Jinsi ya kutoka kwenye kifungo cha madeni

Jinsi ya kutoka kwenye kifungo cha madeni

stabilityman

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2024
Posts
852
Reaction score
1,805
JINSI YA KUTOKA KWENYE KIFUNGO CHA MADENI

Hii ni kwa wale walioko kwenye madeni tayari.


01.ONGEZA KIPATO CHAKO

Hakikisha unaongeza uzalishaji wa kipato chako, tafuta somo linaloeleza Jinsi ya kuongeza kipato chako hapa Darasani.Hakikisha matumizi huongezi.

02.PUNGUZA MATUMIZI YAKO

Lengo ni kutoka kwenye madeni sasa ongeza kipato lakini pia jibane sana ili upate Pesa ya watu.

03.ONGEA NA MDENI WAKO

Nenda ukamwelekeze ukweli,na uonyeshe nia ya kulipa mapema,ili akuongezee siku au muombe umlipe kwa awamu awamu,omba riba isimame n.k nae ni Binadamu atakuelewa ukienda mapema zaidi.


04.UZA MALI ZA THAMANI ULIZONAZO

Hakikisha unauza mali ya thamani upate pesa ya kulipa deni lako mfano uza aridhi n.k ukiuza mwenyewe utapata faida kuliko akiuza MDENI wako kisa deni.

05.FAHAMU MADENI YAKO NA WEKA BAJETI YA KUYALIPA

Hakikisha unafahamu unamadeni kiasi gani weka utaratibu mzuri wa kuyalipa yote.Ukianza na deni Moja baada ya lingine....Anza na lile la usumbufu mkubwa.

06.THAMANISHA DENI LAKO NA MALI YAKO

Badala ya kumpa Fedha ongea naye mpe kitu au mali yenye thamani ya hicho anachokudai....mfano gari,shamba,pesa nusu na kiwanja,n.k

07.ACHA KUENDELEA KUKOPA.

Kuna watu huwa watumwa wa mikopo.

Akikopa deni la kwanza akaanza kudaiwa anakopa tena kwingine mwisho wa siku anakuwa na madeni hata 10.Acha kabisaaa kukopa tena.Uanze kurudisha pesa za watu.


Umejifunza nini hapa
Mimi naitwa James ni mtaalamu wa kuchora raman za nyumba 0743 257 669
a swali gani?

Comment hapa chini....
 
Back
Top Bottom