Jirani yangu simwelewi

Jirani yangu simwelewi

ninavyoona tatizo lipo kwako. hauna mazoea na watu.. huyo ni jiran ako.. so inabd umzoee maan nilivyoelewa yy anajitahd kwa hali na mali kukuzoea. anyways mwekee boundaries kwa kumwelezea anavozengua. tumeumbwa na kukulia katika mazingira tofauti so usishangae yy kuwa hivo. hajui kama anakukera.
MI nipo km mleta uzi stak mazoea ya kimaandaz
 
huyo ni mswahili tu mwenye tamaa na mmbea. Nimeshakutana nao. Nilipomaliza chuo nilikaa nyumba ya peke yangu uswahilini kidogo nikawa naishi kivyangu vyangu sina habari na mtu zaidi ya salamu, ila baadae nikasema nisijitenge sana niwaungishe hata kusuka tu. loh! nilijuta. Mpaka umalize kusukwa ushahadithiwa stori ya kila mwanamke hapo mtaani na wala huwajui unaishia tu enhe..inhi..mmh. Ameshakwambia siri zake zote (we ndo unaona ni siri). Halafu wanawake wa kiswahili karibia wote wanajua wenzao vitu tunanunuliwa na wanaume, kwa hiyo akikuona na kitu kizuri anajua una "bonge la bwana"! Wale watu wanaishi maisha ya raha sana, hawana stress. Ambition kubwa ni kumiliki dera kama la flani, acheze upatu anunue "desin tebo" kama ya fulani .. baas.
Yeah kweli kabisa, hata mi nawaonaga hivyo. Tena sometimes nahisiga wanaenjoy life kuliko sisi, nadhani tunajipa stress sana kwa hizi ambition zetu za ku-aim high kila kitu. Imaginary life tunayo-wish nahisi inatutesa sana bila kujijuwa
 
nafikiri hapo unaweza mweleza ukweli ili usibaki na dukuduku na kubaki free soul
 
Ukipata rafiki wa aina hiyo unapaswa umshike sana Mungu kwani wengi wao sio wazuri.

Ni vyema pia kuhama nyumba hiyo kama uwezekano upo.
 
Watu wa aina hii wapo sana. Wazoee tu. Ukute hakuna zaidi ya admiring tu.

Kuna kina dada flani hivi tunafanya kazi eneo moja. Kila mara wananiuliza nani ananisafishia viatu, nanunua wapi nguo, yadda yadda yadda. Mwingine aliomba shati nililovaa nikajua utani, bwana we.... niliishia kumpa tu.

Usikubali kuwapa nguo uliyovaa. Wanawake wengine hawana nia nzuri na huendekeza ushirikina. Mbaki ni hapi hiyo ilikuwa ni gia ya kukuingia na labda hukuelewa somo.
 
Nashindwa kumuelewa jirani yangu na ananifanya nisiwe comfortable.... Nyumba ninayoishi tupo watano kila mtu na kwake anaijtegemea wote ni vijana na hakuna mwenye familia. Tupo wadada wawili tu. Huyu dada jirani yangu alinikuta wakati akihamia hapo na mwanzoni alipata matatizo nikamsaidia kama kama ambavyo ningemsaidia binadamu yoyote. Aliumwa na hakuwa na ndugu karibu (kwao Shinyanga) hivyo nilimhudumia kwa ukarimu wote nilimpikia, na kumsaidia kufanya usafi hadi alipopata nafuu.

Baada ya kupona maisha yaliendelea japo hatukua na ukaribu zaidi ya salamu na mambo basic kama kushare bills. Kumbuka sisi ni vijana na pretty much ndio tumeanza kujitegema so hatujajiestablish kihiivyo...ila nimegundua huyu jirani yangu ni kama anawivu ama sijui ni kitu gani. Alipokuja kwangu kila alichokiona alitaka kujua ni menunua bei gani na vingine alidiriki kuniuliza umenunuliwa na mpenzi wako? Sikumbuki nilipotezeaje coz sionagi kama ni sawa ku disclose mambo yangu binafsi kwa mtu ambae sio wa karibu.

Ila naona ni kama tabia kila tukionana akiona nimebadilisha style atauliza umesuka bei gani, juzi kaniona na simu kaniuliza mbona hujanionyesha kitu kipya. yani hata nikinunua maybe kiblouse kipya lazima atauliza. Kinachonimaliza ni kwamba hata kama niko ndani napika ataongea from her room eeeeh jirani leo unapika samaki au leo unapika kitu flani? Hua namjibu kwa maneno machache tu.

Bottom line ni kwamba she makes me uncomfortable!!!!!!! Yani very uncomfortable!!!!! Akiona mpenzi wangu wangu yupo ndani atakuja kunigongea either aombe kitunguu au kibiriti.

Nisaidieni jirani wa hivi naishije nae?????
Huyo demu mshamba. Kwa maneno mengine ushamba unamsumbua.
 
WEKA PICHA MKUU
TULITATUE SASA HIVI HILI TATIZO.
 
Hiv si umwambie mm sipend kuulizwa ulizwa y unamkawiza. Au muulize unataka kununua? Akisema ndio mwambie tafuta naul nikupeleke nilipo nunua au nilipo suka. Yan hiyo ni tabia yake jibu short ans asipate la kuuliza
 
Acha majungu mtoa mada,mbaya wako yuko huko ulikopanga yakupasa umwambie ili uwe huru(hit the nail on its head)
 
Mwambie tu ukwel that you don't like the habit just in good terms as grown up...km anajielewa atajua nn cha kufanya...kukaa kimya kutakuumiza na kukufanya more uncomfortable n unsecured.huo n mtazamo wangu tu
 
Back
Top Bottom