Jiongezee Kipato : Natafuta Mfanyakazi wa Kuziendesha Account zangu za Social Networks

SEASON 5

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
481
1,000
Kama wewe uko home tu huna kazi yeyote yawezekana upo unatafuta kazi bado hujapata au ni mama wa nyumbani,au ni kaka wa nyumbani kazi yako kubwa ni kuingia mtandaoni kusoma kuangalia dunia inaendaje nk.

Leo nimekuja natafuta mtu aina yako,ambaye ataweza Post matangazo 24/7 na kujibu comment za wateja huko Online kwa akaunt zangu mbili za FACEBOOK na INSTAGRAM .

Instagram nitakua na account Mbili
Facebook Nitakua na account Mbili

Kazi yako ni kupost insta matangazo ya bidhaaa ninazouza kila page atleast kila siku u post not less than 50 post utakazoziandikia maelezo vizuri kabisa na kwa umakini wa hali ya juu kabisa.

Si lazima upost post 50 tu kama nguvu na ari ya kazi unayo natamani upost zaidi ya hivyo,the more we get customers kupitia online the more malipo yako nitayaongeza kadri kila siku zinavyoenda.

SIFA ZA NINAE MUHITAJI

- Ajue kingereza sio lazima ajue kuongea kama obama atleast awe yule mtu ambae anaweza kujibu comment hata za wateja watakao comment kwa kingereza awajibu kama mtu alie enda shule. (asiwe wa ze ze ze ze zis zis zat)

-Awe na smartphone/PC yake yenye uwezo wa kuingia insta na FB kwa muda wote na hivi vifaaa vyake viwe vizima visiwe na shida shida mara betri bovu mara touch mbovu,awe na kifaa kizima 100%

-Awe tayari kufanya kazi ka bidiiii sana sana sana.

NAMNA YA KUIFANYA

Hii kazi utaifanya ukiwa huko huko ulipo uwe nchini uwe mkoani uwe popote pale ulipo utaifanya hii kazi kadri tu utakavyojipangia wewe namna gani na saa ngapi uingie online.

BANDO

Kila siku nitakua nakuunganisha na BANDO la 1GB huko huko ulipo na wewe utaendelea na kazi kama nilivyokuelekeza cha kufanya utafanya, Hili bando nitakuunga mimi kwa gharama zangu mimi (daily)


MALIPO

Hii kazi tutaanza na malipo ya 30,000 kwa Mwezi kwasababu ni mwanzo lakini kadri nitakavyoona utendaji kazi wako unaridhisha na naona matokeo na unavuka viwango nilivyotarajia basi nitakuongeza huu mshahara kila mwezi.

Malipo haya ya 30,000 yanaweza kupanda zaidi na zaidi hasa wateja wakitiririka wakutosha, Kama nitaona outcome Nzuri basi nadhani nitakununulia vitendea kazi vya maana na OFISI kabisa ili utoke home uwe unaenda ofisini.

Ofisi yako ni mtandaoni kufanya matangazo kupost post kwa fujo zote unazoweza wewe,Malipo ya 30,000 ni madogo lakini si haba kama utayapata.

Kumbuka malipo yako ya kuanzia ni 30,000
Vocha 1000 x 30 = 30,000

so ofisi yako kwa mwezi ina matumizi ya 60,000 ambayo kibiashara ni pesa nyingi sana,kwahyo unapofikiria kazi usijikite sana kwenye malipo waza namna ya kufanya kazi kwa bidiiii ili malipo yako yaongezeke.

ULIPWAJI

Hiii kazi malipo nitakupa mshahara baada ya kazi so ukianza kazi kesho tar 1 mshahara wako nitakuwekea kwenye simu yako tarehe 30.

Nadhani maelezo yangu yatakua yamejitosheleza kwa mtu atae ona hiii inamfaaaa.


TANGAZO LINGINE

Kama kuna kijana anaeishi mbezi ya kimara/mbezi mwisho au kuanzia magomeni to mbezi mwisho hapo katikati na anahitaji kazi ya mshahara usiozidi 50,000 kwa mwezi Akaribie PM.

MAJUKUMU YAKE

Kuja kunisaidia kazi zangu za hapa na pale hasa za kutumia computer na kufungua ofisi asubuhi mapema sana na kunifanyia usafi ofisini kisha atasubiri nikija ofisini yeye atakua huru kuondoka.

Mara nyingi nafungua ofisi saa 5 mpk saa 6 mchana jambo ambalo linanifanya nakosa wateja wa asubuhi,au kuna siku naenda kwenye mizunguko yangu nazunguka huko siku nzima nakuja kufungua ofisi saa 10 jioni au saa 12 jioni.

jambo ambalo asubuhi nakosa wateja,mchana nakosa kutokana na ofisi kuwa imefungwa,kwahiyo wewe utakua kazi yako ni kuwahi ofisini kufungua saa 1 kamili pawe wazi kisha mimi nikija kazini saa 4 au 5 asubuhi wewe utakua huna kazi tena utakua ndio ushamaliza kazi yako utasepa zako kwenu/kwako mpaka kesho tena.

siku nikiwa naenda kwenye mizunguko yangu badala ya kufunga ofisi nitahitaji ubaki ofisini mpka nitakaporudi nikisharudi hata nirudi saa 10 jioni nikifika tu nawewe ndio muda wako wakuondoka umewadia utaondoka zako.

Ki ufupi jukumu lako no. 1 ni kuhakikisha ofisi inakua wazi kuanzia saa 1 kamili asubuhi isitokee hata siku 1 wateja wakaja wakakosa huduma,nikichelewa kuja kazini wateja wa asubuhi utawahudumia.

SIFA ZA KIJANA

Ajue kutumia computer 100%
Ajue kugundua na kufahamu tatzo la kompyuta endapo itatokea ghafla kompyuta imemzimia au imegoma kuwaka
Awe mkweli na mwaminifu


Kwa yeyote ataeona ana FIT katika kazi hizo mbili hapo juuu Namkaribisha PM tuongeee na tupange zaidi.

NOTE

Ukintumia ujumbe PM ukiona nimechelewa kujibu usijali,nikirudi nitausoma na kuujibu na yeyote ataekuja PM nashauri aache na namba za simu kabisa ili nikiiingia nizichukue na kumpgia moja kwa moja. Muda wa kuchati ni mchache sana.

ASANTENI.
 
mkuu SEASON 5 unajua ugumu wa online business?!....post 50 kwa siku?!..
na bado mtu aandike kwa lugha ya kuwateka wateja halafu payment umpe 30k per mwezi?!...
yaani 1k kwa siku?!..
mkuuu kazi yeyote ni kuridhia kwanza,unapoona tangazo la kazi flani unalisoma kisha unajipima Je naliweza? napata maslahi? ukiona hailipi Unaliacha tu mkuu.

Hamna kazi rahisi na ingekua nyepesi nadhani nina vitendea kazi vyote lakini yamenishinda na uwezo wangu wakulipa ni hiyo 30k ambayo ni 1k kwa siku.
 
Mkuu, I can fit your advert, ninafanya online freelancing, nina own PC na smartphone. I use about 15 hrs on PC a day. I would like to help you. Kama utaona ninafaa, we can talk via PM.

Naomba ya kwanza, #Social media management. Maana niko mkoani.

Looking forward to hearing from you.
 
Mkuu, I can fit your advert, ninafanya online freelancing, nina own PC na smartphone. I use about 15 hrs on PC a day. I would like to help you. Kama utaona ninafaa, we can talk via PM.

Naomba ya kwanza, #Social media management. Maana niko mkoani.

Looking forward to hearing from you.
Sasa changamkia basi andika msg kwenye PM yake kabla watu hawajakuwahi. Watu kama mimi naweza kuamua kufanya bila hata malipo kwani nina likizo ndefu na connection ya Internet ni 7/24, PC ya kisasa kabisa na speed ya Internet ni 1gbps. Nikiamua nafanya tu ili ku-pass time na kugundua mambo mapya! 🤣 🤣
 
Sasa changamkia basi andika msg kwenye PM yake kabla watu hawajakuwahi. Watu kama mimi naweza kuamua kufanya bila hata malipo kwani nina likizo ndefu na connection ya Internet ni 7/24, PC ya kisasa kabisa na speed ya Internet ni 1gbps. Nikiamua nafanya tu ili ku-pass time na kugundua mambo mapya! 🤣 🤣
Haha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom