Salaam wana JF!
Katika muendelezo wa tamthilia ya Pesa za Jairo, waziri mkuu leo bungeni amesema kwamba utaratibu wa kumpeleka ndugu Jairo likizo ili kupisha uchunguzi wa kamati teule ya bunge umeanza kuratibiwa na muhishiwa rais.Waziri mkuu amesema hayo wakati akijibu swali la papo kwa hapo la kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni. Katika swali la msingi, ndugu Mbowe alimuuliza waziri mkuu kwamba, je, serikali haioni kwamba ni wakati muafaka kumrudisha ndugu Jairo likizo tena ili apishe uchunguzi wa kamati teule ya bunge?
Katika swali la nyogenza ndugu Mbowe akamuuliza waziri mkuu kwamba, kutokana na majibu ya katibu mkuu kiongozi, ndugu Luhanjo kwamba utaratibu wa uwezeshaji wa bajeti katika wizara ni wa kawaida, je, waziri mkuu unataka kusema hii ndio sera ya serikali? (ndugu Mbowe alitoa mifano ya uwezeshaji huo kwa ofisi ya waziri mkuu na wizara ya Jairo) Hapo waziri mkuu akaleta porojo za siasa, kwamba hilo suala tuiachie kamati teule. Yaani anasahau kwamba hiyo kamati teule ni ya kuchunguza wizara moja tu!