Ulongupanjala
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 7,673
- 12,301
Habari za leo?
Kuna jirani yangu hapa mtaani anafuga ng'ombe. Kawajengea banda kwenye ukuta wa fensi niliojenga mimi na anajaza kifusi cha mavi ya ng'ombe kwenye ukuta huo na kupelekea harufu kali kwa upande wangu hasa kwenye madirisha ya nyumbani.
Naomba mbinu nzuri ya kumtia adabu iwe ya kisheria au ya kibabe. Maana haya maeneo yamepimwa kwa ajili ya makazi na sio ufugaji wa ng'ombe.
Tulishamwambia awe mstaarabu kwa kutokurundika mavi mengi ya ng'ombe na kuleta kero kwetu, tunaona analeta dharau, sasa nimeamua ubaya ubaya liwalo na liwe.
Asanteni.