Mi hata leo nikiambiwa hapana ni hapana tu. Kwanza naheshimu maamuzi, pili huwa sipendi hata kidogo kufukuzia kwa sababu naamini kilicho chako huna haja ya manati. Inanikosti lakini inaniepusha na vingi pia. Wikiendi moja nikielekea Kigamboni kwenye pantoni nilimtokea mrembo mmoja matata sana, straight to the point.... akanijibu noooo. Nikamuaga na kusogea mlango wa kutokea na sikugeuka nyuma. Wakati tunasukumana kuwahi kushuka nikahisi mtu anaingiza mkono kwenye mfuko wa jeans niliovaa kugeuka ni yule dada na tabasamu halafu akapotea mbio. Poa baadae kuangalia kaweka nini ni kijikarasi chenye namba ya simu na ujumbe "HANIFA. NITAFUTE KWA 0655.... Sikumtafuta.