JK: Amkaba koo Waziri Ghasia

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Rais Jakaya Kikwete, jana alimweka katika wakati mgumu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia, baada ya kukatisha mara kwa mara hotuba yake akitaka maelezo ya kina kuhusu masuala yanayohusiana na wizara yake hasa mabilioni yanayotafunwa kutokana na mishahara ya watumishi hewa.

Rais Kikwete alianza kumhoji Waziri Ghasia kwanini mabilioni ya fedha ya watumishi hewa yanaliwa na wahusika hawachukuliwi hatua zozote na wanaendelea kuwa kazini. Alihoji swali hilo baada ya Waziri Ghasia kumweleza kuwa Sh. bilioni tisa zimeliwa katika wizara na idara mbalimbali na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inaendelea na uchunguzi.
Baada ya kauli hiyo, Kikwete aliingilia na kuhoji kwanini wahusika wasitafutwe wakarejesha fedha hizo na kisha wakafikishwa polisi ili waandaliwe mashtaka na kufikishwa mahakamani.

Waziri Ghasia aliposimama na kumweleza Rais Kikwete kuwa polisi na Takukuru wanaendelea na uchunguzi wa sakata hilo, Kikwete aliingilia kati tena na kumweleza kuwa suala hilo liko ndani ya uwezo wa wizara yake hivyo hawapaswi kuitupia mzigo Takukuru. “Hawa watumishi hewa wako wizara zote kwanini hamuwatafuti, maana fedha za umma zinazidi kupotea, Waziri hili liko ndani ya uwezo wenu msiwaachie Takukuru, mkiwaachia hao uchunguzi unaweza kukaa miaka na miaka huku wahusika wakiendelea kutafuna fedha za umma, mnaweza kusema mnaendelea na uchunguzi mkakuta wale wezi mnaowatafuta wengine wamekufa, wengine wameshastaafu haitakuwa na maana…Ni heri tutumie fedha nyingi kwa ajili ya kuwatafuta hawa wezi,” alisema na kuongeza: “Lakini tukomeshe kabisa tatizo hili na hata mkitumia milioni 200 sioni tatizo cha maana nataka tukomeshe wizi huu, na kama hamna fedha za kufanya kazi hiyo semeni mimi nitawapa tu.” Aliiagiza Wizara hiyo kuwasaka watumishi walioiba Sh. bilioni 9 za watumishi hewa ili wazirejeshe na kisha wafikiswe mahakamani.

Baada ya maelezo hayo ya Rais Kikwete, Waziri Ghasia alisimama na kuendelea kumweleza kuwa wizara yake imeanza mkakati wa kuwatafuta watu wanaolipwa mishahara ya watumishi hewa, lakini kabla hajafika mbali Rais Kikwete aliingilia tena kati na kumweleza kuwa watu hao wanafahamika kwa kuwa wako ndani ya utumishi wa umma. “Hawa watu mnawafahamu maana utakuta mwalimu kapelekwa mkoa fulani, lakini haendi, sasa hapo anatafutwa mtu wa kujifanya mwalimu na kuchukua mshahara wake, mtu anachukua jamaa yake au mkewe anamwambia ajaze fomu ili ajifanye ndiye yule mwalimu kwamba kisharipoti kazini sasa mshahara ukishaingia wanajuana wenyewe namna ya kulipana kati ya ofisa utumishi na yule aliyejifanya kuwa ndiye mwalimu,” alisema. “Waziri haya mambo yako ndani ya mamlaka yenu na hampaswi kukasimu mamlaka yenu, tafuteni kamateni watu hawa wachukulieni hatua za kinidhamu, kule Takukuru iwe baadaye kwa hatua zingine maana mkishawagundua wezi hawa hawapaswi kuendelea kuwa kazini.” Rais Kikwete alisema iwapo waziri huyo atawabana makatibu wakuu na wahasibu wakuu wa wizara wanaweza kuwataja watumushi wao wanaohusika na kuchukua mishahara ya watumishi hewa na kisha wawasimamishe kazi kwa hatua zaidi za kisheria.
“Wizara zote na kwenye halmashauri wabaneni hawa watawatajia wezi hawa ila kama mnaona hamna mamlaka nao nipeni kazi hiyo mimi na Luhanjo (Katibu Mkuu Kiongozi) tutafanya kazi hiyo maana hakuna aliye juu yetu, tutapambana nao, hatuwezi kuacha fedha za umma zinaendelea kuliwa kama shamba la bibi,” alisema Kikwete.

Waziri Ghasia aliendelea na hotuba yake akimweleza Rais Kikwete kuwa kumekuwa na tatizo la mrundikano wa watumishi wa umma kwenye ngazi moja bila kupanda vyeo hali iliyomfanya Kikwete kuingilia tena na kuhoji sababu ya kuwepo hali hiyo.
“Kwanini mnaruhusu hali hii, mtumishi kupanda cheo ni haki yake si hisani, hao wanaohusika na kupandisha vyeo watumishi wakishindwa kufanya hivyo washughulikiwe, msiwachekee watumishi wazembe maana mnasababisha malalamiko kila kukicha, fuatilieni kujua watumishi gani hawajapandishwa vyeo na mjue kwanini, mkishajua penye tatizo yule aliyeshindwa kutimiza wajibu wake mwandikieni barua atoe maelezo kwanini kashindwa kutimiza wajibu wake, asipojibu ndani wiki moja basi mumpandishe cheo yule mtumishi aliyecheleweshewa kupandishwa na yule mtumishi aliyezembea kwa kuwa mmefanya kazi yake mumpe adhabu kama kumshusha cheo,” alisema. Kikwete alimweleza Waziri Ghasia kuwa kuna baadhi ya viongozi wanashindwa kupandisha watumishi vyeo kwa chuki tu.
Katika hatua nyingine, Kikwete alithibitisha kuwa gharama za maisha zimezidi kuwa kubwa hivyo alimwagiza Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, kuangalia uwezekano wa kuwaongezea mishahara watumishi wa umma ili kuwapunguzia makali ya maisha.

TAMISEMI WANALEA WEZI
Akiwa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kikwete alisema baadhi ya watumishi wa wizara hiyo ndio wamekuwa wakilea wezi wa fedha za umma kwenye halmashauri nyingi.

Alimwagiza waziri wa wizara hiyo, George Mkuchika, kuhakikisha wanafuatilia matumizi ya fedha za serikali zinazopelekwa kwenye halmashauri kuangalia kama zimetumika ipasavyo. “Huku fedha zinatafunwa sana, maana ripoti zinaandikwa vizuri ila mambo hayajafanyika, mimi mwenyewe kule nyumbani kwangu waliandika kuwa wamejenga madaraja mawili, lakini kila wakati napita hapo sijawahi kuona hilo daraja waliloandika kuwa limejengwa, kuna wakati Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo aliwahi kutaka kuchunguza matumizi ya fedha aliandamwa kuanzia kule wilayani hadi huku juu Tamisemi, sasa inaonekana ninyi mnalea wezi acheni kabisa tabia hiyo,” alisema Rais Kikwete.
CHANZO: NIPASHE
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Yetu macho, tatizo hayo maagizo huwa yanaishia hapo hapo kwani hatuoni hatua zozote kwa hao jamaa tangu zamani!
 
Mchezo wa kuigizaa tu. Ina maana rais hana muda wa kupitia haya mambo na waziri mpaka aulize maswali wakati wa hotuba?

Au ndiyo mambo ya theater tu, anataka watu wamuone mkali, waseme big up JK, kesho wasahau, mambo yanaendelea vile vile.

Sasa kamuwajibisha nani? Kachukua hatua gani? Yaani rais analalamika kama mwananchi wa kawaida wakati ana nguvu zote za dola, huyu mtu anaelewa dhamana ya urais kweli?
 
Angemwajibisha waziri wake kwa kutokuwa makini katika wizara yake kingeeleweka
 
Hi ni kama zile semina elekezi za wakati akiingia madarakani, yetu macho. Sisi tunataka kuona action sio blabla za matembezi ya wizarani.
 
Haya jamani toka 2006 mpaka leo yanaonekana kuwa deal..........maagizo yasiyotekelezwa tumeyazoea sasa na yanaota ubongoni mwetu kama makovu ya sugu vile........

Hata hivyo anastahili pongezi kwa maagizo.....

Naomba mnisaidie wanajamvi......Je mkulu alishafika wizarani kwa Ngeleja? Je alimuambia awawajibishe waliotuingiza kwenye mikataba bomu inayoligharimu taifa kama ile ya Dowans na Richmond na mingine ambayo inagharimu zaidi ya hizo billioni 9 zilizoliwa na wafanyakazi hewa (japo nahisi zimeliwa na watendaji wake na sio wafanyakazi hewa)?

Kama hajapita, basi naomba mliokaribu nae mumuambie kama anataka tumuone wa maana na anamaanisha business akifika huko atoe agizo la kuwajibishwa kwao
 
Mheshimiwa Rais akiwa mkali hivi, nchi itatawalika na kusonga mbele. Ikiwezekana baada ya miezi 6 apitie tena hizo wizara kujua utekelezaji wake.
Mtu akifanya vizuri lazima tu appreciate bila kujali itikadi ya kisiasa
 
Hakuna Lolote hapo. Yeye ndio angekuwa wa kwanza kuwachukulia hatua wale mafisadi waliokwiba pesa zetu halafu yeye akawasamehe na kuwaruhus warejeshe pesa hizo bila kuchukuliwa hatua!!!
 
Rais Jakaya Kikwete, jana alimweka katika wakati mgumu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia, baada ya kukatisha mara kwa mara hotuba yake akitaka maelezo ya kina kuhusu masuala yanayohusiana na wizara yake hasa mabilioni yanayotafunwa kutokana na mishahara ya watumishi hewa.

Rais Kikwete alianza kumhoji Waziri Ghasia kwanini mabilioni ya fedha ya watumishi hewa yanaliwa na wahusika hawachukuliwi hatua zozote na wanaendelea kuwa kazini. Alihoji swali hilo baada ya Waziri Ghasia kumweleza kuwa Sh. bilioni tisa zimeliwa katika wizara na idara mbalimbali na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inaendelea na uchunguzi.
Baada ya kauli hiyo, Kikwete aliingilia na kuhoji kwanini wahusika wasitafutwe wakarejesha fedha hizo na kisha wakafikishwa polisi ili waandaliwe mashtaka na kufikishwa mahakamani.

Waziri Ghasia aliposimama na kumweleza Rais Kikwete kuwa polisi na Takukuru wanaendelea na uchunguzi wa sakata hilo, Kikwete aliingilia kati tena na kumweleza kuwa suala hilo liko ndani ya uwezo wa wizara yake hivyo hawapaswi kuitupia mzigo Takukuru. “Hawa watumishi hewa wako wizara zote kwanini hamuwatafuti, maana fedha za umma zinazidi kupotea, Waziri hili liko ndani ya uwezo wenu msiwaachie Takukuru, mkiwaachia hao uchunguzi unaweza kukaa miaka na miaka huku wahusika wakiendelea kutafuna fedha za umma, mnaweza kusema mnaendelea na uchunguzi mkakuta wale wezi mnaowatafuta wengine wamekufa, wengine wameshastaafu haitakuwa na maana…Ni heri tutumie fedha nyingi kwa ajili ya kuwatafuta hawa wezi,” alisema na kuongeza: “Lakini tukomeshe kabisa tatizo hili na hata mkitumia milioni 200 sioni tatizo cha maana nataka tukomeshe wizi huu, na kama hamna fedha za kufanya kazi hiyo semeni mimi nitawapa tu.” Aliiagiza Wizara hiyo kuwasaka watumishi walioiba Sh. bilioni 9 za watumishi hewa ili wazirejeshe na kisha wafikiswe mahakamani.

Baada ya maelezo hayo ya Rais Kikwete, Waziri Ghasia alisimama na kuendelea kumweleza kuwa wizara yake imeanza mkakati wa kuwatafuta watu wanaolipwa mishahara ya watumishi hewa, lakini kabla hajafika mbali Rais Kikwete aliingilia tena kati na kumweleza kuwa watu hao wanafahamika kwa kuwa wako ndani ya utumishi wa umma. “Hawa watu mnawafahamu maana utakuta mwalimu kapelekwa mkoa fulani, lakini haendi, sasa hapo anatafutwa mtu wa kujifanya mwalimu na kuchukua mshahara wake, mtu anachukua jamaa yake au mkewe anamwambia ajaze fomu ili ajifanye ndiye yule mwalimu kwamba kisharipoti kazini sasa mshahara ukishaingia wanajuana wenyewe namna ya kulipana kati ya ofisa utumishi na yule aliyejifanya kuwa ndiye mwalimu,” alisema. “Waziri haya mambo yako ndani ya mamlaka yenu na hampaswi kukasimu mamlaka yenu, tafuteni kamateni watu hawa wachukulieni hatua za kinidhamu, kule Takukuru iwe baadaye kwa hatua zingine maana mkishawagundua wezi hawa hawapaswi kuendelea kuwa kazini.” Rais Kikwete alisema iwapo waziri huyo atawabana makatibu wakuu na wahasibu wakuu wa wizara wanaweza kuwataja watumushi wao wanaohusika na kuchukua mishahara ya watumishi hewa na kisha wawasimamishe kazi kwa hatua zaidi za kisheria.
“Wizara zote na kwenye halmashauri wabaneni hawa watawatajia wezi hawa ila kama mnaona hamna mamlaka nao nipeni kazi hiyo mimi na Luhanjo (Katibu Mkuu Kiongozi) tutafanya kazi hiyo maana hakuna aliye juu yetu, tutapambana nao, hatuwezi kuacha fedha za umma zinaendelea kuliwa kama shamba la bibi,” alisema Kikwete.

Waziri Ghasia aliendelea na hotuba yake akimweleza Rais Kikwete kuwa kumekuwa na tatizo la mrundikano wa watumishi wa umma kwenye ngazi moja bila kupanda vyeo hali iliyomfanya Kikwete kuingilia tena na kuhoji sababu ya kuwepo hali hiyo.
“Kwanini mnaruhusu hali hii, mtumishi kupanda cheo ni haki yake si hisani, hao wanaohusika na kupandisha vyeo watumishi wakishindwa kufanya hivyo washughulikiwe, msiwachekee watumishi wazembe maana mnasababisha malalamiko kila kukicha, fuatilieni kujua watumishi gani hawajapandishwa vyeo na mjue kwanini, mkishajua penye tatizo yule aliyeshindwa kutimiza wajibu wake mwandikieni barua atoe maelezo kwanini kashindwa kutimiza wajibu wake, asipojibu ndani wiki moja basi mumpandishe cheo yule mtumishi aliyecheleweshewa kupandishwa na yule mtumishi aliyezembea kwa kuwa mmefanya kazi yake mumpe adhabu kama kumshusha cheo,” alisema. Kikwete alimweleza Waziri Ghasia kuwa kuna baadhi ya viongozi wanashindwa kupandisha watumishi vyeo kwa chuki tu.
Katika hatua nyingine, Kikwete alithibitisha kuwa gharama za maisha zimezidi kuwa kubwa hivyo alimwagiza Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, kuangalia uwezekano wa kuwaongezea mishahara watumishi wa umma ili kuwapunguzia makali ya maisha.

TAMISEMI WANALEA WEZI
Akiwa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kikwete alisema baadhi ya watumishi wa wizara hiyo ndio wamekuwa wakilea wezi wa fedha za umma kwenye halmashauri nyingi.

Alimwagiza waziri wa wizara hiyo, George Mkuchika, kuhakikisha wanafuatilia matumizi ya fedha za serikali zinazopelekwa kwenye halmashauri kuangalia kama zimetumika ipasavyo. “Huku fedha zinatafunwa sana, maana ripoti zinaandikwa vizuri ila mambo hayajafanyika, mimi mwenyewe kule nyumbani kwangu waliandika kuwa wamejenga madaraja mawili, lakini kila wakati napita hapo sijawahi kuona hilo daraja waliloandika kuwa limejengwa, kuna wakati Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo aliwahi kutaka kuchunguza matumizi ya fedha aliandamwa kuanzia kule wilayani hadi huku juu Tamisemi, sasa inaonekana ninyi mnalea wezi acheni kabisa tabia hiyo,” alisema Rais Kikwete.
CHANZO: NIPASHE

Porojo tu, haya tangu nazaliwa nayasikia na yanaishia kwenye majukwa. Amesema yameisha. Wanaoiba ni marafiki, ndugu etc, nani amfunge paka kengere. Acha waibe, CHUKUA CHAKO MAPEMA. mbona akina RA wamechukua chao mapema. MSINIUE
 
I wish him luck. lakini lazzima awe na nguzu za kuwatoa wanaoharibu, hasa wa ngazi za juu
 
jana nilicheka sana...eti anasema.....'' ni nani anapaswa kuwapandisha watu vyeo?'' ghasia akajibu ni yule plae.....ni wewe? yaani unatakiwa ukiwa unafika ofisin computa yako inaflash tu majina ya wanaopaswa kupandishwa vyeo......computa mnazo jamani zitumieni vizuri''

halafu jamani hivi hili swala la watumishi hewa ni mpaka atembelee wizara husika ndo ajue? hawa mawaziri huwa hawapeleki ripot?

alitakiwa amuwajibishe hapohapo huyo ghasia hayo sio majibu yeye kama waziri anashindwaje kuwawajibisha watu waliokula fedha za umma eti anangoja takukuru wawathibitishe!!mie ndio maana nasema always tatizo ni system nzima ya CCM na serikali yao na sio kikwete peke yake!!!yaani CCM wanatakiwa wasafishe hizo takataka zote!
Rais Jakaya Kikwete, jana alimweka katika wakati mgumu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia, baada ya kukatisha mara kwa mara hotuba yake akitaka maelezo ya kina kuhusu masuala yanayohusiana na wizara yake hasa mabilioni yanayotafunwa kutokana na mishahara ya watumishi hewa.

Rais Kikwete alianza kumhoji Waziri Ghasia kwanini mabilioni ya fedha ya watumishi hewa yanaliwa na wahusika hawachukuliwi hatua zozote na wanaendelea kuwa kazini. Alihoji swali hilo baada ya Waziri Ghasia kumweleza kuwa Sh. bilioni tisa zimeliwa katika wizara na idara mbalimbali na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inaendelea na uchunguzi.
Baada ya kauli hiyo, Kikwete aliingilia na kuhoji kwanini wahusika wasitafutwe wakarejesha fedha hizo na kisha wakafikishwa polisi ili waandaliwe mashtaka na kufikishwa mahakamani.

Waziri Ghasia aliposimama na kumweleza Rais Kikwete kuwa polisi na Takukuru wanaendelea na uchunguzi wa sakata hilo, Kikwete aliingilia kati tena na kumweleza kuwa suala hilo liko ndani ya uwezo wa wizara yake hivyo hawapaswi kuitupia mzigo Takukuru. "Hawa watumishi hewa wako wizara zote kwanini hamuwatafuti, maana fedha za umma zinazidi kupotea, Waziri hili liko ndani ya uwezo wenu msiwaachie Takukuru, mkiwaachia hao uchunguzi unaweza kukaa miaka na miaka huku wahusika wakiendelea kutafuna fedha za umma, mnaweza kusema mnaendelea na uchunguzi mkakuta wale wezi mnaowatafuta wengine wamekufa, wengine wameshastaafu haitakuwa na maana…Ni heri tutumie fedha nyingi kwa ajili ya kuwatafuta hawa wezi," alisema na kuongeza: "Lakini tukomeshe kabisa tatizo hili na hata mkitumia milioni 200 sioni tatizo cha maana nataka tukomeshe wizi huu, na kama hamna fedha za kufanya kazi hiyo semeni mimi nitawapa tu." Aliiagiza Wizara hiyo kuwasaka watumishi walioiba Sh. bilioni 9 za watumishi hewa ili wazirejeshe na kisha wafikiswe mahakamani.

Baada ya maelezo hayo ya Rais Kikwete, Waziri Ghasia alisimama na kuendelea kumweleza kuwa wizara yake imeanza mkakati wa kuwatafuta watu wanaolipwa mishahara ya watumishi hewa, lakini kabla hajafika mbali Rais Kikwete aliingilia tena kati na kumweleza kuwa watu hao wanafahamika kwa kuwa wako ndani ya utumishi wa umma. "Hawa watu mnawafahamu maana utakuta mwalimu kapelekwa mkoa fulani, lakini haendi, sasa hapo anatafutwa mtu wa kujifanya mwalimu na kuchukua mshahara wake, mtu anachukua jamaa yake au mkewe anamwambia ajaze fomu ili ajifanye ndiye yule mwalimu kwamba kisharipoti kazini sasa mshahara ukishaingia wanajuana wenyewe namna ya kulipana kati ya ofisa utumishi na yule aliyejifanya kuwa ndiye mwalimu," alisema. "Waziri haya mambo yako ndani ya mamlaka yenu na hampaswi kukasimu mamlaka yenu, tafuteni kamateni watu hawa wachukulieni hatua za kinidhamu, kule Takukuru iwe baadaye kwa hatua zingine maana mkishawagundua wezi hawa hawapaswi kuendelea kuwa kazini." Rais Kikwete alisema iwapo waziri huyo atawabana makatibu wakuu na wahasibu wakuu wa wizara wanaweza kuwataja watumushi wao wanaohusika na kuchukua mishahara ya watumishi hewa na kisha wawasimamishe kazi kwa hatua zaidi za kisheria.
"Wizara zote na kwenye halmashauri wabaneni hawa watawatajia wezi hawa ila kama mnaona hamna mamlaka nao nipeni kazi hiyo mimi na Luhanjo (Katibu Mkuu Kiongozi) tutafanya kazi hiyo maana hakuna aliye juu yetu, tutapambana nao, hatuwezi kuacha fedha za umma zinaendelea kuliwa kama shamba la bibi," alisema Kikwete.

Waziri Ghasia aliendelea na hotuba yake akimweleza Rais Kikwete kuwa kumekuwa na tatizo la mrundikano wa watumishi wa umma kwenye ngazi moja bila kupanda vyeo hali iliyomfanya Kikwete kuingilia tena na kuhoji sababu ya kuwepo hali hiyo.
"Kwanini mnaruhusu hali hii, mtumishi kupanda cheo ni haki yake si hisani, hao wanaohusika na kupandisha vyeo watumishi wakishindwa kufanya hivyo washughulikiwe, msiwachekee watumishi wazembe maana mnasababisha malalamiko kila kukicha, fuatilieni kujua watumishi gani hawajapandishwa vyeo na mjue kwanini, mkishajua penye tatizo yule aliyeshindwa kutimiza wajibu wake mwandikieni barua atoe maelezo kwanini kashindwa kutimiza wajibu wake, asipojibu ndani wiki moja basi mumpandishe cheo yule mtumishi aliyecheleweshewa kupandishwa na yule mtumishi aliyezembea kwa kuwa mmefanya kazi yake mumpe adhabu kama kumshusha cheo," alisema. Kikwete alimweleza Waziri Ghasia kuwa kuna baadhi ya viongozi wanashindwa kupandisha watumishi vyeo kwa chuki tu.
Katika hatua nyingine, Kikwete alithibitisha kuwa gharama za maisha zimezidi kuwa kubwa hivyo alimwagiza Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, kuangalia uwezekano wa kuwaongezea mishahara watumishi wa umma ili kuwapunguzia makali ya maisha.

TAMISEMI WANALEA WEZI
Akiwa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kikwete alisema baadhi ya watumishi wa wizara hiyo ndio wamekuwa wakilea wezi wa fedha za umma kwenye halmashauri nyingi.

Alimwagiza waziri wa wizara hiyo, George Mkuchika, kuhakikisha wanafuatilia matumizi ya fedha za serikali zinazopelekwa kwenye halmashauri kuangalia kama zimetumika ipasavyo. "Huku fedha zinatafunwa sana, maana ripoti zinaandikwa vizuri ila mambo hayajafanyika, mimi mwenyewe kule nyumbani kwangu waliandika kuwa wamejenga madaraja mawili, lakini kila wakati napita hapo sijawahi kuona hilo daraja waliloandika kuwa limejengwa, kuna wakati Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo aliwahi kutaka kuchunguza matumizi ya fedha aliandamwa kuanzia kule wilayani hadi huku juu Tamisemi, sasa inaonekana ninyi mnalea wezi acheni kabisa tabia hiyo," alisema Rais Kikwete.
CHANZO: NIPASHE
 
Kikwete anaumwa kiharusi mbona hawakamati Lowassa, Rosta aziz, karamagi, chenge na mramba kuwapeleka polisi maana hao ndio mafisadi papa. hana lolote kikwete
 
Big up JK

Hakuna cha kulisifia hapo!! Limeachia mabilioni yanaliwa ovyo ovyo tu leo ndo akomalie hizo zinazoliwa na watumishi, mbona ameshindwa kuchukua hatua katika mabilioni ya EPA mpaka leo hatujui kesi zimeishia wapi!! Hebu aache usanii hapa P*****f zake hana aibu!!!! Hata kama cup la babu limefanya mambo bado hatujaona, hebu awajibike zaidi.
 
” Rais Kikwete alisema iwapo waziri huyo atawabana makatibu wakuu na wahasibu wakuu wa wizara wanaweza kuwataja watumushi wao wanaohusika na kuchukua mishahara ya watumishi hewa na kisha wawasimamishe kazi kwa hatua zaidi za kisheria.

“Wizara zote na kwenye halmashauri wabaneni hawa watawatajia wezi hawa ila kama mnaona hamna mamlaka nao nipeni kazi hiyo mimi na Luhanjo (Katibu Mkuu Kiongozi) tutafanya kazi hiyo maana hakuna aliye juu yetu, tutapambana nao, hatuwezi kuacha fedha za umma zinaendelea kuliwa kama shamba la bibi,” alisema Kikwete.

Here we go again! Been telling one and all that Jakaya is MEGA-SMART upstairs. Eh there has a pen finally dropped; he knows what he wants and how to go about it - smart Eh!
 
Mchezo wa kuigizaa tu. Ina maana rais hana muda wa kupitia haya mambo na waziri mpaka aulize maswali wakati wa hotuba?

Au ndiyo mambo ya theater tu, anataka watu wamuone mkali, waseme big up JK, kesho wasahau, mambo yanaendelea vile vile.

Sasa kamuwajibisha nani? Kachukua hatua gani? Yaani rais analalamika kama mwananchi wa kawaida wakati ana nguvu zote za dola, huyu mtu anaelewa dhamana ya urais kweli?
Kiranga thank you for summarizing ambapo na mimi nilikuwa nataka kujenga hoja yangu
 
Back
Top Bottom