JK aitabiria CCM kifo

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
22,378
19,212
Rais Kikwete ametoa utabiri huo wakati wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa CCM huko mkoani Mbeya. Alisema kwamba chama kimekithiri kwa ufisadi, dhuluma, rushwa, hongo, umangimeza na vitendo vingi vichafu suala ambalo linapunguza imani ya wananchi kwa chama na serikali.

JK alionya kwamba endapo chama hakitachukua hatua za makusudi kujisafisha, hakitavuka 2015 na akawatahadhalisha wanachama wake kujiandaa kisaikolojia kuchukua nafasi ya chama kikuu cha upinzani baada ya uchaguzi wa mwaka 2015--kwa kuwa haoni dalili za chama kujirekebisha na kurejesha mvuto kwa watanzania kabla ya uchaguzi ujao.

Akihojiwa na idhaa ya kiswahili ya BBC leo asubuhi, kada maarufu wa CCM na ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya madini, Bw Richard Kasesela, alikiri kwamba sasa hivi CCM ni kama gulio--mwenye pesa ndiye anayenunua uongozi. 'Watu wanatembeza pesa makanisani na misikitini mchana kweupe bila kuhojiwa wamezipataje hizo fedha', alihoji Bw Kasesela.

MY TAKE:
Ni afadhali wanaCCM mmeamua kusema ukweli. Vzr sana!
 
Wanahitaji kufanya kazi ya ziada ili kurudisha fikra na imani toka kwa wananchi. Lakini sioni kama juhudi za makusudi zinfanyika kwa hilo na kwa hiyo wajiandae kisaikolojia kuwa chama dume cha UPINZANI. This time, Watapigwa tu...
 
hata ccm ikianguka nani hasa wakuiongoza hii nchi? sioni. siipendi ccm ila sioni mbadala. wate wachumia tumbo na wengine hawajitambui kabisa. wasikini Tanzania. haina mtetezi.
 
Kama ni kweli, kaaz kweli kweli... Tutasikia na kushuhudia mengi kabla ya 2015
 
Utabiri anazugia tu anajuwa kisha kufa anatafuta tu njia nzuri ya kumkabidhi nape na mizigo mingine
 
Igekuwa CCM ni timu ya mpira tungeweza kusema kwamba JK amecheza kamari kuombea CCM ifungwe na timu pinzani--kwa hivyo anaivuruga timu kwa maslahi yake. Lakini kwa kuwa ni chama cha siasa, naona kaamua kukiua chama kabisa ili akuiondoka madarakani 2015, aache upinzani unatawala--ndio maana anawataka wanaCCM kujianda kisaikolojia. Ama kweli kufa kwa CCM ni mapenzi ya Mungu!
 
Hii mada ni ya uongo, uzushi na imepotosha ukweli

Ya ukweli ni ipi sasa? Hebu tupe ya ukweli unayojua wewe...maneno yametamkwa mchana kweupe halafu wewe unapinga kwa faida ya nani?
 
Kuna wafia chama hawaelewi hata ulichokiandika na aliyoyasema Rais wao. Hawa niwakuangalia kwa makini sana maana hata baadhi ya nchi za kiafrika ambazo zimefanyamageuzi ya kiuongozi, watu kama hoa wamevuruga amani ya nchi zao. Tanzania tusiruhusu kitu kama hicho. Waendelee kuandaliwa kisaikolojia kuachia madaraka.
 
Utabiri anazugia tu anajuwa kisha kufa anatafuta tu njia nzuri ya kumkabidhi nape na mizigo mingine

Kama ni utabiri basi ulishafanywa na Marehemu Nyerere lakini wao wakaamua kuziba masikio

MWALIMU NYERERE ALIUONA MPASUKO WA CCM
Posted by Sufyan Omar in Makala za wasomaji

Dec 31, 2013
HIVI karibuni Chama Cha Mapinduzi kimefanya mabadiliko ya uongozi katika sekretarieti na kamati kuu kwa kile kilichoitwa kujivua gamba.

Tafsiri hii ya kujivua gamba ilianza kutolewa na Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akihutubia katika kilele cha sherehe za miaka 34 ya CCM mnamo Februari 5 mwaka huu.

Akieleza haja ya CCM kujivua gamba, Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho, alibainisha kuwapo kwa mchakato wa mageuzi ya ndani ya CCM ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kushindana na kushinda katika uchaguzi ujao.(Gamba wameshindwa kulivua limekwamia kiunoni... cc Chenge)

Kutemwa kwa baadhi ya viongozi wa CCM kunatokana na viongozi hao kuhusishwa na baadhi ya kashfa za ufisadi kitu ambacho kimekuwa kikichafua chama hicho kwa muda mrefu sana.(Mpaka leo hakuna aliyetemwa...Labda alimaanisha EL?)

Kashfa hizi zimekuwa zikileta mpasuko ndani ya chama na hata kama hawatakuwa makini na kuendelea kujivua magamba mpasuko utazidi kuongezeka na hatimaye si ajabu miaka ijayo tusione CCM. Kashfa ni nyingi kwa kweli,kwa mfano sijui
richmondi, Epa, Dowans
n.k. Hizi zooote zinawahusu viongozi wa CCM. (EL, RA, Mr Clean na Mkulu mwenyewe)

Mwalimu Nyerere aliyoana haya.

Hali ya ufisadi ndani ya CCM iliyosababisha kutokea kwa mabadiliko hayo ilitabiriwa na Hayati Mwalimu Julius Nyerere, alikionya CCM kutoendekeza rushwa.

Katika kitabu chake cha Nyufa chenye hotuba aliyoitoa Machi 13, 1995, Mwalimu Nyerere ametaja nyufa tano zilizoikumba nchi ambapo alisema kuwa ufa wa nne ni rushwa ndani ya CCM na serikali yake.

Mwalimu Nyerere amebainisha kuwa chanzo cha mpasuko ndani ya CCM ni kutokana na viongozi wa chama hicho kukosa maadili na hasa pale kilipoikana misingi ya Azimio la Arusha.

"Kuna miiko ndani ya Azimio la Arusha…, viongozi wetu walikutana Zanzibar wakaona Azimio la Arusha halifai, wakatutangazia na hawakuzungumzia kwamba tumekutana Zanzibar tumeona Azimio la Arusha halifai. Walikuja kimyakimya tukaona wanaanza kufanya mambo ambayo hayafanani na Azimio la Arusha. Wenye akili tukajua limekwisha hilo", anasema Mwalimu Nyerere.

Kwa mujibu wa Mwalimu Nyerere, hakuna serikali popote duniani inayoendeshwa bila miiko. Anazitaja nchi za Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na Japan na kusema kuwa zinaendeshwa kwa miiko.

"Kwa hiyo nchi zote zina miiko. Hapa sasa hatuna. Wameacha miiko ya Azimio la Arusha, hawakuweka miiko mingine, sasa ni holela tu," anasema.

Kutokana na hali hiyo, Mwalimu Nyerere anasema kuwa imefungua milango ya rushwa ambayo awali ilikuwa imebanwa. Anakumbushia enzi za TANU ambapo licha ya kuwa na miiko ya uongozi, kulikuwa na kanuni za TANU. Moja kati ya kanuni hizo ni ile iliyorithishwa CCM inayosema, "Rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala sitapokea rushwa".

"Usije ukadhani kwamba wakati wa awamu ya kwanza palikuwa hapana rushwa, ilikuwapo lakini tulikuwa wakali sana. Siku za mwanzo kabisa tulitaka watu wajue hivyo. Tukapitisha sheria kwamba mtu akila rushwa, eh kiongozi wetu anakula rushwa: anayetoa, aliyepokea … wote wanapata msukosuko," anasema Mwalimu Nyerere.

Akieleza sifa ya kiongozi anayepaswa kuiongoza Tanzania, Mwalimu Nyerere anasema kuwa kiongozi bora si yule anayechukia rushwa tu, bali pia awe na uwezo wa kuwaambia rafiki zake kwa kauli ambayo wataiheshimu na hawatarudia tena.

"Sasa Tanzania inanuka rushwa. Tunataka kiongozi atakayesema; ‘rushwa kwangu ni mwiko, mwaminifu kabisa hawezi kugusa rushwa na watoa rushwa watamjua hivyo.

"Ikulu ni mahali patakatifu, mimi sikuchaguliwa na wananchi wa Tanzania kupageuza kuwa pango la wanyang'anyi", anasema Mwalimu Nyerere.

Akizungumzia rushwa katika uchaguzi Mwalimu Nyerere anakumbushia enzi ya utawala wake ndani ya TANU na CCM akisema kuwa mali ingeweza kumkwamisha mgombea;

"Zamani katika CCM na katika TANU, tunapochagua mgombea wetu kama ana mali tunamuuliza ‘hii umeipata wapi?'. Mali ilikuwa kigezo cha kupoteza sifa ya kuwa mgombea," anasema.
(Ndio maana akamkataa EL)
Kwa misingi hiyo kujivua gamba pekee hakutushi, tunapaswa kuwa na viongozi wenye uadilifu wa kweli, wanaochukia rushwa na jamii iwaelewe hivyo.

Kimsingi rushwa ikiendekezwa italimong'onyoa taifa.
 
hata ccm ikianguka nani hasa wakuiongoza hii nchi? sioni. siipendi ccm ila sioni mbadala. wate wachumia tumbo na wengine hawajitambui kabisa. wasikini Tanzania. haina mtetezi.

Asiye jitambua wewe. Nchi inawezaje kukaa utupu (nina maana ya uogozi). Ina maana huko ktk box ambalo huwezikujitoa mwenyewe? Inaonekana upo hapa jf muda mlefu lakini haijakusaidia kubadirika kimawazo. Sorry for attacking you! hii nikwasababu wapo watanzania wengine kama wewe lakini hawafikiri mbadala wa matatizo yanayorikabili taifa.

Lakini pia ni megudua wengine ni magamba waliokata tamaa, hivyo wanachokifanya sasa ni kukatisha tamaa wengine waone hakuna tena mbadala baada ya wao kushindwa. Hii roho razima kuikemea ikiwezekana hata katika majukwaa ya siasa ( of course I will do)
 
Back
Top Bottom