Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,350
Jirani yangu Engineer Peter alitafutiwa mchumba na wazazi kutoka kijijini kwao. Mchumba ni mtoto wa mkatekista Thomas, mama Peter alimpenda Immaculate mtoto wa mkatekista kwakuwa alimudu kuongoza sala baada ya misa asubuhi kanisani. Mama alimuona huyu atamfaa Peter kwakuwa ni mvivu wa kusali.
Kwa kweli Engineer Peter hakumpenda kabisa Immaculate ambae alijifunza kushona baada ya kumaliza darasa la kidato cha nne.
Harusi ilikuwa ya kuhadithiwa kijijini kwani kila aliyehudhuria alipata sahani ya pilau ng’ombe na pilau kuku kwa wasiokula ng’ombe pamoja na chupa ya soda. Baada ya harusi walirudi mjini na Engineer Peter alishangaza wengi kazini kwani hakwenda hata week ya fungate.
Immaculate na Peter walibahatika kupata watoto wa tatu. Peter amepata mchepuko hasikii haambiwi. Huyu dada ni mhasibu ofisini kwa kina Peter ambae amefiwa na mume na ameachwa na watoto wawili.
Peter amekuwa ndiyo Baba wa nyumba. Mhasibu Clara alishajua Engineer Peter ni genius na amemuomba awe anawapa wanawe tuition ya physics na maths kwa ujira wa papuchi.
Majibu ya form four yametoka, watoto wa Clara wametoka na division one ya point saba. Mtoto wa Peter amepata division three, uwezo anao lakini hakupata support ya kutosha wakati anajiandaa na mitihani.
Huyu ndiyo genius Engineer Peter.