Zungu Pule said:Bro, huyu Upendo Msuya ni yupi? Kuna wakati fulani nikiwa bongo, Mzee mmoja wa "system" akawa ananipa stori kuhusu Kiongozi wa nchi anavyofanya mambo kienyeji. Akanipa mfano wa dada/mama mmoja ambaye (to the best of my memory) alikuwa anamiliki Antelope Safaris - kampuni ambayo ofisi zake ziko Millenium Tower, Kijitonyama. Huyu mama ilikuwa ateuliwe "within few days" kushika wadhifa fulani nyeti (based on the principle of camaraderie or personal affairs). I suspect ni huyu Upendo Msuya. Someone should know what I am trying communicate.
tanzania daima said:tume ya haki za binadamu yapata katibu mtendaji
tume ya haki za binadamu na utawala bora imepata katibu mtendaji mpya ambaye ni wakili wa kujitegemea, upendo msuya (50), aliyeapishwa na rais jakaya kikwete, jana ikulu.
msuya, mwenye uzoefu wa masuala ya sheria kwa zaidi ya miaka 25, aliteuliwa na rais kikwete kushika wadhifa huo, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na gad mjemmas, aliyeteuliwa kuwa jaji wa mahakama kuu ya tanzania mwishoni mwa mwaka jana.
Waliohudhuria sherehe fupi ya kuapishwa kwa msuya ni pamoja na makamu wa rais, dk. Ali mohamed shein, waziri mkuu, edward lowassa, waziri wa nchi ofisi ya rais (siasa na uhusiano wa jamii), kingunge ngombale-mwiru, waziri wa katiba na sheria, dk. Mary nagu, mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na utawala bora, jaji robert kisanga.
Viongozi wengine waliohudhuria katibu mkuu kiongozi (ikulu), philemon luhanjo, katibu mkuu wizara ya katiba na sheria, sazi salula, na mkurugenzi mkuu wa takukuru, edward hoseah, makamishna wa tume ya haki za binadamu na baadhi ya maofisa waandamizi wa tume hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuapishwa kwake, katibu mtendaji huyo mpya alisema moja ya masuala muhimu atakayoanza nayo ni kuhakikisha majukumu ya tume yanatangazwa vya kutosha kwa wananchi, ili wajue namna ya kuitumia katika matatizo ya ukiukaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora.
uzoefu wa kisheria na masuala ya utawala alionao msuya unatokana na kuwa hakimu mkazi katika mahakama za kivukoni na kisutu (1983-1991), mkurugenzi wa idara ya mahakama za mwanzo (1992- 1996), wakili wa kujitegemea (1996 hadi sasa), wakili wa serikali na msajili wa makampuni na masuala ya hatimiliki katika serikali ya botswana (1998 – 2004).
Swala la Jaji jundu tuliache sasa tujadili Jaji mpya kachaguliwa na Rais Kikwete anaitwa Catherine Opiyo amechaguliwa leo kwenda mahakama ya Rufaa.tupeni wasifu wake,dini yake, ameolewa au bado,kwanini kamchagua Mwanamke ameacha wanaume
Joka Kuu.
Vipi kuhusu Asha Rose Migiro kuna mtu aliwahi kuniambia ndio wa kwanza kuwa na PhD na alikuwa best student Udsm sina uhakika na hilo nalileta kwako kama changamoto.
Kuhani,
..kuna mama anaitwa Julie Manning alikuwa AG wakati wa Juliasi. nadhani wakati huo AG alikuwa pia ndiye waziri wa sheria.
..sijui ni katika mazingira gani Mama Manning aliondoka ktk wadhifa wa AG. baada ya hapo hakusikika tena, mpaka majuzi Mkapa alimpokuja kumpa kazi.
NB:
..inawezekana Julie Manning ndiyo mwanamke wa kwanza Mtanzania kuhitimu LL.B pale UDSM.
..Damian Lubuva alitokea wapi kabla hajawa AG? sakata ya OIC ndiyo ilimuondoa wizara ya sheria
...Kwanza kabisa naomba Kuhani uwe unafanya utafiti kabla ya kuandika au kuelezea mambo kadha wa kadha...Kama aliwahi kuapishwa kuwa Wakili, basi hakuwahi... pamoja na ukweli kuwa ana jina la kikristo nadhani alibadili dini.
Kuhani said:Na Lubuva kumbe ni OIC ndio the cause of his undoing pale Wizara ya Sheria, ha hahahaaaa aa duuu. Kwa nini walim-maindi sasa, hebu lete mchongo. Lakini ishu ya OIC kwani ilifika Wizara ya Sheria au iliishia Zanzibar halafu Bara wakaipiga buti, Lubuva alikuwa implicated vipi maskini ya Mungu.
By the way Lubuva aliwahi kuwa AG Zanzibar pia. Na kabla ya kuwa AG wa bara na waziri wa sheria alikuwa jaji Mahakama Kuu mwaka mmoja, around 1984. Kabla ya hapo sijui alikuwa wapi. Kwa hiyo the picture building up pale Justice ni kwamba Lubuva alimfuata Warioba, Warioba alimfuata Manning, Manning ndio atakuwa aliwafuata kina Fundikira and them, you know?
Sakata la OIC na Lubuva ilikuwaje?
Jokakuu,
Lubuva ni m-Bara wa Kondoa. Japo alikuwa Attorney General wa Zanzibar. Hivi unajua hata Jaji Mkuu Ramadhani alikuwa Jaji Mkuu Zanzibar? Na kabla ya kuwa Jaji Mkuu Zanzibar, Ramadhani alikuwa deputy Attorney General wa Lubuva. Kwa hiyo wa-Bara wawili walikuwa wana run the show at Justice in Zanzibar! Duuuh noma! Ila wenyewe wanapenda manake huwa wanaleta hata Wanaigeria wawe majaji! Sijui hakuna wataalam Zanzibar? Hivi Zanzibar ina watu wangapi anyway?
Wakina Mwiba wasije wakanirukia, lakini wenyewe Wanzanzibar wanapenda kupangiwa pangiwa sheria na ma aliens, kama ulivyo intimate, we utamletaje m-Nigeria awe jaji? Yani unawa dis wazawa wote kuwa hakuna anaefaa mpaka ulete wakuja?
By the way, according to "ze dataz" ni kwamba jaji mwanamke wa kwanza ni Mama Eusebia Munuo: "...Eusebia anasema April 1987, aliteuliwa kuwa jaji wa kwanza mwakamke katika Mahakama Kuu mkoni Arusha...Eusebia ambaye ni hakimu wa kwanza mwanamke Tanzania..." Unless wanamaanisha alikuwa jaji wa kwanza Arusha, simuelewi hapo mwandishi Happiness Katabazi wa Tanzania Daima (hiyo mi-typo yenyewe inakutia mtu mashaka na kile anachokisema.) Na kama Mama Mnuo ndio alikuwa jaji wa kwanza wa kike, je jaji mstaafu Mama Manning ambae pia AG in the 70's, alikuwa jaji lini?