Augustine Moshi
JF-Expert Member
- Apr 22, 2006
- 2,554
- 1,382
hata ccm ikianguka nani hasa wakuiongoza hii nchi? sioni. siipendi ccm ila sioni mbadala. wate wachumia tumbo na wengine hawajitambui kabisa. wasikini Tanzania. haina mtetezi.
Hii mbinu ya kusema hakuna mbadala ilishindwa Kenya na Zambia. Kenya walisema wengi KANU tu ndiyo inaweza kutawala Kenya. Kura zikapigwa, KANU ikaanguka, na nchi ikafaidika sana. Zambia hivyo hivyo: walisema wale wanaogopa mabadiliko ni UNIP tu ndiyo inaiweza Zambia. Kura zikapigwa, UNIP ikaangukia pua na Zambia ikaondoka kwenye lindi la kudidimia.
Sasa ni zamu ya CCM. Itoke tu, maana tumechoka.