Jiwe la sumu ya nyoka

Pole sana
Yanapatikana wapi hayo mawe
Kutokutangazwa sana naona sababu huku mijini nyoka ni nadra sana kukutana nao sababu hayana soko
 
Kweli a long time ago ili jiwe Mzee wangu alilinunua sijui wapi mara nyingi ilipotokea mtu kugongwa na jamii ya viumbe weyenye sumu aliwekewa jiwe hilo leusi, ajabu lilikuwa linachukuliwa na hata majirani,hata watu wa ng"ambo nyingine.

Ni jiwe lisilokwisha,kweli utaalam huo wa jiwe la nyoka sijui limetoka wapi,kusema wamasai sijui,km kuna ukweli wowote kwani kule kanda ya ziwa yalikuwa yakiuzwa kwa wingi tu,wakt ule hata hawa wamaasai hawakuwa wakisafiri kila kona km leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu utalijua kwa kuliweka/kuligusa kwa ncha ya ulimi wako kwa mbele. Kama ni lenyewe litang'ang'ania halibanduki kirahisi na utahisi kufyonzwa ktk ulimi wako na kulibandua hapo utatumia nguvu. Lina rangi nyeusi kama mkaa na ni rough kidogo. Kama haling'ang'anii unapolilamba kwa ncha ya ulimi wako achana nalo. Ni Fake. Unaweza kuyapata mawe hayo siku za minada/magulio au kwa watembezaji stendi ya Mabasi pale Msamvu Morogoro na wanalihifadhi katika nylon ili lisipate unyevunyevu kwani litafyonza na kupoteza ubora wake.
 
Usiliamini 100% hilo jiwe kama tiba ya sumu ya nyoka,hasa wenye sumu kali kama vile Cobra au Blackmamba...jiwe hili husaidia sana kwa nyoka wasio na sumu kali pamoja na wadudu jamii ya nge,buibui na tandu..Kwa wale wakazi na watakao bahatika kufika Wilaya ya Kilosa hasa maeneo Kilosa mjini mtafute mtaalam mmoja anajulikana kwa jina la Dk.Madinga..Huyu jamaa huuza haya mawe kwa bei rahisi kabisa pamoja na dawa za kunywa pale utakapopata shambulio la nyoka wenye sumu kali,dawa zake ni msaada mkubwa kwa watu wengi sana hasa wale wanaojishughulisha na kilimo cha mpunga na mahindi ambako kesi za nyoka....Kuongeza tu huyu Dk.Madinga hutumiwa pia na hosp.ya wilaya kutoa huduma kwa wagonjwa wa kesi za nyoka,si unajua dawa za nyoka Hosp za serikali ni haba sana na mda mwingine hazipatikani kabisa..
 

Mkuu Mshana jr wagunduzi wa jiwe hilo ni wazee wa kisukuma wala si wamasai. Hata mimi najua kulitengeneza nilifundishwa na babu yangu. Huwa linanyonya sumu tu kutoka kwenye damu wala halinyonyi damu kama ulivyosema hapo juu ila siku hizi kunamatapeli yanauza mawe feki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…