Jinsi ya uchanganyaji wa chakula cha kuku!

M-pesa

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
602
151
mwenye kufahamu rationing ya chakula cha kuku wa nyama si vibaya akiweka hapa jamvini ili wadau wenye kuvutiwa na hii kitu wanufaike.
Ninasikia tu kwamba mahitaji ni dagaa, chokaa/kombe/mifupa, pumba za mahindi, mchanga, damu ya ng'ombe iliyogandishwa n.k.
Asanteni
 
Mods tusaidie kulink na topic za huko nyuma nakumbuka ilishwahi ongelewa hii kitu nami nahitaji hii taarifa; lakini mdau kama uko dar fikapale jengo la wizara ya kilimo na chakula kuna handaouts nzuri sana na waweza kukutana na washauri wahusika ama watu wa idara ya kilimo upande wa ufugaji!
 
Ushauri: kama una mradi wa kuku wengi, ukitengeneza hiko chakula fanya najaribio kwa kuku wachache kama ukuaji wao utakuwa mzuri. Niliwahi kupewa formula tena kwa gharama ilikuwa kubwa kuliko kununua chakula lakini kuku walidumaa.
 
Jana kuna mtaalamu aliweka uzi jinsi ya kufuga kuku wa kienyeji aliweka mchanganuo mzuri sana jaribu kuutafuta then um pm atakusahdi kwa sababu kama anaweza fuga kuku wa kienyej na uakika hata wa kisasa awatampa taabu kukupa mchanganuo wa jinc ya kuchanganya chakula.
 
shukrani mkuu!

asante sana mkuu nitajitahidi kufanya hivyo
Mods tusaidie kulink na topic za huko nyuma nakumbuka ilishwahi ongelewa hii kitu nami nahitaji hii taarifa; lakini mdau kama uko dar fikapale jengo la wizara ya kilimo na chakula kuna handaouts nzuri sana na waweza kukutana na washauri wahusika ama watu wa idara ya kilimo upande wa ufugaji!
 
Habari wote jamani, ni kweli inabidi mods watusaidie kuhusu kuziunganisha hizi maana mamabo mengi tunajifunza hapa, kila mara ninarydi hapa na kuchota mambo mapya.
Sasa kuhusu chakula naomba nikushauri kwa kuanzia jaribu kununua hata starter tu kwa wauzaji wazuri, kichunguze sana uone harufu rangi na texture yake, waweza kusaga kiasi kwa ajili ya finisher huku ukiangalia kuku wanakuwaje. mfano mashudu mengi bila mahindi kwenye finisher yanafanya kuku wako anakuwa mafuta mengi sana ila uzito hana na mahindi mengi paraza yanasaidia uzito mkubwa kwa kuku, vilevile uongezaji wa kuku bora inasaidia ukingaji wa magonjwa mbalimbali,
Nakushauri nunua mifuko michache ya kuanzia, nunua vitu vyote vinavyohitajika kwa kusaga kwenye mashine mfano 'Hill...' iko maeneo ya Bunju njia ya bagamoyo wanasaga na kuuza hivyo vyakula na vikorokoro vyoote vinavyohitajika. Unakuwa na chakula chako kama backup na cha kununua hadi ujue jinsi gani kuku wanakula, wanaadhiriwa na vyakula. Round ya pili utakuwa umeishajua ufanye nini moja kwa moja. Kama unatoka mbali waweza nunua vitu muhimu tu na mahindi na vitu vingine ukaenda nunua jirani na shamba lako. Naweka mchanganuo niliwahi pewa na mfugaji mwenzangu unasaidia, pia na mwongozo kidogo wa ufugaji toka wizara husika. Usisite kuwauliza mashine kama formula yako imepunguka vitu wanaweza kuwa msaada zaidi.
 
Attachments

  • Kuku wa kisasa.xlsx
    12.5 KB · Views: 739

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom