meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,464
- 4,828
- Thread starter
- #21
una covermatibabu ya meningitis?
CHF ni moja ya social health insurence zinazoweza wakomboa wananchi kupitia risk pooling. Yaani wazima kuwachangia wagonjwa. Tatizo kubwa lililopo kwa sasa kwenye mfuko huu ni utaratibu mbaya wa matumizi ya fedha hizi. Zinalipiwa per diem badala ya kununulia dawa, maeneo mengi hazitumiki kabisa kutokana na ukiritimba wa sheria zake/za manunuzi. Watu walichanga na baadae kuona mfuko huu hauwasaidii kitu kwa kuwa fedha yake haiwarudii walengwa. Nyingi hubaki kama bakaa kwenye accounts za halmashauri.
Ili kuboresha mfuko huu, ni lazima halmashauri zitunge sheria na taratibu za mfuko huu zitakazosimamia ukusanyaji wake na matumizi yake. Vinginevyo hakuna mwananchi atakae changa na asione fedha yake imefanya nini.
Ina cover matibabu ya meningitis?
Unaweza ukadhani ni swali la utani !
Meningitis ni ugonjwa unaotibiwa kwa mgonjwa kulazwa,kufanyiwa vipimo ikiwa ni pamoja CSF analysis,kupewa dawa na matibabu saidizi!Kimuongozo CHF hatakiwi kuhudumia wagonjwa waliolazwa la uzoefu nilioupata kutoka kwa wilaya zilizofanikiwa katika CHF kwa sasa zinahudumia wagonjwa waliolazwa na hawajapata hasara au kushindwa kuwahudumia.
Mkuu nahisi bado unaongelea experiance ya miaka ya nyuma ambapo mapato ya mfuko huu yalitumika vibaya.
Matumizi ya mfuko huu yameelekezwa vizuri tu yaani asilimia 60+ inatakiwa kununua dawa na vifaa tiba,asilimia zilizobaki ni kwa ajili ya motisha(extra duty allowance),ukarabati mdogo na ajira.
Tatizo lililolalamikiwa sana ni kuhusu matumizi ya fedha inayoitwa tele kwa tele,hii ni fedha inayotolewa kwa halmashauri husika baada ya kuenroll wateja wa CHF yaani kama halmashauri imepata wanachama 100 *5000 =500000 basi central gov/NHIf itawaongezea 500000 nyingine(hii ndio ilikuwa inaliwa badala ya kupelekwa kwenye kituo)
kumbuka kila kituo kinatakiwa kuwa na account ya CHF na signatories ni mkuu wa kituo husika na mwenyekiti wa kamati ya kituo.
Usidharau nguvu ya uwepo wa fedha hizi,kwani kwa sasa ndizo zinazofanya huduma ziendelee katika vituo vyetu pamoja na kutokuwepo au kucheleweshwa kwa fedha za wahisani.
Nasisitiza kuwa CHF inaweza kuwa mbadala wa fedha za wahisani.