Jirani yetu limbukeni anatuboa

hii makitu imekuwa tabu sana. yani kila kona ni tabu tupu. pale kwangu dah ni noma aisee..nimewambia lakini baada ya muda mfupi wanarudi hewani tena. huwa nafurahi sana umeme ukikatika napata muda wa kulala, sasa hapo JOTO kali hunisibu tena tabu nyingine hiyo.. mjini hapa kaz kwelikweli.
 
:A S angry::A S angry::A S angry: kwa kweli inatia hasira sana, Mimi jirani yangu pia alikuwa nafanya hivyo , nilimfuata nikamweleza, hakunijibu kitu ila aliendelea kufungulia kwa sauti kiasi kwamba hatuwezi hata kutizama TV maana hatusikii, nikaenda kwa mjumbe akaja akamweleza, akaacha kwa muda wa wiki akaanza tena, tena hapo ndipo alipoanza kuweka nyimbo za taarabu, basi nikaenda serikali za mtaa, nikawaambia wakaja wakamchukulia hatua, walimtoza faini ya sh 50,000/- pale pale na akaambiwa akiendelea atafungwa. Tangu siku ile mpk leo hii kakoma hafungulii tena mziki kwa sauti. KUISHI USWAHILINI NI NOMA!!!
 
Ningekuwa mimi dawa yao ni kuwa na mziki mkubwa zaidi yao,natafuta siku akiwa anaumwa nami nafungulia muziki kwa sauti ya juu,atajirekebisha tu.

Ha haa haa! Yaani kuna wakati natamani niwashe mziki mkubwa na kuziheuza spika kuelekea kwake, lkn naona tusije kuwa wote wajinga. Sijui watoto wake kama wanalala vizuri.
 

Ha haa haa, hiyo tamu mkuu. Usiku huu, jamaa tayari kaanza, yaani yeye hana cha taarifa ya habari wala nini, yaani kama dala dala. Taabu kweli hii.
 
Hilo tatizo hata mimi linanisibu, nasubiria ushauri pia, manake mtu mzima kumfundisha kazi kweli kweli

Na wewe mwaga ugali akimwaga mboga!
Niliwahi kuishi Mwananyamala kisiwani mwaka 2006 jirani mmoja alikuwa na tabia hiyo. Nilichofanya baada ya kugundua kuwa radio yake ni ndogo kuliko yangu niliamua kumuonesha kazi. Niliweka spika usawa wa dirisha lake nikaweka plate zote cd nikafungulia sauti ya mwisho na kuweka repeat! Niliondoka kama masaa saba. Niliporudi nikazima na kusema wanafikiri wao tu ndo wanaradio, hadi nahama miezi sita baadaye sikuisikia tena radio yake!
 
Mimi pia hili tatizo jirani yangu ni mzaramo yaani tabu tupu toka anunue kamchina kake basi ni taabu kuna mida huwa natamani nikamtie vitasa,yaan hajui cha mchana wala usiku.kero
 
Jaribu kumwambia, huenda hajui sehem ya kupunguzia saut na anaona aibu kuuliza..!!
 
Hahahahahahahaha

 
Nunua na ww music system yenye akili. Fungulia mpaka mwisho na hutaisikia radio mkuluma yake.
Mwisho ataona aibu na kuizima radio yke inayokoroma kuipusha nyumba yake kupata nyufa.
 

Mkuu Tanzania Mpya, laiti kama mngekuwa mmepanga kwenye nyumba moja na hiyo nyumbe isiwe na dari, Ungenunua kilo 2 za nyama unaziweka kwako bila kupika unafunga na kusafiri kwa wiki 2 unamwacha na yeye acheze na harufu ya uozoo kwa kipindi chote ukiwa likizo!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Tafuta fundi pikipiki aje hapo karibu na dirisha lake ,kila dakika unalipiga resi mwenyewe atakimbia na kuzima kiredio
 

Impections should be allopwed to cancel themselves
 


Unaonekana hauna self-confidence; Nenda kaishi Ulaya kwa wazungu wenzio
 
Dawa ni moja tu nunua yale maredio yenye maspika makubwa mawili marefuuuuu urefu unaolingana na mtoto wa darasa la tano na fungua mwenyewe atazima kimziki chake.
Pole sana tena ukizingatia kuwa siku hizi mambo ya startimes yanahusika basi kutwa kusikiliza taarab wakina gea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…