JK ametufanyia nini miaka hii 5 hadi tumchague? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK ametufanyia nini miaka hii 5 hadi tumchague?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ibrah, May 15, 2010.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Wadau, miaka 5 ya kwanza awamu ya Rais Kikwete iko ukingoni. Kila kiongozi hupimwa na mazuri na mabaya yake ili aweze kuaminiwa na kupewa kipindi kingine cha uchaguzi. Viongozi wa Taifa letu tangu uhuru wamekuwa 4 sasa na kila awamu imekuwa na jema la kujivunia ambalo imetuachia.

  Rais wa 1, Nyerere: Kaleta Uhuru na katuachia mshikamano na uzalendo ambao sasa unaporomoka

  Rais wa 2, Mwinyi: Katuletea soko huria na kutuondoa kwenye upungufu mkubwa wa bidhaa

  Rais wa 3, Mkapa: Alisaidia sana kuukuza uchumi wa nchi yetu, kuongeza mapato ya ndani, kurejesha nidhamu ya matumizi ya pesa za umma, kujenga mitandao ya barabara za lami, daraja la Mkapa na Umoja.

  Rais wa 4, Kikwete: Ametufanyia nini hadi sasa hivi ambalo angalau twaweza kumwamini kwa awamu nyingine?
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  May 15, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kikwete katufundisha udokozi katika mali ya Umma, kuoa wake wengi, katufundisha kula kwa mipaka ya kamba zetu shingoni, katufunza kupendelea kwa misingi ya kibaguzi, katufunza matusi, katufunza kuwa wakazi wapwani ni watu wenye akili isiyofaa kupewa madaraka makubwa ya nnchi, katupa somo kuwa IKULU SI MAHALA PATAKATIFU.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Cha kwanza alisema angetuletea Real Madrid -- hadi sasa hatujawaona!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sikubaliani na hii niliyoweka katika red. Angalau ungeongeza: 'mara tu baada ya kazi hii nzuri, aliuwageuka wananchi, akawasaliti ile mbaya kwa kufungua milango ya BoT na kuruhusu wachache kuiba mabilioni kwa raha zao!!!
   
 5. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  MIAKA MITANO YA SERIKALI YA AWAMU YA NNE:

  [​IMG]
  *TUMFUNDE NINI RAIS JAKAYA KIKWETE?

  Na Happiness Katabazi

  UONGOZI wa Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, umebakisha takriban miezi tisa kabla haujamaliza kipindi chake cha miaka mitano ambacho kimeainishwa katika Katiba ya nchi.

  Moja kati ya mambo aliyokuwa ameahidi Kikwete pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye kampeni za kuwania kiti cha urais ni kuwaletea Watanzania maisha bora pasi na kuainisha njia za kutekelezea ahadi hiyo ambayo sasa inaonekana ni kitendawili kikubwa kilichokosa mteguaji.

  Ni ukweli usiopingika kuwa ahadi hiyo na kauli mbiu ya Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya vilivyochangia kumpa ushindi wa kishindo alioupata mwaka 2005 na kuwabwaga washindani wake kutoka vyama vya upinzani.

  Ushindi huo haukupatikana kwa uraisi kutokana na kukabiliwa na upinzani mkali ndani na nje ya CCM, kundi la wanamtandao lililokuwa likiratibiwa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, ambao wanasemekana kuwa ‘maswahiba' wa Rais Kikwete ambao ndio waliokuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha mtandao wao unamuingiza mgombea wao Ikulu iwe kwa mbinu chafu au safi.

  Rais mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye kwa wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa CCM, alilazimika kumpigia kampeni Rais Kikwete hata kama alikuwa hajui ni mbinu gani zingetumika kutimiza ahadi ya maisha bora kwa kila Mtanzania; ahadi hizi za kwenye kampeni hizo ziligubikwa na mizengwe ya kila aina.

  Baada ya Kikwete kuingia madarakani wanamtandao waliofanikisha safari yake ya kuingia Ikulu walijikuta kila mmoja wao akizawadiwa kulingana na nafasi yake kwenye mtandao. Waliochangia fedha nyingi nafasi zao zilikuwa kubwa (uwaziri), waliouunganisha mtandao na kuufanya ufanikiwe wakaambulia vyeo serikalini, kuanzia ukatibu mkuu hadi ukuu wa wilaya.

  Waliokuwa kwenye jamii wakatupiwa mfupa wa kutafuna ulioitwa ‘mabilioni ya JK'.

  Hayo ndiyo yaliyokuwa matokeo ya maisha bora kwa kila Mtanzania. Aliyepata alipata na aliyekosa alikosa. Sandakalawe…amina!

  Leo CCM imeparaganyika siyo tena chama kile kilichomteua Kikwete akitetee kipate ushindi wa Tsunami, kuna makundi yanayowania nafasi ya urais wa nchi kwa udi na uvumba tena kwa kauli za kushtua na za kuulaumu utawala wa sasa kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo pamoja na kuwalea baadhi ya wanachama wenzao wanaodaiwa kuwa ni mafisadi.

  Si jambo la ajabu kwa makundi hayo kuibuka kwa kasi kipindi hiki na kudai nchi imekosa uongozi imara kwa kuwa baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Kikwete katika kipindi hiki cha miaka mitano kashindwa kuvunja makundi na kukiunganisha chama kwani bado kuna CCM mtandao ile ya wasio wanamtandao.

  Jambo jingine ni kushindwa kukiondoa chama na watu walio karibu naye katika kashfa mbalimbali za ubadhirifu wa fedha (ufisadi) unaoonekana kuwa wa kitaasisi zaidi kuliko ilivyofikiriwa mwanzoni kuwa ni utashi wa baadhi ya watu wenye tamaa za kuchuma mali kwa njia zisizo halali.

  Chama hivi sasa kinaonekana kukumbatiwa na baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa ni matajiri ambao kila wanachokisema ndicho kinachofuatwa hali ambayo imekifanya kipoteze sifa ile kilichojizolea siku nyingi kuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi ambao walihenya kukiimarisha chini ya utawala wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere.

  Lakini kubwa zaidi ambalo watu wamekuwa wakililalamikia ni kuwa serikali yao imegeuka kuwa ya kidhalimu; isiyojali wananchi wake hasa kwa kutekeleza sera ya ubinafsishaji, kubomoa bomoa nyumba, unyang'anyaji wa mali za watu bila fidia inayostahili.

  Cha kusikitisha zaidi hata zile ahadi tamu tamu walizokuwa wakipewa huku wakigaiwa fulana, kofia na khanga za kuisifu CCM, karibu zote zote hazijatekelezwa ipasavyo ikiwemo elimu bure kwa vijana hadi chuo kikuu, nyumba za serikali zilizouzwa kurejeshwa mikononi mwa serikali pamoja na maboresho makubwa ya sekta ya afya.

  Leo hii wale waliokuwa mstari wa mbele kusema kuwa ahadi hizo zingetekelezwa wamekuwa wakitembea vichwa chini kwa aibu kila wanapopita na kushuhudia umaskini unavyozidi kushamiri kadiri siku zinavyosonga mbele, elimu inavyozidi kushuka, nchi inavyozidi kutegemea misaada kutoka nje na mambo mengi ambayo kimsingi yanaondoa dhana nzima ya taifa kuwa huru.

  Utawala wa sasa unaweza kujivunia mafanikio ya kujenga na kuanzisha mahusiano mazuri na nchi nyingi duniani, baadhi ya sekta angalau naweza kusema zimeweza kupiga hatua za kimaendeleo, uhuru wa kutoa maoni kwa wananchi ambao umeainishwa kwenye Ibara ya 18(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, umepanuka kwa kiasi kikubwa chini ya uongozi wa Rais Kikwete kulinganisha na awamu zilizopita.

  Rais Kikwete, bado amezingirwa na kundi kubwa la wapambe wanaodai wanampenda na wanamshauri vizuri. Hawa baadhi yao leo nalazimika kuwaita ni ‘mbwa mwitu' waliovaa ngozi ya kondoo, kwa sababu wakati mwingine Rais anashindwa kuona uborongaji wa mambo unaofanywa na watendaji walio chini yake lakini wapambe hawa wanashindwa kumueleza ukweli badala yake wanabaki wakimsifia kwa kuteua watendaji wachapa kazi na makini ilhali wajua wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

  Aina hii ya wapambe haijaanza kwa Rais Kikwete pekee kwani ilianza katika Awamu ya Mwalimu Nyerere, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.

  Viongozi ama kwa kujua au kutokujua wamejikuta wakikubaliana na maelezo wanayopewa kila mara na wapambe hao ambapo wamekuwa wakijitahidi kujenga ukuta mkubwa kati ya viongozi na wananchi kwa hofu kuwa fursa hiyo ikipatikana wananchi wataeleza kila kitu kuhusu matatizo yao pamoja na utendaji usioridhisha.

  Nina hakika wapambe hawa hawataishia hapa hata kura zako (Kikwete) zitakapotosha katika kipindi chako cha pili cha kuliongoza taifa kwa miaka mitano mingine (2010-2015), ndipo utaanza kuona rangi halisi za wapambe na wale uliowapa madarakani kwa kuwa wanajua huwezi tena kuwania kiti hicho kulingana na matakwa ya Katiba.

  Wengi wao watajitenga nawe, licha ya baadhi yao hivi sasa kutokubaliana nawe; bali wanafanya hivyo kwa woga na unafiki hasa kutokana na nguvu uliyonayo katika kiti cha ukuu wa nchi, hawa watakusaliti na watakupaka matope na kila aina ya uchafu kiasi cha kufanya uchukiwe na jamii kama anavyoonekana Rais mstaafu, Benjami Mkapa.

  Najua wakati huo hutakuwa na nguvu ya kuwadhibiti kama ilivyo hivi sasa. Leo wanakuchekea na kukupamba kwa kuwa uko madarakani, lakini kesho watakukimbia na kukucheka huku wakikuzomea kwa yale waliyokushauri vibaya na ukayafuata.

  Ni vyema Kikwete ungesikia wosia huu ukabadilika kwa kuamua kuwa rais wa Watanzania wote . Kumbuka Watanzania walikuchagua uwaongoze siyo ugeuze urais kuwa ni kikundi cha watu wachache.

  Ni vyema pia rais wetu na serikali unayoingoza mngesikia wosia huu na kuamua kuwa watenda haki mkasimamia haki za wanyonge wa nchi hii badala ya hao mafisadi na matajiri wanaodaiwa kuwa na ushawishi mkubwa kwako. Hivi kweli utakapoondoka Ikulu hizo kampuni za madini ambazo serikali inaonekana kuzitetea na kuzilinda kwa gharama kubwa zitayaenzi yale yote uliyozifanyia?

  Ni vyema Kikwete ukayatafakari yanayoendelea kumpata mtangulizi wako Rais mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye wakati anakaribia kustaafu na alivyostaafu alijikuta anakabiliwa na wimbi kubwa la kashfa dhidi ya serikali yake na familia yake ambazo ziliibuliwa na kuenezwa na kukuzwa na vyombo vya habari na wale waliokuwa baadhi ya wapambe wake wa karibu ambao aliwaamini na kuwapenda.

  Wapambe hao wengine walikuwa ni wataalamu wa fani mbalimbali; walimshauri baadhi ya sera ikiwemo ile ya uuzwaji wa nyumba za serikali, ubinafsishaji; Rais Mkapa bila kujua alikuwa akitegwa na mbwa mwitu hao aliidhinisha sera hizo zitumike lakini mwisho wa siku walimgeuka na kuanza kumcheka na kumpakazia kwamba ameuza nchi na nyumba za serikali.

  Na hata wewe Rais Kikwete ambaye wakati Mkapa akiwa madarakani, ulikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, sera hizo wakati zinapitishwa ulikuwa ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri, ulizikubali. Na bado ningali nikikumbuka mwaka 2005 ulivyokuwa ukiomba kura uliwaahadi wananchi kuwa wakikuchagua utazirejesha nyumba hizo serikalini lakini hadi sasa bado ahadi hiyo inaonekana mwiba kwako na kwa watendaji wako.

  Na kwa tafsiri ya ahadi hiyo, wewe ulikuwa ukiikosoa kinyumenyume sera hiyo ya uuzwaji wa nyumba za serikali kwa watumishi wake iliyoasisiwa na serikali ya Mkapa hali iliyopelekea wananchi wakuone wewe ni shujaa na Mkapa akaonekana ni kiongozi asiye mzalendo kwa taifa lake na fisadi wa kupindukia.

  Baadhi ya wananchi wasiotaka kutafuta ukweli na kuchambua mambo kwa kina wanaendelea kumchukia Mkapa, utafikiri hakuwahi kufanya jema hata moja katika utawala wake.

  Jambo hilo ni hatari kwa usalama wa taifa letu siku za usoni kwani mtindo huu wa wanasiasa uchwara wasiotaka kutumia nguvu ya hoja kupinga maamuzi yaliyochukuliwa na wanasiasa wenzao matokeo yake wanaamua kutumia uzushi na majungu kwa kushirikiana na baadhi ya waandishi ‘wachumia tumbo' na kuanza kuchapisha baadhi ya habari za uongo dhidi ya viongozi tena wakubwa wa nchi hii, tukae tukijua ipo siku hao wanaochafuliwa kwa uzushi uvumilivu utawashinda kwani nao ni binadamu hawajatolewa nyongo, nao watajitokeza hadharani kuanika wanachokijua, ni wazi nchi haitakalika.Tusifike huko.

  Mwisho ni vyema Rais Kikwete ujue kwamba Tanzania haina uongozi wa kichifu au usultani inapotokea watoto wa rais kwa kipindi kifupi tu wanatumia jina la rais kupewa madaraka kwenye chama kinachoongozwa na baba yao, tabia kama hiyo ni chanzo cha udhaifu mkubwa kwa rais mwenyewe na ishara ya kutokuwa makini.

  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika

  0716 774494
  Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Januari 17 mwaka 2010  JK aeleza mafanikio katika elimu  Wednesday, 21 April 2010 06:55  Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali ya Awamu ya Nne imefanikiwa kuwezesha asilimia 96 ya watoto wenye umri wa kwenda shule kuwa darasani kutoka asilimia 35 miaka sita iliyopita.
  Rais Kikwete alisema hayo juzi jioni Jijini New York katika hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa kwa ajili ya kuzindua rasmi Mfuko wa Elimu Tanzania.
  "Mafanikio yetu ya kwanza yametokana na kuweza kuandikisha watoto kujiunga na elimu ya msingi na kuhakikisha kila mtoto anayetakiwa kuwa shule anakuwa darasani, miaka 6 iliyopita asilimia 35 ya watoto Tanzania ambao walitakiwa kuwa darasani walikuwa mitaani au wapo katika ajira," aliwaambia waalikwa waliohudhuria chakula hicho na kuongeza:
  "Tumefanikiwa kuandikisha watoto shuleni kwa asilimia 96 na tumedhamiria kuwapeleka wote shuleni."
  Mfuko wa Elimu Tanzania, ni Shirika lisilo la Kiserikali lililoanzishwa na marafiki wa Tanzania wa Kimarekani kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.
  Kwa miaka minne sasa Serikali ya Awamu ya Nne imefanya jitihada kuhakikisha sekta ya elimu hapa nchini inaboreshwa na kuimarishwa. Kwa kuzingatia hayo , bajeti ya sekta ya elimu imekuwa ikiongoza kwa ukubwa nchini ili kuhakikisha kuwa malengo ya msingi ya Awamu ya Nne yanafanikiwa.
  Rais alielezea mafanikio makubwa yaliyofikiwa ambapo mwaka 2000, Tanzania ilikuwa na shule za sekondari 927 na hadi kufikia mwaka 2009 shule hizo zimeongezeka kwa asilimia 400 na kufikia idadi ya shule 4,102.
  Aliyaelezea mafanikio mengine kuwa ni mwaka 2006 na 2009, jumla ya shule za sekondari 2,377 zilijengwa na hivyo kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka 524,325 mwaka 2005 hadi kufikia wanafunzi milioni 1.6.
  Rais Kikwete alikamilisha ziara yake ya kikazi nchini Marekani na alitarajia kurejea nchini
  http://tzlivenews.com/blogs/blog/4338-jk-aeleza-mafanikio-katika-elimu.html

  SOMA ILANI YA CCM:
  View attachment mafanikioilani.pdf
   
 6. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  katuletea maisha bora na ajira
   
 7. G

  Godwine JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  wengine watamchagua kwa kitendo chake cha kutaka kuwatawanya wafanyakazi kwa vifaru, na kutoa ahadi ya kama wakigoma basi wengine atawapoteza na kutumia majeshi kuzima juhudi za wafanyakazi kutaka maisha bora, kwani wafanyakazi hawajui maisha bora ni kwa wakubwa tuu wao hayawahusu kwani wakulima na wafanyakazi ni watwana tuu.

  hii ndio bongo
   
 8. M

  Mkono JF-Expert Member

  #8
  May 16, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mimi siwezi kuwa mnafiki, kama orodha ya wagombea kiti cha urais itakuja kwa sura ile ya mwaka 2005 haitakuwepo sababu ya mimi kuhoji iwapo JK anafaa ama kinyume chake,Hata kama KIKWETE anaharibu kwa wale aliogombea nao uchaguzi uliopita yeye ndo anaendelea kuwa bora ya....
   
 9. S

  Smartgirl New Member

  #9
  May 17, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kuna jambo ambalo anaweza akajipiga kifua kwamba kalifanya kwa usahihi, ukamilifu
  na uaminifu wote kweli?!!!!!!!!!!!!!!!!!!? sijui!!!!!!!!!
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  May 17, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  haha hahaha Rais wetu msaniii jamani tunakuwa kama hatumjui..
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  May 17, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Kuna watu huwa mnakosa vya kuandika ..maisha bora na ajira ziko wapi????????????????????
   
 12. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #12
  May 17, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Pamoja na kuongea humu jamani tarehe 22 mkajiandikishe woote humu ndani na familia zetu tumtoe huyu jamaa inawezekana. Nimechoka kumsikia huyu jamaa katufanyia uhuni huuu.
   
 13. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #13
  May 17, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  JK amefanya yafuatayo miongoni mwa mengi.
  1.Kasaidia kuongeza umasikini miongoni mwa watanzania
  2. Kaongeza kima cha chini kwa TZS 4,000.00
  3. Kasaidia kuitangaza nchi kwa kusafiri mara nyingi nchi za nje
   
 14. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #14
  May 17, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  amefanya mengi tu wakuu.
  1. ametembelea nchi nyingi sana duniani kwa pesa ya wananchi
  2. amekuwa mzembe kiasi cha kuongeza maisha magumu kwa watz
  3. amewaficha mafisadi wa epa ka kuwasamehe makosa yao wakileta pesa walizoiba, wakati watz wanaoiba kuku wanawekwa ndani
  4. anazidisha msambatiko wa jamii nchini kwa kulea mambo yanaoongeza udini nchini
  5. amewatembelea watz masikinni vijijini bila kuwasaidia lolote ili wamuone yeye ni mtu wa watu...
  6. amekuwa mwongeaji mzuri vitendo vichache...
   
 15. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #15
  May 17, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kushusha thamani ya shilingi toka 1000 hadi 1400 kwa dola 1
   
 16. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #16
  May 17, 2010
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,274
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kapewa jezi ya real madrid...
  Kapiga picha jukwaani na bi kidude
  Amekuwa raisi wa kwanza kujitangaza hadharani kuwa ahitaji kura za wananchi(wafanyakazi)
   
 17. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #17
  May 17, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Kaalika bongofleva ikulu.
  Kawa rais wa kwanza mke wake kutembea na msafara
  mke wake anafanya kazi za uma wakati hatuja mwajiri
  amekuwa na seriksli kubwa kuliko waliomtangulia
  rais wa kwanza kubadilisha magari ya ikulu
   
 18. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #18
  May 17, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  yeah analysis nzuri sana, umemuumba katika sura zake hasa.
   
 19. m

  mtoto wa mjini JF-Expert Member

  #19
  May 17, 2010
  Joined: Jan 18, 2010
  Messages: 1,536
  Likes Received: 679
  Trophy Points: 280
  Ametupa uhuru wa kulalama.
   
 20. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #20
  May 17, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  Mi nadhani Ben Mkapa ndo aliwaficha mafisadi. Japo bado kuna Usanii kwa bwana JK japo tumeona sanaa ya washukiwa wachache kufikikishwa mahakamani na kulala gerezani. Ni mwanzo mzuri . Ukiwa ndani ya boksi inahitaji guts , uzalendo wa taifa na kuweka maslahi ya chama pembeni.
   
Loading...