Wasalaamu wana JF!
Baada ya kutafakari sana nimeona nije na mada hii hapa jamvini ili tujisaidie wenyewe kama watanzania na wanajamii,namaanisha tusisubiri serikali,wanasiasa au wahisani watusaidie!
UTANGULIZI
Nadhani tumesikia mara kwa mara kuhusu vilio vya wananchi kuhusu utoaji wa huduma katika vituo vya afya hususani vile vya serikali.Tumesikia kuhusu uhaba wa dawa na vifaa muhimu vya tiba bila ya kupata suluhisho la kudumu.
Pia tumesikia juu ya ukosefu wa fedha unaopelekea kukosekana kwa dawa na vifaa tiba.Ukosefu huu umeelezwa na kuhusishwa na bajeti ndogo inayotengwa katika wizara ya afya mfano mzuri ni mwaka huu tumejionea bajeti ya wizara hii ikishuka kwa takribani 1/4 kulinganisha na mwaka jana kinyume kabisa na makubaliano ya Abuja ambayo yanapendekeza karibu asilimia 15 ya bajeti ya nchi ilenge afya.
Pia tumesikia kuhusu ucheleweshaji au usitishwaji wa bajeti za wahisani katika sekta hii.
Vile vile ni mara chache kusikia halmashauri imetenga au kutoa pesa zitokanazo na makusanyo ya ndani kwa ajili ya idara ya afya.
Serikali both local na central zinaamini fedha kutoka kwa wahisani zinatosha kuhudumia sekta ya afya!
KUHUSU UCHANGIAJI WA WANANCHI KATIKA HUDUMA ZA AFYA
Kuna mfumo uliowekwa kwa wananchi kuchangia huduma za afya;
1.Uchangiaji wa fedha wakati wa kupata huduma yaani papo kwa papo.hapa ni kama vile unavyohudhuria hospitali na kutakiwa kulipa fedha kwa ajili ya faili,vipimo au kulazwa wadini.
Mfumo huu ni mzuri lakini una changamoto nyingi hasa hasa rushwa.
2.Mfumo wa pili ni ule wa kutimia bima za afya,hapa naongelea wale waajiriwa.
NHIF yaweza kuwa ndio bima ya afya iliyofanikiwa au kutimiwa kwa wingi hapa nchini.
3.Mfumo wa tatu na muhimu kwa mada hii ni ule wa mfuko wa afa ya jamii (CHF aka community health fund).
Nitelezea zaidi kuhusu CHF hapo chini.
Kwa ufupi mfumo hii mitatu ndiyo mifumo muhimu ya jinsi gani mwananchi anaweza kuchangia huduma za afya nchini.Yawezekana kuna mingine lakini kwa ufupi na umuhimu hiyo hapo juu ndio mifumo ya kuchangia huduma za afya nchni.
KUHUSU CHF
Kama nilivyosema hapo juu huu ni mfuko wa uchangiaji huduma za afya kwa ngazi ya jamii.
Kila kaya hutakiwa kuchangia kiasi flani cha fedha kwa mwaka mara nyingi ni 5000 au 10000 kwa mwaka na hivyo mwanakaya atakapoumwa atatakiwa kutibiwa matibabu ya kawaida kwa mwaka mzima bila kutoa chochote katika kituo chake cha karibu.Tukumbuke kuwa wastani wa kaya nchini ni 4-6 hivyo mfuko utawajibika kwa watu wanne mpaka sita kwa kutegemea ukubwa wa kaya katika maeneo mbalimbali.
Mfuko huu ni mzuri kwa familia masikini zisizo na ajira rasmi.kuna maeneo kama singida wanasema 'kuku mmoja tiba mwaka mzima'
pia halmashauri yaweza kupewa fedha kulingana na idadi ya kaya zilizojiunga kwa mfano zimejiunga kaya 100 na kulipa shilingi 10000*100 ambayo ni shilingi 1000000 basi halmashauri itapewa nyongeza ya sh. 1000000.
Matumizi ya fedha zinazotokana na mfuko huu ni manunuzi ya dawa na vifaa tiba,posho na ukarabati katika kituo kilichoandikisha wanachama.
Kwa ufupi tu haya ndio yanayohusu mfuko huu wa afya ya jamii.
MAONI YANGU
Kwa kuwa jamii kubwa ya watanzania ni masikini lakini sio masikini wa kukosa 5000 au 10000 kwa mwaka ni vyema tukahamasishana kujiunga na mfuko huu.
Tatizo la dawa na vifaa tiba linaweza kumalizwa kwa kuwezesha kila kaya kuwa insured na mfuko huu.
Tujenge utamaduni wa kuchangia huduma za afya na tuondokane na kasumba ya kutegemea hisani za watu wa marekani!
Nipo tayari kwa ufafanuzi zaidi...!
Kumbuka:Sijatokea NHIF/MOHSW bali ni mdau katika sekta ya afya nimejitolea kuhamasisha kwa manufaa ya jamii yetu masikini.
KARIBUNI KWA MJADALA
Nyongeza ya mdau
IronLady