JK aendelea kula Kuku as UN Representative kwenye Mgogoro wa LIbya

Chiwaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
5,726
3,762
Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete bado anaendelea kulitumikia bara la Afrika ambapo kama haufahamu, yeye pia ni Mjumbe maalum wa umoja wa Afrika katika usuluhishi wa mgogoro wa Libya.

JK ameshiriki mkutano wa kamati ya wakuu wa nchi wa umoja wa Afrika kuhusu Libya iliyokutana Brazaville, Congo chini ya uenyekiti wa Rais wa Congo Brazaville Dennis Sassou Ngueso ambapo kamati hiyo inaundwa na Marais wa Congo Brazaville, Afrika Kusini, Chad na Mauritania.

Mkutano huo uliitishwa kwa lengo la kupokea taarifa ya usuluhishi wa mgogoro huo na kuweka msimamo wa umoja wa Afrika katika utafutaji wa suluhu katika mgogoro wa Libya.-Kwa hisani ya Millardayo .com
jk1.jpeg


jk-3.jpeg
 
Mbona nikimuona kwenye picha ni tofauti nikikutana nae live??
Kwenye picha anaonekana amenawiri
 
Back
Top Bottom