mabilioni yanayotafunwa kutokana na mishahara ya watumishi hewa.(1)
Rais Kikwete alianza kumhoji Waziri Ghasia kwanini mabilioni ya fedha ya watumishi hewa yanaliwa na wahusika hawachukuliwi hatua zozote na wanaendelea kuwa kazini(2).
Baada ya kauli hiyo, Kikwete aliingilia na kuhoji kwanini wahusika wasitafutwe wakarejesha fedha hizo na kisha wakafikishwa polisi ili waandaliwe mashtaka na kufikishwa mahakamani.(3)
Waziri Ghasia aliposimama na kumweleza Rais Kikwete kuwa polisi na Takukuru wanaendelea na uchunguzi wa sakata hilo, Kikwete aliingilia kati tena na kumweleza kuwa suala hilo liko ndani ya uwezo wa wizara yake hivyo hawapaswi kuitupia mzigo Takukuru. Hawa watumishi hewa wako wizara zote kwanini hamuwatafuti, maana fedha za umma zinazidi kupotea, Waziri hili liko ndani ya uwezo wenu msiwaachie Takukuru, mkiwaachia hao uchunguzi unaweza kukaa miaka na miaka huku wahusika wakiendelea kutafuna fedha za umma, mnaweza kusema mnaendelea na uchunguzi mkakuta wale wezi mnaowatafuta wengine wamekufa, wengine wameshastaafu (4).
Baada ya maelezo hayo ya Rais Kikwete, Waziri Ghasia alisimama na kuendelea kumweleza kuwa wizara yake imeanza mkakati wa kuwatafuta watu wanaolipwa mishahara ya watumishi hewa, lakini kabla hajafika mbali Rais Kikwete aliingilia tena kati na kumweleza kuwa watu hao wanafahamika kwa kuwa wako ndani ya utumishi wa umma.
Waziri haya mambo yako ndani ya mamlaka yenu na hampaswi kukasimu mamlaka yenu(5),
Wizara zote na kwenye halmashauri wabaneni hawa watawatajia wezi hawa ila kama mnaona hamna mamlaka nao nipeni kazi hiyo mimi na Luhanjo (Katibu Mkuu Kiongozi) tutafanya kazi hiyo maana hakuna aliye juu yetu, tutapambana nao, hatuwezi kuacha fedha za umma zinaendelea kuliwa kama shamba la bibi, alisema Kikwete.(6)
.
Katika hatua nyingine, Kikwete alithibitisha kuwa gharama za maisha zimezidi kuwa kubwa hivyo alimwagiza Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, kuangalia uwezekano wa kuwaongezea mishahara watumishi wa umma ili kuwapunguzia makali ya maisha.(7)
TAMISEMI WANALEA WEZI
Akiwa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kikwete alisema baadhi ya watumishi wa wizara hiyo ndio wamekuwa wakilea wezi wa fedha za umma kwenye halmashauri nyingi.(8)
CHANZO: NIPASHE
My take:
1. Kikwete kama waziri wa siku nyingi katika idara hajui kuwa pesa zinatafunwa hadi ashangae leo.
2. Yeye amewachukulia hatua gani wale wa Richmond, Kagoda, Meremeta, Tangold aliopelekewa majina na bunge
3. Jk amemfikisha nani mahakamani, na ile kamati yake ya kusimamia pesa za EPA imerudhisha kiasi gani
4. Mbona yale yaliyokuwa ndani ya uwezo wake hajafanya hata moja,na je si kweli yeye aliaachia watu wakastaafu wakiwa wezi
5. Kwanini Richomnd, EPA n.k alikasimu madaraka kwa Takukuru na tume ya luhanjo.
6. Haa!!! JK,shamba la bibi? lipi zaidi ya Richmond,EPA,Kagoda, Meremeta na Dowans. Please Mr President are you candid with your talk.
7. Kuongeza mishahara ni suluhisho la matatizo?, kipi bora kuongeza mishahara au kuzuia Inflation.Unataka twende sokoni na furushi
la pesa kununua mkate.! Uliwasiliana na wachumi wako kabla ya kusema haya Mheshimiwa Rais.
8. Haa! JK kuna mlezi wa wezi zaidi yako? hawa si wanafuata nyayo tu.
Conclusion: Huyu ndiye hasa JMK. Anajaribu kuonyesha kuwa anafanya kazi. Hakuna alichokisema ambacho yeye amewahi kufanya tofauti. Haya yote alipaswa kuongea na waziri wake katika vikao. Tulitaka tusikie mikakati ya kuboresha hali ya maisha ya wafanyakazi na si maswali na majibu.
Kama kawaida yake lengo lilikuwa kuonyesha kuwa anajali na anasilikiza shida za wananchi.
Utendaji kazi wa namna hii hautufikishi mahali popote. Huu ni usanii tu kuwalaumu mawaziri wake kwa kile asichokifanya. Yeye ndiye chanzo cha mfumuko wa bei, kulea wezi na utendaji mbovu. Kama angelikuwa makini Hawa Ghasia asingekuwa waziri tena, lakini si tunajua uwaziri ni suala la 'technical know who'