X!!. JIRANI TAM TAMUU
28
Endelea...
"Shomy: seif sikubali nina ujauzito wako....
Nyumba nzima ilishituka kwani kila mmoja alijua shomy ni mke wa juma,
Sheikh alisimama,
"Seif kwaheri siwezi kufungishisha hii ndoa mpaka utakapojipanga,
Sheikh na watu wake waliondoka nikabaki na msala wa shomy,
"Seif: unasemaje shomy?.
"Nina mimba yako,
Kichwa kiligonga mala mia zaidi nikajiuliza kwanini shomy aonge mbele ya watu?. Tena mmewe akiwepo,
Juma aligeuka akaangaliana mkewe kisha akamuuliza,
"Shomy una mimba ya seif? "Ndio,
"Kwa hiyo ulinisaliti mke wangu?.
"Nisamehe mme wangu,
Niliingilia kati,
"Juma wewe ndie uliyeanza kutoka na mke wangu kabla mimi sijatoka na mkeo kwa hiyo umsamehe mkeo,,
"Seif nakubali ila juwa kuwa mimi sijadhini na mkeo ila wewe umefanya mapenzi na mke wangu roho inaniuma sana,
"Nitaamini vp hujatembea naye?.
Mke wangu aliingia kati,
"Mme sikuwahi kuzini nje ya ndoa yangu wala sikuwahi kuzini kabla ya ya ndoa yangu nazani unajua uliniowa nikiwa na bikira yangu,,
"Mke wangu nini kilikukumba wewe mpaka ukawa karibu na juma?.
"Mme wangu nisamehe sema ukweli nilijuwa kuwa kwa kuwa sikuwa chaguo lako basi utakuja niacha kwa sababu niliona unaanza kubadilika mala kunifokea mala kukata kula chakula changu hiyo hali ndio iliyonifanya nitafte faraja nje ila nimegundua wewe ni mwanaume bora kwangu kwa kuwa nimeelewa mimi ndie niliye kosea na pia juma nilikuwa nafahamiana naye toka zamani na aliwahi kunichumbia kwa kipindi cha nyuma kwa hiyo nilijikuta nataka kurudisha mapenzi kwake ila nimeliona kosa langu nililiofanya kwako nisamehe seif naomba unisamehe mpenzi wangu,,
Nilikaa kimya nikamsikiliza mke wangu maneno yake niliona yana ukweli mtupu ila sikuweza kukubali mbele ya watu ili nisijeonekana mimi ni mkosaji,
"Nimekuelewa ila sitaki kulazimisha akiri yangu kukupenda,,
"Shomy: seif unaniweka upande gani mimi?
Swali la shomy lilinichanganya sana nikashindwa nionge nini?.