Jinsi ya mzazi kumchukulia cheti cha sekondari mtoto wake aliye nje ya nchi

UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
3,446
5,414
Jamani naomba kupata maelekezo kuna uwezekano kwa mzazi kumchukulia mtoto wako cheti chake cha form four au six kama yeye mwenyewe hayupo nchini na nina documents zote zinazoonyesha hayupo.

Cheti original kinahitajika chuoni alipo. Je, kuna uwezekano wa mzazi kukichukuwa? Na je, utaratibu upoje?

Kama nimeweza kumlipia karo miaka yote hata cheti siwezi kupewa? Jamani naomba mwenye kuelewa utaratibu anisaidie.
 
Unaonaje ukifika shuleni kwa mtoto ili uweze kuonana na uongozi wa shule kujua kama watakupa.
Nimeenda na wanasisitiza mwongozo wa wizara unaeleza utaratibu .Utaratibu wanasema ni mwanafunzi kuja mwenyewe na picha yake ,kitambulisho na kaweka alama ya dole.Hawamtambui mzazi hata kama umelipa wewe Ada,una viambatanisho vyote kuwa wewe ndio mzazi
 
Nimeenda na wanasisitiza mwongozo wa wizara unaeleza utaratibu .Utaratibu wanasema ni mwanafunzi kuja mwenyewe na picha yake ,kitambulisho na kaweka alama ya dole.Hawamtambui mzazi hata kama umelipa wewe Adams,una viambatanisho vyote kuwa wewe ndio mzazi
Basi kama utaratibu ndiyo huo itabidi ufuate.
 
Sasa si uwasiliane na shule husika? Au mwanzo alisomea jamiiforums sekondari
Nimeenda ndugu ,wamenikatalia na hawatoi na wanasema hakuna alternative. Sasa nikajiuliza kama motto akinipa power of attorney bado wamesema haiwezekani.Sasa mwenye kujua unafanyaje.Mimi naming kuna alternative
 
Nimeenda ndugu ,wamenikatalia na hawatoi na wanasema hakuna alternative. Sasa nikajiuliza kama motto akinipa power of attorney bado wamesema haiwezekani.Sasa mwenye kujua unafanyaje.Mimi naming kuna alternative
Mwanao kahitimu mwaka gani?
 
Mwaka hu, ndio vyeti vimetoka viko mashuleni
Mlete achukue cheti chake. Maana wizara inamjua mwanafunzi na siyo mzazi. Kuna mahala unakiri kuwa wanataka asaini na aweke alama ya dole gumba.

Kwenye mambo hayo ni suala gumu kufanikisha bila mhusika mwenyewe kuwepo. Labda angekuwa mgonjwa taabani au hayupo katika ulimwengu wa mwili ila kama yupo lazima wampe yeye.
 
Sina jibu hapa lakini swala la vyeti Tanzania ni pasua kichwa-imagine unasoma Mtwara Chuo na unatoka Mwanza, halafu ukienda graduu unakuta vyeti bado na chuo kinataka ufunge safari nyingine toka Mwanza hadi Mtwara kufuata cheti tu na lazima uende wewe mwenyewe.

Nilifikiri miaka inavyosonga na technology kuwa makini ingewezekana mwanafunzi ambaye hadaiwi kitu apelekewe cheti chake au siku ya graduu kwa vyeti vya vyuo viwe tayari lakini kwa vyuo vingi sivyo kabisa.

Kwa mimi niliesoma zamani sielewi kabisa vyeti vyangu viwili nilitumiwa toka nje ya nchi, cha form 6 nilitumiwa na shule. Wizara, NACTE, NECTA na TCU na vyuo wanatakiwa warejee tena kwenye hili swala.
 
Sina jibu hapa lakini swala la vyeti Tanzania ni pasua kichwa-imagine unasoma Mtwara Chuo na unatoka Mwanza, halafu ukienda graduu unakuta vyeti bado na chuo kinataka ufunge safari nyingine toka Mwanza hadi Mtwara kufuata cheti tu na lazima uende wewe mwenyewe. Nilifikiri miaka inavyosonga na technology kuwa makini ingewezekana mwanafunzi ambaye hadaiwi kitu apelekewe cheti chake au siku ya graduu kwa vyeti vya vyuo viwe tayari lakini kwa vyuo vingi sivyo kabisa.
Kwa mimi niliesoma zamani sielewi kabisa vyeti vyangu viwili nilitumiwa toka nje ya nchi, cha form 6 nilitumiwa na shule. Wizara, NACTE, NECTA na TCU na vyuo wanatakiwa warejee tena kwenye hili swala.
Yes zamani mzazi aliruhusiwa pia kuchukua.Kwa sasa wanasema watu wanafoji au kuvitumia.Cha kushangaza docs nyingi sensitive watu wanachukuliana ikiwepo passport nk nashangaa cheti chenye picha na kila kitu kiko kwa mtandao.Imagine mzazi aliyelipa Ada naye hana uwezo wa kuchukua hata kwa kutumika chochote kisheria.nimeshangaa sana.Walioko wizarani watuambie tufanyeje
 
Yes zamani mzazi aliruhusiwa pia kuchukua.Kwa sasa wanasema watu wanafoji au kuvitumia.Cha kushangaza docs nyingi sensitive watu wanachukuliana ikiwepo passport nk nashangaa cheti chenye picha na kila kitu kiko kwa mtandao.Imagine mzazi aliyelipa Adam naye Jana uwezo wa kuchukua hata kwa kutumika chochote kisheria.nimeshangaa sana.Walioko wizarani watuambie tufanyeje
Kwa sasa ni rahisi zaidi kutambua vyeti feki na pia mawasiliano ni rahisi zaidi kwa mwenye cheti kuomba nani apewe cheti chake ampelekee au kupostiwa. Basi tu tuna mawazo mgando au hatutaki kufikiri.
 
Mimi nilishamchukulia ..... cheti chake.

Aliandika barua ya mimi kuomba kumchukulia cheti chake. Nilitoa copy vitambulisho vyangu wakanikubalia.
 
Mimi nilishamchukulia ..... cheti chake.

Aliandika barua ya mimi kuomba kumchukulia cheti chake. Nilitoa copy vitambulisho vyangu wakanikubalia.
Wewe ulikuwa kama mzazi au.Nimemwambia mwalimu mkuu wa shule kama mwenyewe kupitia mwanasheria anaweza kuandika barua wanasema mwongozo unakataza.Nimejichokea na hiyo miongozo kwa kweli kwani Ada nilipe then cheti siruhusiwi
 
Back
Top Bottom