Sumu ya nyoka ni dawa mujaarabu kwa wenye matatizo ya heart attack ,.Tusiwaue nyoka hovyo

undefine

JF-Expert Member
Nov 17, 2016
439
1,000
Je kuna ulazima wa kuwaua nyoka wote kama baadhi ya watu wenye mitizamo ya kwamba nyoka kila akionekana ni kupigwa mpaka afe ?

1.kwanza itakuwa sio fair kwenye eco system kuna baadhi ya wanyama kama nyegere ,nguchiro hutegemea nyoka kama chakula Chao pendwa na pia kuna ndege kama eagle chakula chao ni nyoka,pia nyoka chakula chao ni panya na chura ambao wadudu hawa ni waharibifu na hawapendwi na watu .kuwaangamiza nyoka na kutaka wasiwepo ni kuharibu food chain.

2.imegundulika hivi karibuni ya kwamba kuna protein nyingi kwenye sumu ya nyoka ambayo huitwa trowaglerix,watafiti wanasema protein hiyo inakaa kwenye seli ya damu ya platelet ambayo husaidia damu ipite vizuri kwenye mishipa ya moyo na hivyo kumsaidia mgonjwa aliepata heart attack apone .

Heart attack hutokea pale damu inapozuiliwa kupita kwenye mishipa "arteries.damu huzuiliwa kupita kwenye mishipa ya moyo sababu ya clots iliyotengenezwa na seli ya platelet ambayo huzuia flow ya damu kupitisha oxygen kwenye moyo.,mfano mtu anapojikata au amepata jeraha lililomsababishia damu itoke kuna mahala itafika patatengenezeka clots muunganiko wa damu ambayo hufanya damu isiendelee kutoka sasa hizi clots zikitengenezeka kwenye mishipa ya moyo ambayo itasababisha damu izuiliwe kupeleka oxygen kwenye moyo na hivyo kumpelekea mtu kupata mshituko wa moyo na huenda kufa.

Sasa traowaglerix Inapoungana na damu ,compound mpya huzuia seli za damu ya platelet kutengeneza clots na hivyo damu itakuwa inapita vizuri kwenye mishipa na kupeleka oxygen kwenye moyo.


Dr Kevin marzo mkuu wa kitengo cha cardiology NY

"dawa nyingi zinazotumika kutibia wagonjwa wenye mshituko wa moyo huhusisha seli ya platelets .

" uendelezo wa tafiti hii mpya ya sumu ya nyoka ambayo itaweza kuzuia blood clot ni ugunduzi unaofurahisha-Dr Kevin


NB:Snake venom inafaida kwa wagonjwa wa mshituko wa moyo ,watu wengi hufariki sababu ya mshituko wa moyo sasa tiba ya uhakika imepatikana sumu ya nyoka husaidia kutengeneza dawa ambayo husaidia damu isiweze kuganda kwenye mishipa na hivyo kuzuia damu kupita na kusababisha heart attack ,protein inayopatikana kwenye sumu ya nyoka ni dawa mujaarabu

Tusiwaue nyoka kikatili kila tuwaonapo ,nyoka amepewa sumu na Mungu ili aitumie kwenye kuwinda kitoweo chake kama panya ,na hiyo sumu ina msaada mkubwa kwenye kutengeneza dawa kwa wanaadamu,pindi tuwaonapo nyoka wenye sumu tuwaite mamlaka husika waje kuwatoa ili kuepusha madhara kwako wewe na kwa nyoka kujaribu kumuua utamlazimisha awe aggressive wakati ni mpole na pia kuwaua utaharibu food chain.


Tajirika na Kilimo cha Nyoka: Tuwapende na kuwatumia Nyoka badala ya kuwaua
 

Humble African

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
4,773
2,000
Mbona sumu ya nyuki yaani "bee venom" inaweza kutibu ukimwi lakini kila siku waswahili tumeng'ang'ania kula asali tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom