

La msingi wasioneane aibu wala wasimbebe mtu. Wasitumie hulka za kisiasa bali wafanye kazi kwa misingi na taratibu za kamati.

Kabwe Zito hakikisha unatunza nyaraka zako zote zilizosainiwa na kila mjumbe wa kamati kila mnapomaliza kazi mojawapo ya kamati. Na hakikisha unaisoma riport ya mwisho na kuwa na kopi yako iliyosainiwa na wanakamati wote. Usikubali kuburuzwa usipopaelewa nenda kaulize wataalamu husika kutokana na mahitaji. wakati wa kamati ya minofu ya samaki Walibadilisha ripoti Lamwai akabaki anashangaa na kutokuamini. Kamti ni vita kamati ni kujisafisha. Hivyo kazi tunakupa ya kupeperusha bendera ya Tanzania.

Hongera Kikwete kwa hili.
 
Kamati au tume au whatever the heck waliita iliyokuwa inapitia mikataba ya madini wakati wa Buzwagi ukisainiwa London ilikuwa na tofauti gani na hii kamati mbovu ya Bomani, Mwakyembe, na Cheyo?

..mwafrika,

..ile haikuwa kamati[in the real sense]but kundi fulani la wahuni!au waliotiwa uhuni!

..hii nyingine tusubiri tuone!na hamu sana ya kuona kitakachojiri! watu wanatabirika!
 
Wabongo! mie kisha choka kabisa, sijui Rais afanye nini?, akifanya hili zuri basi linachochocholewa la mafisadi, Jamani kila kitu kinafanywa kwa muda wake!

Msishangilie kuwekwa kwa Zitto humo. Kama mnakumbuka JK alivyosema, tatizo sio mikataba ya madini, tatizo ni sheria zetu tulizojiwekea, HIZI SHERIA ZIMEPITWA NA WAKATI.

Kama kamati inapitia na kurekebisha sheria sawa, lakini msitegemee kamati zirekebishe mikataba!!!!!! Mama Kejo amekuwa akizunguka duniani kuangalia best practices, baada ya kumaliza sasa naamini atakuwa na inputs za maana kwenye kamati.

Kwahiyo wandugu msishangae Zitto wenu akiingia ndani na kutoka na kuwapa taarifa kuwa jamani mikataba ipo safi! Najua mtaanza kumrushia madongo kuwa kanunuliwa!! Mark my words mtasema tu nyie waafrika!

Mtasema kwasababu HAKUNA MIKATABA MIBOVU, ila SHERIA ZILIZOPO ZINAZOHUSIANA NA KODI NA MAPATO YA MADINI NDIO MBOVU.

Mwenye kuelewa aelewe mwenye kupinga tuuuuuuuuuuu aendelee.
 
Kamati zimekuwa nyingi sana,Na mpaka sasa sijaona mafanikio ya hizi kamati..Kuanzia kamati ya Rushwa ililyokuwa chini na mzee WArioba,Kamati ya kupendekeza mishahara ya wafanyakazi wa Umma,Kamati ya Kuchunguza Madai Ya Mengi na Manji.
Rais anatzakiwa aje ajieleze mbele za watu nini kimo ndani ya hiyo mikataba..
Mie siungu Kamati amabyo inakuwa siyo huru kwasababu inategemea terms of reference,wewe unadhani katika hiyo kamati hata kama zitto yumo itatoa pendekezo zaidi ya matakwa ya Muungwana??
Muungwana kawawahi wapinzani,Wanajipongeza sasa kwa sababu wameweza kumaliza tuhuma za ufisadi mapema kabla wapinzania hawajaja na jambo flan ambalo linaweza kusemwa leo..
 
Wakuu wote;

Nimesoma mpaka page 8 ya thread hii; nilichoona ni kwamba kuna uelewa tofauti wa madhumuni ya kuunda tume kama nilvyomsikia mh. Rais, nilivyomsikia Rais wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM, ni kwamba ataunda tume nyingine ya Madini [ku-replace ile ya mheshimiwa Masha ambayo ilikuwa tume ya Serikali] nia ikiwa kuangalia wapi kuna mapungufu kwenye sheria ya 1998 ya madini kiasi kwamba tunakosa kama nchi maslahi stahiki.

Kwangu mimi naiona Tume hii, kama tume ya kuangalia tunatoka wapi tuko wapi, na tufanye nini ili tuweze kufaidika na madini yetu.

Tume hii sio kwa ajili ya kumchunguza Mh. Karamagi na Wizara yake...

Tume hii sio kuchunguza kwa nini mkataba ulisainiwa London,

In short tume hii sio ya kuchunguza mkataba mmoja specific, lakini tume inaweza chunguza mkataba mmoja au michache kama case studies.

Hivyo ndivyo nilivyoelewa!!!

Ndio maana Mh. Rais akasema "sisi kama serikali tulikuwa tunaendelea na Mh. Masha nadhani bado anaendelea hata baada ya kuwa naibu waziri wizara ya mambo ya ndani, lakini wenzetu naona hawatuamini, sasa tumeamua kuenda tume ambayo itawakuwa inajumuisha watu wengine zaidi ikiwepo upinzani, ... au hata dini kama nili lazima", ila la dini tone yake ilikuwa ya utani)

Quote hiyo ya mh. Rais, sio exact kama alivyosema lakini content ilikuwa similar na hiyo.

So sio jambo jipya, ni wajumbe wapya!!! na Terms of Reference Pana zaidi, ambazo expected output ni utungaji wa sheria mpya ya madini kama ... tume hii itagundua kwamba loyalt ya sasa ya 3.0% ni ndogo, inatakiwa say 10%, na vingine na vingine etc...
 
Wana Jambo wenzangu salaam... Kwa kweli kamati ya JK ya madini na ile ya Bunge ya Richmond zinaashiria kuwa sasa CCM chini ya JK ndiyo wanaanza kazi rasmi ya kusafisha Tanzania. Tukubali kuwa JK alikuwa amebanwa mikono kwa sababu nyingi amabazo na uhakika zilikuwa juu ya uwezo wake (tukubali kuwa CCM alikuwa bado hajaipanga kisawasawa).... Uchaguzi tayari amepata NEC, viongozi mikoa, viongozi taifa, mpaka kwenye matawi.....Sasa kikubwa ni kuangalia wale waliokuwa wanapiga kelele kama walikuwa "genuine" au blah blah blah....Najua Zitto ana kazi kubwa ya kufanya na nina imani atapita kifua mbele... Mzee wetu Mapesa pia yumo kwenye kamati hizo na hivyo nina uhakika hatutarudi nyuma kuanzia sasa vita mbele....Wananchi tumpe JK ushirikiano hata kama wengine kama sisi ni upinzani, sasa wote tumekubali kuwa kuna mwanga mwisho wa pango.......
Mungu Ibariki Tanzania na Watu Wake......
 
Safi sana. Bunge limeumbuka kwa kumsimamisha Zitto kazi. Ameteuliwa kusimamia alichokipigania hata kabla ya kifungo chake kuisha.
 
Mwakyembe hapo kwenye kamati hana mashaka sana kwani yeye pia naona kama ni mtu anaetamani radical changes.
Zitto atumie mwanya huu huu kuwaadabisha wale wabunge waliomshupalia na kuwaonyesha kwamba walikua very wrong.Pia ktk kumshukuru na kumsifia rais amaanishe kweli kimaslahi kwa Taifa.

Cheyo na CCM ni damudamu hana la maana saana hata kama yuko kwenye kamati ya Uchumi na fedha.Ni lipi aliolofanya kule?Cheyo anapowekwa mahali na CCM ni utata sana.

Uhusianao wa huyu jamaa na CCM utakumbukwa vizuri sana kwenye uchaguzi wa Wabunge wa bunge la E.Africa.

Zitto atumie huu uteuzi kuonyesha alijua nini alichokua anaongea na kuwaprove wrong wabunge wote 274 wa ccm.
 
Wakuu wote;

Nimesoma mpaka page 8 ya thread hii; nilichoona ni kwamba kuna uelewa tofauti wa madhumuni ya kuunda tume kama nilvyomsikia mh. Rais, nilivyomsikia Rais wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM, ni kwamba ataunda tume nyingine ya Madini [ku-replace ile ya mheshimiwa Masha ambayo ilikuwa tume ya Serikali] nia ikiwa kuangalia wapi kuna mapungufu kwenye sheria ya 1998 ya madini kiasi kwamba tunakosa kama nchi maslahi stahiki.

Kwangu mimi naiona Tume hii, kama tume ya kuangalia tunatoka wapi tuko wapi, na tufanye nini ili tuweze kufaidika na madini yetu.

Tume hii sio kwa ajili ya kumchunguza Mh. Karamagi na Wizara yake...

Tume hii sio kuchunguza kwa nini mkapa ulisainiwa London,

In short tume hii sio ya kuchunguza mkataba mmoja specific, lakini tume inaweza chunguza mkataba mmoja au michache kama case studies.

Hivyo ndivyo nilivyoelewa!!!

Ndio maana Mh. Rais akasema "sisi kama serikali tulikuwa tunaendelea na Mh. Masha nadhani bado anaendelea hata baada ya kuwa naibu waziri wizara ya mambo ya ndani, lakini wenzetu naona hawatuamini, sasa tumeamua kuenda tume ambayo itawakuwa inajumuisha watu wengine zaidi ikiwepo upinzani, ... au hata dini kama nili lazima", ila la dini tone yake ilikuwa ya utani)

Quote hiyo ya mh. Rais, sio exact kama alivyosema lakini content ilikuwa similar na hiyo.

So sio jambo jipya, ni wajumbe wapya!!! na Terms of Reference Pana zaidi, ambazo expected output ni utungaji wa sheria mpya ya madini kama ... tume hii itagundua kwamba loyalt ya sasa ya 3.0% ni ndogo, inatakiwa say 10%, na vingine na vingine etc...

Jitahidi na wewe ndugu yangu, sijui kama wataelewa!!!!! Hawa jamaa wamechagua kutoeelewa milele!
 
Angeteua wote toka CCM tungesema tusitarajie jipya kwani ni walewale; kachanganya na wapinzani tunasema lengo ni kuwaziba midomo (kuwanunua). Afanye nini tena Rais? Kweli nafsi huridhishwa na kile inachotaka! Labda turudie uchaguzi mkuu!
 
"Mchawi mpe mwanao alee" waswahili wanasema. JK is try to play politics, this can be bad for CCM and the whole picture. I want to see if this kamati will agree each other on anything.
 
Back
Top Bottom