Mwendabure
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 2,138
- 1,040
Kati ya Vingunge wa Magamba walioifikisha kaburini mikoa ya kusini hasa Lindi na Mtwara huyu Mama yumo. Nguvu yake ndani ya Chama cha Magamba ameielekeza ktk kuweka wabunge maboya majimbo ya kusini hasa majimbo ya Nanyumbu, Masasi na jimboni kwake Lulindi kwa maslahi ya chama chake badala ya maslahi ya wananchi. Majibu mnayo wenyewe Dastan Mkapa (nanyumbu) Bi Kasembe (masasi) Jerome Bwanausi (lulindi) alihakikisha anatumia ushawishi wake kuwapitisha hawa kwakuwa tu ni vibaraka wa chama na kuacha vijana wengine ndani ya chama ambao wanakubalika na wananchi wa majimbo haya tena bila kujali itikadi ya vyama. Mwaka 2005 kwa kushirikiana na mh. Ben waliweka kioja cha karne kwa kupitisha boya lile Suleiman Kunchaya kilichotokea ni aibu kwao na hadi leo hakuna aliyetayari hata kukumbuka kwa jinsi Kunchaya alivyokuwa mzigo kwa wakazi wa jimbo la Lulindi kwa kipindi chote cha miaka mitano alichokuwa mbunge. Kwa majimbo ya Masasi na Nanyumbu hali kadhalika Bibi huyu anayatia mkono atakavyo tena bila chembe ya haya wala huruma.
Sina chuki na Bibi huyu na natambua mchango wake japo kwa yale machache. Ila napenda nieleweke hapa kuwa, nguvu aliyonayo Bibi huyu kuanzia ndani ya chama na wakazi wa majimbo hayo niliyotaja na mikoa ya kusini kwa ujumla wake hajaitumia kwa maslahi na ustawi wa wananchi hasa bali kwa maslahi ya chama chake. Na hili lipo wazi hasa kwa wale waliowahi kuhudhuria mikutano yake ya hadhara alipokuwa mbunge wa Lulindi, akiwa huko hasa maeneo ya vijijini ni vitisho na kejeli kwa wale wote wanaojaribu kutofautiana na chama cha magamba na kuagiza washughulikiwe vilivyo kwa hali yoyote. Na kusahau kuwa wapo pia wasio wapenzi wala wanachama wa Magamba wamempigia kura.
Pia Bibi huyu kwa nafasi yake amechangia sana kukandamiza na kudumaza mawazo na fikra za wakaazi wa mikoa ya kusini hasa ktk majimbo hayo tajwa. Huwa anafikia hata kutamka kuwa watu wa kusini hawana asili ya upinzani yani si asili yao!
Huyu Bibi amechoka hana jipya na kwangu binafsi ni zaidi ya janga kwa mikoa ya kusini. Bibi huyu ni kati ya watu wanaojivunia mafanikia ya kuitosa mikoa ya Lindi na Mtwara ktk lindi la ufukara kwaajili ya vyeo vya kupewa kama hivi huku watu wa kusini wakilia na kusaga meno! Mbaya zaidi amefanikiwa pakubwa kupanda 'mfumomagamba' ambao umeshamiri kiasi itawachukua miaka dahari watu wa huko kujikwamua kutoka mfumomagamba. Hatufai na ni janga amechangia kuifilisi mikoa hii hasa KIFIKRA na KIMTAZAMO.
'Anyone with a gun plz!!