JK aitabiria CCM kifo

Mtahangaika sana kupotosha na kuchochea chuki dhidi ya jk, ila hamtaweza
 
Sijawahai kusema lakini leo nasema kwamba "NAMPONGEZA RAIS KWA MANENO HAYO" JK anajua mwaka 2010 alipita kwa mbinde ndio maana anawatahadharisha wana ccm juu ya tabia zao mbaya.Kikwetu umenena.Big up
 
Hivi si kuna mwenzao mmoja alishasema kuwa CCM imeoza?

JK anapoteza muda wa kuongea tu hiki chama kilishaoza siku nyingiiiii,sema watu walikuwa kwenye usingizi wa pono tu!

Sasa watanzania wameanza kujitambua!
 
It is just a matter of time, time will tell where ccm will be in 10 years time
 
mkuu nipe huo mbadala unaouona wewe. maana naona umeamua kunishambulia kweli kweli. mimi sijauona.

Asiye jitambua wewe. Nchi inawezaje kukaa utupu (nina maana ya uogozi). Ina maana huko ktk box ambalo huwezikujitoa mwenyewe? Inaonekana upo hapa jf muda mlefu lakini haijakusaidia kubadirika kimawazo. Sorry for attacking you! hii nikwasababu wapo watanzania wengine kama wewe lakini hawafikiri mbadala wa matatizo yanayorikabili taifa.

Lakini pia ni megudua wengine ni magamba waliokata tamaa, hivyo wanachokifanya sasa ni kukatisha tamaa wengine waone hakuna tena mbadala baada ya wao kushindwa. Hii roho razima kuikemea ikiwezekana hata katika majukwaa ya siasa ( of course I will do)
 
Mtakufa ninyi' mtaiacha CCM madarakan

Je, unapingana na Mwenyekiti wako (Kikwete)? Kama ndivyo basi tuambie wewe una maoni gani juu ya hiyo kauli ya JK...suala la kufa na kuiacha CCM linaingiaje hapa wakati JK mwenyewe amesishasoma alama za nyakati na kuujua ukweli? Kama wewe una akili kuliko mwenyekiti wako, tetea hoja sio unaropoka tu kama bwabwa halafu unaondoka bila kueleza kitu chochote!
 
Ccm kufa ni Sawa na kukauka bahari mtaendelea kusubiri sana bahari ikauke muingize magari kwenda zanzibar kwa barabara
 
tetesi ni kwamba 2015 majengo yote tuliyodhulumiwa na ccm tutarejeshewa , OFISI NDOGO LUMUMBA kugeuzwa kuwa MACHINGA COMPLEX !
 
Hao ndivyo walivyokuwa tangu zamani ila hatukujua maovu ya ccm kwa sababu hapakuwepo Cdm,waliokuwepo enzihizo akina Mtikila,Mrema,Zitto wa Cuf Hamad Rashid,Hashim Rungwe,Seif Sharif Hamad nawachumia tumbo engine ambao kaziyao ilikuwa nikula Rushwa pale wagunduapo inshu
 
Rais Kikwete ametoa utabiri huo wakati wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa CCM huko mkoani Mbeya. Alisema kwamba chama kimekithiri kwa ufisadi, dhuluma, rushwa, hongo, umangimeza na vitendo vingi vichafu suala ambalo linapunguza imani ya wananchi kwa chama na serikali.

JK alionya kwamba endapo chama hakitachukua hatua za makusudi kujisafisha, hakitavuka 2015 na akawatahadhalisha wanachama wake kujiandaa kisaikolojia kuchukua nafasi ya chama kikuu cha upinzani baada ya uchaguzi wa mwaka 2015--kwa kuwa haoni dalili za chama kujirekebisha na kurejesha mvuto kwa watanzania kabla ya uchaguzi ujao.

Akihojiwa na idhaa ya kiswahili ya BBC leo asubuhi, kada maarufu wa CCM na ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya madini, Bw Richard Kasesela, alikiri kwamba sasa hivi CCM ni kama gulio--mwenye pesa ndiye anayenunua uongozi. 'Watu wanatembeza pesa makanisani na misikitini mchana kweupe bila kuhojiwa wamezipataje hizo fedha', alihoji Bw Kasesela.

MY TAKE:
Ni afadhali wanaCCM mmeamua kusema ukweli. Vzr sana!

Safi sana kaka richad baambie
 
Back
Top Bottom