Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,039
- 3,486
Wakuu,
Hili ni bandiko la ushauri kwa mam;laka husika lakini kuwekwa kwenye mjadala kuhusu jiwe kubwa la aina yake ambalo linatumika kama utambulisho wa jiji la Mwanza.
Jiwe hili liko pembezoni mwa mwa ufukwe wa ziwa Viktoria karibu na feri ya Kamanga na sambamba na barabara ya Nasser inayoelekea Ikulu ndogo huko Capri-Point.
Jiwe hili alilitumia mchezaji wa ngoma za kienyeji za kisukuma aitwaye Igulu Bugomola (Ng'wanamalundi/Mwanamalundi-thin legs and tall) ambapo alipanda juu yake baada ya kusimika vijiti vya miti kwenye mwamba na kukwea hadi juu kisha akaa na kucheza. Mpaka leo kuna masalia ya matundu ya yaliyotumika kusimika vijiti hivyo na sehemu alipokaa aliacha alama ya upande mmoja wa kalio. Igulu Bugomola alias Mwanamalundi alizaliwa huko Mwakabunga Nera wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza mwaka 1846. Huyu Mwanamalundi alitokea kuwa na uwezo wa kucheza vizuri ngoma za kisukuma kwa ufasaha mkubwa akiambatana na miujiza ya kimazingara. (Soma kitabu kilichoandikwa na Boniphas Z. Boaz kwa undani zaidi).
Wakati wakoloni walipoingia nchini Tanganyika, moja ya maeneo ambayo Mjerumani aliyatamani sana ni jiji la Mwanza ambapo mtawala aitwaye Otto Von Bismarck sanamu lake liliwekwa juu ya jiwe hilo lililoko karibu na Kamanga feri. Baada ya sanamu kuwekwa juu ya jiwe na jina likaitwa 'BISMARCK'.
Ilipotokea vita kuu ya pili ya dunia kati ya Mjerumani na Mwingereza (WWII) 1939-1945 ambapo Mjerumani alishindwa vita na Mwingereza na kwa kuwa Mwingereza alimchukia Mjerumani waliamuru sanamau la mtawala wa Kijerumani kuvunjwa na kutupwa majini kitendo ambacho kilitekelezwa haraka sana.Masalia ya sanamu hilo yapo mpaka leo hapo majini.
Napendekeza ili kulinda urithi wa kihistoria wa wenyeji jiwe hilo libadilishwe na kuitwa jina la 'Miujiza ya Mwanamalundi-The miracles of Mwanamalundi' kama utambulisha wa jiji hilo la miamba ya mawe.
Pamoja na jiwe hilo lipo jingine lenye maajabu maeneo ya Bugarika linaitwa majimoto ambalo linaukumbi wa wazi chini yake linafaa kwa utalii wa ndani na nje
Nawasilisha