JK: Amkaba koo Waziri Ghasia

JK: Amkaba koo Waziri Ghasia

Objectivity ya JF ni sawa na ya binti ambae ndio kwanza amevunja ungo. Full kuendeshwa na hormones....emotions dont build countries. Education, innovation, enterprise, good governance, rule of law, sound economic and fiscal policy, increasing the franchise, those are the things that build nations.Jazba, one sided pessimistic subjective perceptions do not. JK kwa hili muungeni mkono akishindwa ku enforce kwa watumishi wake basi ndio mmlaumu. Radicals never really achieve anything. Ask Maximillien Robespiere .

Ndugu yangu sijui kama tupo katika ukurasa mmoja. Rejea wanachosema watu kwanza. Ni kuwa hakuna kipya JK asichokijua kuhusu watumishi hewa. Amekuwa hadi waziri wa fedha, sasa kama Rais hapaswi kuja kufoka kama mtu aliyeona miujiza.Alitakiwa aeleze solution.
Pili, anasema wezi wakamatwe, wapi hao ikiwa yeye ameshindwa kukamata majambazi na bado ameyakumbatia.
Anasema wasitegemee Takukururu, mbona yeye amezuia mambo mengi kwa mgongo wa takukuru.

Miaka 5 imepita eti anarudi kutathmini aliyoagiza 2005, tathmini ya sayansi gani hiyo hapa duniani. Jk anasema waongeze mishahara, haa! hajui kitu kinaitwa inflation!
Watu wana hasira kwasababu hakuna lolote, nchi ipo ipo haina dira, kila siku afadhali ya jana, halafu wewe unasema aungwe mkono ku enforce, kwa lipi la maana. Aungwe mkono kwa tabasamu na usanii katika maisha yetu.
 
Objectivity ya JF ni sawa na ya binti ambae ndio kwanza amevunja ungo. Full kuendeshwa na hormones....emotions dont build countries. Education, innovation, enterprise, good governance, rule of law, sound economic and fiscal policy, increasing the franchise, those are the things that build nations.Jazba, one sided pessimistic subjective perceptions do not. JK kwa hili muungeni mkono akishindwa ku enforce kwa watumishi wake basi ndio mmlaumu. Radicals never really achieve anything. Ask Maximillien Robespiere .
Tumuunge mkono usanii wake ama what are trying to say??, since 2006 amekuwa akicheza ngoma ile ile sisi tumeishazoea kuona ngonjera zake za kubwatuka kwenye TV ili imuongezee popularity stance baada ya hapo hakuna kinachoendelea, kama ku enforce angeanza na akina RA, NGELEJA na EL.
 
Rais Jakaya Kikwete, jana alimweka katika wakati mgumu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia, baada ya kukatisha mara kwa mara hotuba yake akitaka maelezo ya kina kuhusu masuala yanayohusiana na wizara yake hasa mabilioni yanayotafunwa kutokana na mishahara ya watumishi hewa.

Rais Kikwete alianza kumhoji Waziri Ghasia kwanini mabilioni ya fedha ya watumishi hewa yanaliwa na wahusika hawachukuliwi hatua zozote na wanaendelea kuwa kazini. Alihoji swali hilo baada ya Waziri Ghasia kumweleza kuwa Sh. bilioni tisa zimeliwa katika wizara na idara mbalimbali na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inaendelea na uchunguzi.
Baada ya kauli hiyo, Kikwete aliingilia na kuhoji kwanini wahusika wasitafutwe wakarejesha fedha hizo na kisha wakafikishwa polisi ili waandaliwe mashtaka na kufikishwa mahakamani.

Waziri Ghasia aliposimama na kumweleza Rais Kikwete kuwa polisi na Takukuru wanaendelea na uchunguzi wa sakata hilo, Kikwete aliingilia kati tena na kumweleza kuwa suala hilo liko ndani ya uwezo wa wizara yake hivyo hawapaswi kuitupia mzigo Takukuru. “Hawa watumishi hewa wako wizara zote kwanini hamuwatafuti, maana fedha za umma zinazidi kupotea, Waziri hili liko ndani ya uwezo wenu msiwaachie Takukuru, mkiwaachia hao uchunguzi unaweza kukaa miaka na miaka huku wahusika wakiendelea kutafuna fedha za umma, mnaweza kusema mnaendelea na uchunguzi mkakuta wale wezi mnaowatafuta wengine wamekufa, wengine wameshastaafu haitakuwa na maana…Ni heri tutumie fedha nyingi kwa ajili ya kuwatafuta hawa wezi,” alisema na kuongeza: “Lakini tukomeshe kabisa tatizo hili na hata mkitumia milioni 200 sioni tatizo cha maana nataka tukomeshe wizi huu, na kama hamna fedha za kufanya kazi hiyo semeni mimi nitawapa tu.” Aliiagiza Wizara hiyo kuwasaka watumishi walioiba Sh. bilioni 9 za watumishi hewa ili wazirejeshe na kisha wafikiswe mahakamani.

Baada ya maelezo hayo ya Rais Kikwete, Waziri Ghasia alisimama na kuendelea kumweleza kuwa wizara yake imeanza mkakati wa kuwatafuta watu wanaolipwa mishahara ya watumishi hewa, lakini kabla hajafika mbali Rais Kikwete aliingilia tena kati na kumweleza kuwa watu hao wanafahamika kwa kuwa wako ndani ya utumishi wa umma. “Hawa watu mnawafahamu maana utakuta mwalimu kapelekwa mkoa fulani, lakini haendi, sasa hapo anatafutwa mtu wa kujifanya mwalimu na kuchukua mshahara wake, mtu anachukua jamaa yake au mkewe anamwambia ajaze fomu ili ajifanye ndiye yule mwalimu kwamba kisharipoti kazini sasa mshahara ukishaingia wanajuana wenyewe namna ya kulipana kati ya ofisa utumishi na yule aliyejifanya kuwa ndiye mwalimu,” alisema. “Waziri haya mambo yako ndani ya mamlaka yenu na hampaswi kukasimu mamlaka yenu, tafuteni kamateni watu hawa wachukulieni hatua za kinidhamu, kule Takukuru iwe baadaye kwa hatua zingine maana mkishawagundua wezi hawa hawapaswi kuendelea kuwa kazini.” Rais Kikwete alisema iwapo waziri huyo atawabana makatibu wakuu na wahasibu wakuu wa wizara wanaweza kuwataja watumushi wao wanaohusika na kuchukua mishahara ya watumishi hewa na kisha wawasimamishe kazi kwa hatua zaidi za kisheria.
“Wizara zote na kwenye halmashauri wabaneni hawa watawatajia wezi hawa ila kama mnaona hamna mamlaka nao nipeni kazi hiyo mimi na Luhanjo (Katibu Mkuu Kiongozi) tutafanya kazi hiyo maana hakuna aliye juu yetu, tutapambana nao, hatuwezi kuacha fedha za umma zinaendelea kuliwa kama shamba la bibi,” alisema Kikwete.

Waziri Ghasia aliendelea na hotuba yake akimweleza Rais Kikwete kuwa kumekuwa na tatizo la mrundikano wa watumishi wa umma kwenye ngazi moja bila kupanda vyeo hali iliyomfanya Kikwete kuingilia tena na kuhoji sababu ya kuwepo hali hiyo.
“Kwanini mnaruhusu hali hii, mtumishi kupanda cheo ni haki yake si hisani, hao wanaohusika na kupandisha vyeo watumishi wakishindwa kufanya hivyo washughulikiwe, msiwachekee watumishi wazembe maana mnasababisha malalamiko kila kukicha, fuatilieni kujua watumishi gani hawajapandishwa vyeo na mjue kwanini, mkishajua penye tatizo yule aliyeshindwa kutimiza wajibu wake mwandikieni barua atoe maelezo kwanini kashindwa kutimiza wajibu wake, asipojibu ndani wiki moja basi mumpandishe cheo yule mtumishi aliyecheleweshewa kupandishwa na yule mtumishi aliyezembea kwa kuwa mmefanya kazi yake mumpe adhabu kama kumshusha cheo,” alisema. Kikwete alimweleza Waziri Ghasia kuwa kuna baadhi ya viongozi wanashindwa kupandisha watumishi vyeo kwa chuki tu.
Katika hatua nyingine, Kikwete alithibitisha kuwa gharama za maisha zimezidi kuwa kubwa hivyo alimwagiza Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, kuangalia uwezekano wa kuwaongezea mishahara watumishi wa umma ili kuwapunguzia makali ya maisha.

TAMISEMI WANALEA WEZI
Akiwa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kikwete alisema baadhi ya watumishi wa wizara hiyo ndio wamekuwa wakilea wezi wa fedha za umma kwenye halmashauri nyingi.

Alimwagiza waziri wa wizara hiyo, George Mkuchika, kuhakikisha wanafuatilia matumizi ya fedha za serikali zinazopelekwa kwenye halmashauri kuangalia kama zimetumika ipasavyo. “Huku fedha zinatafunwa sana, maana ripoti zinaandikwa vizuri ila mambo hayajafanyika, mimi mwenyewe kule nyumbani kwangu waliandika kuwa wamejenga madaraja mawili, lakini kila wakati napita hapo sijawahi kuona hilo daraja waliloandika kuwa limejengwa, kuna wakati Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo aliwahi kutaka kuchunguza matumizi ya fedha aliandamwa kuanzia kule wilayani hadi huku juu Tamisemi, sasa inaonekana ninyi mnalea wezi acheni kabisa tabia hiyo,” alisema Rais Kikwete.
CHANZO: NIPASHE
Jamaa amezinduka nini??????? Kikombe cha babu!!!!!!!!
 
Kamkaba koo lipi? Labda kama siku hizi kuna koo miguuni. Wizi mtupu wizi mtupu. Usitegemee jambo la maana kutoka huyu mtu zaidi ya 2015.
 
Yetu macho, tatizo hayo maagizo huwa yanaishia hapo hapo kwani hatuoni hatua zozote kwa hao jamaa tangu zamani!

Atuaeleze maagizo aliyotoa 2006 yametekelezwa kiasi gani na hatua gani zimechukuliwa kwa wasiotekeleza. Kwani kwenye baraza la mawaziri huwa wanaongelea nini!! mbona maagizo katika wizara nyingi anazotembelea inaonyesha kama vile hakuna communication kati ya raisi na mawaziri wake?
 
juha juha

nashindwa kuelewa mimi na wewe juha ni nani? Kifalsafa ku-appreciate kitu kizuri cha mtu ni alama ya intellectuals, sasa mimi niliye huru kimawazo ambaye ninaweza kumsifia mtu yeyote bila roho kuniuma au wewe uliyekubali mawazo yako kutawaliwa na mtu au chama fulani kwamba kumsifia mtu asiyetoka kwenye chama hicho we roho inakuuma! ZINDUKA
 
Ndugu yangu sijui kama tupo katika ukurasa mmoja. Rejea wanachosema watu kwanza. Ni kuwa hakuna kipya JK asichokijua kuhusu watumishi hewa. Amekuwa hadi waziri wa fedha, sasa kama Rais hapaswi kuja kufoka kama mtu aliyeona miujiza.Alitakiwa aeleze solution.
Pili, anasema wezi wakamatwe, wapi hao ikiwa yeye ameshindwa kukamata majambazi na bado ameyakumbatia.
Anasema wasitegemee Takukururu, mbona yeye amezuia mambo mengi kwa mgongo wa takukuru.

Miaka 5 imepita eti anarudi kutathmini aliyoagiza 2005, tathmini ya sayansi gani hiyo hapa duniani. Jk anasema waongeze mishahara, haa! hajui kitu kinaitwa inflation!
Watu wana hasira kwasababu hakuna lolote, nchi ipo ipo haina dira, kila siku afadhali ya jana, halafu wewe unasema aungwe mkono ku enforce, kwa lipi la maana. Aungwe mkono kwa tabasamu na usanii katika maisha yetu.

HTML:
Tumuunge mkono usanii wake ama what are trying to say??, since 2006 amekuwa akicheza ngoma ile ile sisi tumeishazoea kuona ngonjera zake za kubwatuka kwenye TV ili imuongezee popularity stance baada ya hapo hakuna kinachoendelea, kama ku enforce angeanza na akina RA, NGELEJA na EL.

Ni kweli kabisa anachofanya ni usanii kama sio matusi kwa watanzania kufikiri ni wajinga kiasi hicho wawe hawajamshtukia.
 
Mheshimiwa Rais akiwa mkali hivi, nchi itatawalika na kusonga mbele. Ikiwezekana baada ya miezi 6 apitie tena hizo wizara kujua utekelezaji wake.
Mtu akifanya vizuri lazima tu appreciate bila kujali itikadi ya kisiasa

Yaani mwenzetu unaona hapa Rais kafanya kazi ya maana??? Kweli Watanzania tuna safari ndefu!!!
 


Mi nina mashaka kidogo, kwa mfano hao wanaokwiba wanatumwa na maboss wao itakuwaje? Itabaki kuwa wimbo wa Taifa. Ni miaka mingi tu tunasikia habari hizi lakini sijawahi sikia watu wanachukuliwa hatua kihivyo,,
yetu macho ngoja tuwe na subira,,,,,
 
Hongera Mhe. Rais Jk kwa hatua hiyo. Nakuomba sisitiza suala la nyongeza ya mishahara kwa watumishi kwani hali halisi unaijua na wasimamie hao uliowaagiza waongeze mishahara na wasijifanye wameongeza mishahara. kwa nyongeza ya mishahara ya watumishi si tu utawapunguzia makali ya maisha watumishi hao bali hata wategemezi wao kwa kuzingatia asili yetu ya extended families. Hongera tena kwa mwandishi wa Post hii.
 
Back
Top Bottom