Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,199
- 1,969
Tunakumbuka jinsi JK alivyodai kwamba hazitaki kura za wafanyakazi wa Tanzania na kwamba hata kama wakigoma MIAKA NANE (8) wasingeweza kuongezewa mishahara! Lakini muda si muda JK pamoja na wasemaji wake walitushangaza kwa kudai kwamba eti JK hakusema maneno hayo na kabla vumbi halijatua JK aliwaahidi wafanyakazi eti "atawaongezea mishahara" na kweli aliwaongezea! Mpaka sasa Dkt Slaa anakusudia kupeleka pingamizi kwa msajili wa vyama vya siasa dhidi ya JK kwa "kuwahonga" wafanyakazi ili apigiwe kura!
Ni vifungu gani basi vilivyovujwa?
Kifungu cha 21 (1) (a) cha Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010 ambacho kinazungumzia "matendo yaliyokatazwa" kinasema kwamba:
"Kila mtu ambaye kabla au wakati wa kipindi cha kampeni, moja kwa moja au kwa namna nyingine yoyote, kupitia kwa mtu mwingine yeyote au kwa niaba yake, anatoa, anakopesha au anakubali kutoa au kukopesha, au anatoa, anaahidi au kumpatia au anajaribu kumpatia fedha yoyote au kitu chochote chenye thamani, mpiga kura au kwa ajili ya mtu yeyote kwa niaba ya mpiga kura yeyote au kwa ajili ya mtu mwingine yeyote kwa nia ya kumshawishi kupiga kura, au kuacha kupiga kura au kumrubuni mtu yeyote kutendo hicho kwa niaba ya mpiga kura huyo kupiga kura au kuacha kupiga kura katika kura za maoni au uchaguzi wowote."
Kifungu cha 24 (2), (7) kinasema:
"Mgombea yeyote ambaye, yeye mwenyewe, wakala wake au chama chake kitafanya kitendo ambacho kimekatazwa atakuwa au kitakuwa kimepoteza sifa za kushiriki katika kura za maoni na uchaguzi. Endapo mgombea au wakala wake au chama chake cha siasa atafanya kitendo ambacho kinapelekea kuwa ni kitendo kilichokatazwa na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaweza kufungua kesi ya jinai au kesi ya uchaguzi dhidi ya mgombea huyo."
ADHABU: Mgombea atatozwa faini isiyozidi milioni moja. (Kifungu cha 26 (b))
Kwa maoni yangu, JK anatakiwa akae pembeni ili watu wenye sifa za kugombea waendelee na mchakato wa uchaguzi! Msajili wa Vyama vya Siasa achukue hatua zinazostahili na kama hajachukua hatua hizo basi Mwanasheria Mkuu amfikishe mahakamani kama Sheria inavyosema!
Tujadili!