Jinsi ya kutunza Watoto Njiti katika chumba maalum

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
20210225_083702_0000.png


Kuhakikisha ngozi ya mtoto inakuwa imegusana na ngozi ya mama ( skin to skin contact/ kangaroo mother care). Hapa mama anashauriwa kumbeba mtoto kwa kumgusisha katk ngozi ya mama uda mwingi ili kumkinga mtoto kupoteza joto.

Ii/Kumfunika mtoto kwa nguo nzito iliasipoteze joto. Nguo hizo lazima ziwe safi muda wote ili mtoto asipate homa itokanayo na vijidudu kama vile bacteria nk (sepsis)

ii/ Njia nyingine ni kuwaweka watoto hao katika mashine maalum yenye hewa iliyopashwa joto(Air-heated Incubator) ambayo ina joto kadri ya mahitaji ya mtoto njiti.

iii/ Njia nyingine ni kutumia matandiko ambayo yana mzunguko wa maji yaliyopashwa joto(Heated water-filled mattress)

Iv/ Mashine nyingine ni ile inayotoa joto ambalo humfikia mtoto mfano wa joto la jua linavyotufikia(Overhead Radiant warmer). Ambayo picha yake imeonyeshwa hapa chini. Mashine hizi zote zinahitaji uangalizi wa karibu sana muda wote mtoto awekwapo katika mashine hizo ili kkugundua mabadiliko yoyote kwa mtoto na kuchukua hatua mara moja

Overhead Radiant warmer
v/ Njia nyingine ni kumpaka mtoto mafuta(Oil application) mafuta husaidia kuziba vitundu vidogovidogo vilivyo katika vinyweleo katika ngozi ya mwili ili kuzuia joto kupttea kupitia vitundu hivyo

Vi/ Njia nyingine ni kumfunika mtoto kwa mfuko maalum unaojulikana kama polythene sheet.mfuko huu ni maalumu kwa watoto lakini unafanya kazi sawa na mifuko mingine wanayotumia mama ntilie kufunikia vyakula visipoe kama vile maandazi na wali,kwa sababu unazuia joto kupotea

Vi/ mtoto azaliwapo mwili wake huwa umefunikwa na kitu mafuta mazito kama girisi,( Vernix caseosa) wengine huona kama ni uchafu la! Kama mtoto amezaliwa njiti usijaribu kutoa maana utasababisha ngozi ya mtoto kuwa wazi hivyo kupoteza joto kwa wingi.

Vii/ Mtoto njiti asiogeshwe mpaka siku aliyo tarajiwa kuzaliwa ifike, hivyo hakikisha mazingira ya kumhudumia yanazingatia usafi wa hali ya juu(Neonatal Intensive Care Unit Protocol)

VIII/ Hakikisha mtoto anapata lishe kwa mujibu wa taratibu za kulisha watoto njiti(Neonatal and low birth weight feeding schedule
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom