Ni kero zipi uliwahi kupitia kwa kuishi na majirani wasumbufu/wakorofi?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,028
Kuna kipindi niliwahi kupanga nyumba hapo zamani, ilikuwa na miti mingi yenye matunda ndani ya fensi, nikaja kuambiwa kuna mtu huwa anakuja usiku nikizima taa anaruka ukuta anachuma matunda (asante kwa jirani yangu mzaramo alinijuza hili).

Siku ijayo usiku ulipofika nilimwambia wife azime taa mimi nikabaki nje nikatafta kasehemu kalikojificha kenye giza nikakaketi kwenye kiti cha plastiki tayari kwa kusubiri tukio, pia nilibeba tochi kubwa pamoja na bakora ndefu ya kumtembezea kioigo mhujumu wangu wa matunda.

Imefika mida ya saa tano hivi nikaiona njemba inaruka ukuta, alicheki cheku mazingira huku mimi namchora tu, alivyojiamini kwamba hali ni shwari alipanda kwenye mti wa mapera yalikuwa yameiva si mchezo.

Chap chap nikasogelea huo mti nikammulika na mwanga mkali wa tochi na kumuamuru ashuke mara moja, basi wakati anashuka akiwa anaomba msamaha mara kwa mara huku akiwa anatetemeka, kafika chini kaanza kunipa Kiswahili kwamba huo mti walikuwa na makubaliano na mwenye nyumba aliyekuwepo kabla yangu kwamba awe anayachuma mda wowote, :) :), nilimwambia kwani mimi ni huyo mmiliki aliekuwepo kabla yangu? akawa anatetemeka tu.

Nikampiga interview pale ndio akawa akaniambia ukweli kwamba anachumaga matunda mchanganyiko alafu anamuuzia mtu anaefanya biashara za matunda huko mjini.

kiukweli ilibidi nimtembezee kipigo lakini nikamchimba biti iwe mwanzo na mwisho kufanya huo ujinga,kama anataka matunda awe anakuja mchana nitampa ruksa ayachume.
 
Sasa jamaa si alikuwa akikata kimba linakuwa gumu kuliko ugumu wa maisha yenyewe uliomfanya kuiba mapera?

Au nasema uongo jaman?😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom