Jirani yangu akinifanyia hili kisheria nifanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jirani yangu akinifanyia hili kisheria nifanyaje?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by ndyoko, Nov 14, 2011.

 1. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Waheshimiwa mimi ninaishi na majirani wawili tunaopakana mpaka wa viwanja vyetu. Na wote tunatumia njia moja kufika majumbani kwetu na njia hiyo inaishia kwenye kiwanja changu. Majirani zangu hao wawili kwa muda majirani zangu hawa wametoboa upenyo ktk 'fence' za nyumba zao na wameelekeza maji machafu kwenye nyumba yangu.

  Hii inasababisha maji machafu kutoka nyumba zao yote kutuama kwenye kiwanja changu. Lakini pia mwingine amepanda maua kwenye njia inayoingia kwangu hali inayopelekea mimi kuingia kwa shida nyumbani kwangu hasa ninapoingia na gari.

  Je ktk mazingira kama haya, ni hatua gani nnazoweza kuzichukua kisheria ili waweze kufunga matundu ya maji machafu wanayoyatiririsha kwenye kiwanja changu? Nisaidieni waheshimiwa.
   
 2. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Hebu tuwasikie wataalamu hata mimi nina tatizo kama lako ndugu
   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Kwenye hili jukwaa kuna wakati inabidi usubiri feedback hata miezi, sijui kesi nyingi mahakamani?
   
 4. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mpm mr rocky
   
 5. J

  Jamuhuri Huru Member

  #5
  Nov 15, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani waungwana mimi naona hili tatizo ni common maeneo mengi sana hasa kule tunakoishi wenzangu na mimi, alimaarufu kama Uswahilini. Ukifika sehemu kama Buguruni, Manzese, Vingunguti, Ilala Mchikichini, Maeneo furani kule Temeke nk hili hatalikuta wazi wazi. In short suruhu ya hili ni kuonana na wale tunaowaita Bibi au Bwana Afya, hao watumishi wa Serikali wanawajibu wakuwafungulia mashakata watu wanatillilisha maji ovyo mitaani, na wewe unakua kama shaidi wao katika hiyo kesi. Ukishindwa kuwapata basi wasiliana na serikali ya kijiji/mtaa wanawafahamu na watawapa taarifa kisha watafwatilia.
  Mimi nilishawahi kushuhudia kesi ya aina hiyo mtu alipigwa faini live na kama angeshindwa alikua apelekwe Keko, yeye alikua anafuga kitimoto a.k.a nguruwe kwenye makazi halafu anatililisha maji ovyo na siunajua mfugo huo unavyonuka.
  So nawashauri watafuteni Bibi au Bwana Afya wa kata zenu hilo ni kati ya majukumu yao.
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180

  Nashukuru sana ndugu kwa ushauri wako mzuri. Talifanyia kazi hilo haraka
   
 7. L

  Leornado JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ongea na majirani zako kwanza, ikishindikana nenda kwa katibu kata wako yaeye ataamua ninikifanyike. Ikishindakana watihise unaena ngazi za juu. Hapo wataogopa manake fine yake ni kubwa mno ikiwemo kwenda jela.
   
 8. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Thanx mkuu, nilishaongea nao kwani hata walitaka kuongea! Ntachukua ushauri wako na kuufanyia kazi immediately
   
 9. Dunda kwetu

  Dunda kwetu JF-Expert Member

  #9
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 265
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Iko hiivi.waite au nenda kaongee nao irani zako,ukikosa muafaka waambie utakwenda ngazi za juu hilo walifahamu.utakuwa umetimiza wajibu wako wa kibinadamu kama binadamu.Hatua ya pili kamwambie mumbe wenu wa nyumba kumi na umuonyeshe hali halisi yeye ndie atakae kuwa shahidi No mbili ikiwa kama hajalitatua tatizo.Hatua ya tatu kawaone watu bwana au bibi afya kama walivyosema wadau
   
 10. Caren

  Caren JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Kuna sheria inaitwa Tort Law au sheria ya madhara. Hii ndiyo huwa inagovern masuala yako. Una haki ya kulalalamika on the principles of Ryland Versus Fletcher. Naomba nishee na wewe one a paragraph in one of the judgements ili uweze kujua to what extent sheria hii inaangalia:- This reasoning, which is echoed in some academic writing and the Canadian case of Motherwell v Motherwell (1976) 73 D.L.R. (3rd) 62 which the Court of Appeal followed, is based upon a fundamental mistake about the remedy which the tort of nuisance provides. It arises, I think, out of a misapplication of an important distinction drawn by Lord Westbury L.C. in St. Helen's Smelting Co v Tipping 11 H.L.C. 642, 650. In that case, the plaintiff bought a 1300 acre estate in Lancashire. He complained that his hedges, trees and shrubs were being damaged by pollution from the defendants' copper smelting works a mile and a half away. The defendants said that the area was full of factories and chemical works and that if the plaintiff was entitled to complain, industry would be brought to a halt. Lord Westbury said: My Lords, in matters of this description it appears to me that it is a very desirable thing to mark the difference between an action brought for a nuisance upon the ground that the alleged nuisance produces material injury to the property, and an action brought for a nuisance on the ground that the thing alleged to be a nuisance is productive of sensible personal discomfort. With regard to the latter, namely the personal inconvenience and interference with one's enjoyment, one's quiet, one's personal freedom, anything that discomposes or injuriously affects the senses or the nerves, whether that may or may not be denominated a nuisance, must undoubtedly depend greatly on the circumstances of the place where the thing complained of actually occurs. If a man lives in a town, it is necessary that he should subject himself to the consequences of those operations of trade which may be carried on in his immediate locality, which are actually necessary for trade and commerce, and also for the enjoyment of property, and for the benefit of the inhabitants of the town and of the public at large. If a man lives in a street where there are numerous shops, and a shop is opened next door to him, which is carried on in a fair and reasonable way, he has no ground for complaint, because to himself individually there may arise much discomfort from the trade carried on in that shop. But when an occupation is carried on by one person in the neighbourhood of another, and the result of that trade, or occupation, or business, is a material injury to property, then there unquestionably arises a very different consideration. I think, my Lords, that in a case of that description, the submission which is required from persons living in society to that amount of discomfort which may be necessary for the legitimate and free exercise of the trade of their neighbours, would not apply in circumstances the immediate result of which is sensible injury to the value of the property.
   
 11. c

  chegreyson JF-Expert Member

  #11
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 735
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 60
  Kwani haujakaa na jirani zako ili kupata ufumbuzi wa tatizo lenu?
   
 12. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Jenga fence ya tofali halafu uone hayo maji watayaelekeza wapi!!
   
 13. M-pesa

  M-pesa JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2011
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ingia gharama kwa ku divert njia ya maji kuyarudisha yanakotoka then usikilizia itakuwaje.
   
 14. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #14
  Nov 25, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mimi kama mtaalamu wa sheria za mkononi, kwanza nitang'oa hayo maua waliyootesha barabarani...au nitayakanyagia mbali.
  Pili, naweka ukuta hayo maji waliyoelekeza kwangu yabaki kwao. Halafu siku mojamoja nafyatua risasi mbili tatu hewani nikiwa kwangu....yani na-test silaha yangu.
   
 15. t

  tryphone Member

  #15
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama mchangiaji mmoja livyosema hapo juu,ipo sheria ya madhara ambayo inaweza kukusaidia kutatua tatizo lako ikiwa ni pamoja na compasation ya damages ulizopata kutokana na uchafu huo pamoja na kufungiwa njia.....unachotakiwa ni kufika kwa mwanasheria na kumweleza ambaye atakupa ushauri wa kisheria
   
 16. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Thanx alot!
   
 17. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #17
  Nov 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,060
  Likes Received: 6,507
  Trophy Points: 280
  pole mwaya
  uswazi kwetu hayo ndo maisha ya kawaida sana.
   
 18. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #18
  Nov 30, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,642
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Mkuu mimi nina rafiki yangu wa karibu sana pia ni mhanga wa tatizo kama hili. tena kwake jirani mmoja ameweka bomba la maji mpakani na fence hivyo maji machafu yanaelekea kwake. mwingine anamwaga uchafu wa aina yeyote hata akichinja kuku anamwaga kabisa huo uchafu kwenye fence hivyo maji machafu yanaelekea upande wake, mwingine anafuga bata ambao wanachomoka kwake wanajiachia wapendavyo kwa jirani yangu. dah jamaa anasema ni kero tupu hajui afanyeje. wataalam wa sheria watatoa muongozo

   
 19. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #19
  Nov 30, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Pole sana ndugu yangu, mimi nilikumbwa na huo mkasa kwanguwalipitisha mambomba ya maji (mradi wa kichina) ndani ya kiwanja changu bila kuniambia mwingine akatobowa karo la maji taka akaweka bomba lake nilicho fanya niliwapa taarifa kuwa ninangoa bomba zao, pia walipanda michongoma ndani ya kiwanja changu kuashiria mipaka na mweingine akajenga ndani ya kiwanja changu tukavutana nikaona wananipotezea muda nilichokifanya nikafyeka ile michongoma nikajenga ukuta na yule aliejenga baraza la sebuleni kwenye kiwanja changu nikavunja na kuweka ukuta hadi juu sikumwachia hata nafasi ya kupita mbwa na mabomba walipitishia kwangu nikangoa yote na yule alie weka la majitaka nalo nikatoa nikaziba sasa hivi wameshika adabu kila mtu alieingia ktk kiwanja changu amebomoa upande wake ili aweze kupita, taarifa nilishapeleka hadi baraza la ardhi nikapata baraka zote. Now tunaishi kwa adabu zote.

  Najua mtajiuuliza wakati wanapitisha mabomba na kujenga nilikuwa wapi, niliijenga hiyo nyumba nikabakiza finnishing kipindi na kusanya za kumalizia nilikaa kwa muda mrefu takribani 8 yrs ndio nikaanza tena ujenzi ndipo yalinikuta hayo
   
Loading...