Jinsi ya kuthibitisha PIN Google Adsense

Bonge Mpya

Member
Jul 6, 2021
12
45
Habari zenu

Sina hakika kama hili ni jukwaa sahihi kwa hii mada, lakini Naomba kuiwasilisha humu kwa mwenye kufahamu basi anifahamishe.

Nimekuwa nikijihusisha na Blogging kwa miaka 4 sasa na nimepata uzoefu mkubwa sana kuanzia kwenye kutengeneza blog, kuendesha blog na ku-brand. Kufikia mwezi wa 6 mwaka huu yaani mwezi uliopita nikaamua ku-apply kwenye matangazo ya Google (AdSense) na ndani ya siku mbili blog yangu ikawa imekubaliwa.

Baada ya kufatilia kwa umakini hatua za malipo ya AdSense nikapata kujua kuwa ni lazima kufanya PIN verification ambapo Google wanatuma barua au mail kwenye sanduku la posta uliloandika.

Sasa shida yangu iko hapa kwenye kupokea barua. Kwa yeyote aliewahi kupokea barua au hata kusikia mtu aliwahi kupokea barua Naomba nijulishwe anuani au sanduku la posta (P. O. BOX) alilotumia kupokea barua ili na Mimi nitumie sanduku hilo hilo.

Asanteni
 
online24

Member
Jul 20, 2020
97
150
Cha kwanza kabla ya kupokea PIN CODE za ggogle lazima ufanye yafutayo,:
1.Uverify Identity: Ili google waweze kukutumia PIN code lazima ufanye ichi kitu ili gogle wakutambue mtu wanaemtumia ni mtu kweli, ili kuverify Identity unaambatanisha Kitambulisho chako either cha mpiga kura au chaTaifa au Lesseni ya Udereva, hakikisha ivi vitambulisho vina majina sawa na majina yako ya account yako ya Email uliyofungulia iyo Adsence.
2. Ukishakamilisha iyo hatua sasa hakikisha umejaza Addres yako vizur ili uweze kutumiwa PIN code kutoka google. Address yako ndo watakayoitumia kukutumia barua yenye izo PIN code, hakikisha unaeka sanduku la posta ambalo liko Active
 
Bonge Mpya

Member
Jul 6, 2021
12
45
Cha kwanza kabla ya kupokea PIN CODE za ggogle lazima ufanye yafutayo,:
1.Uverify Identity: Ili google waweze kukutumia PIN code lazima ufanye ichi kitu ili gogle wakutambue mtu wanaemtumia ni mtu kweli, ili kuverify Identity unaambatanisha Kitambulisho chako either cha mpiga kura au chaTaifa au Lesseni ya Udereva....
Asante kwa elimu ya ziada. Mkuu shukran
 
Kylan

Member
Feb 5, 2017
52
95
Asante sana. Vipi nikitumia hata haya masanduku ya posta ya mashuleni

Lakini mi navyofahamu sanduku la posta ni kama kituo cha mzigo wako kufikia, sio lazima umiliki sanduku.

Unachotakiwa kufanya ni kuchagua posta unayotaka kupokelea hiyo barua. Mfano kama hiyo posta ipo Ubungo basi unachagua namba ya sanduku tu kwa mfano 100 na anwani yako itasomeka kama ifuatavyo:

SELMAX,
P.O BOX 100,
UBUNGO - DAR ES SALAAM

Barua itafika posta ya Ubungo kwenye sanduku 100 kwa jina la SELMAX. Na posta wanakupigia poa simu kama barua itakuwa na namba ya simu au ukienda kuiliza watakuuliza ulituma sanduku namba ngapi na jina ulilotumia mfano hapo, sanduku namba ni 100 na jina ni SELMAX.

Mimi hufanya hivyo ninavyonunua vitu AliExpress na huwa nabadili anwani kama nataka kupokelea mzigo sehemu tofauti.
 
Ahaa asante sana... Wewe huwa unatumia sanduku namba ngap ambalo liko active. (Kama Upo ubungo)
 
Kylan

Member
Feb 5, 2017
52
95
Ahaa asante sana... Wewe huwa unatumia sanduku namba ngap ambalo liko active. (Kama Upo ubungo)

Active kwa maana ya linalolipiwa na mtu au shirika fulani ambapo wanakuwa na funguo kabisa?

Kwa ufupi masanduku yote ni active kwa sababu wanaoyamiliki ni wao posta na wanafunguo zote. Mi huwa natumia 141 kwa sababu ni sanduku nililokuwa nikilitumi toka nikisoma nikalifanya kama langu japo silipiii na badili tu maeneo ya kupokelea mzigo kwa sanduku hilo hilo.

Wewe chagua sanduku lolote mfano kuanzia moja mpaka mia au mia tano. Mzigo ukifika kama wao posta hawatakupigia watauweka kwenye hilo sanduku kama unawekeka mfano barua lakini hutaweza kuuchukua kwa sababu humiliki hilo sanduku kwa maana huna funguo, kwa hiyo utaingia moja kwa moja ofisini kwao wao watakupatia baada ya malipo.
 
Ahaa Sawa nimeshakuelewa bro... Asante sana
 
Bonge Mpya

Member
Jul 6, 2021
12
45
Selmax kwahiyo umekaa miaka minne yote bila kuwa na ads. Unapataje hela sasa miaka yote hiyo
Mwanzoni nilikuwa naitumia tu kwa ajili ya mafunzo. Badae nkaanza kuweka content na watu wakavutiwa. Hapo ndipo nikaanza rasmi kufanya Blogging, ilikuw mwaka jana mwezi Juni.
Baada ya kuwa napata moderate traffic ndipo likaja wazo la kuweka matangazo ili kujipatia pesa ya blog kujiendesha.
Nafikiri changamoto uliyopo mbele ni kubwa kwasababu sioni watanzania walioweka wazi kuhusu AdSense halisi. Wengi wanaelezea tips tu on what AdSense is and how it makes money.
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,261
2,000

Ulitumia muda mwingi sana kujifunza. AdSense hailipi sana ila ni ya kuanzia. Mtiti uko kwenye payment methods, tafuta nyuzi nyingi za website humu zipo ikibidi tag wale unaoona walitoa nondo.

Unatoa contents za lugha gani. Una viewers wangapi kwa mwezi
 
Bonge Mpya

Member
Jul 6, 2021
12
45
Ulitumia muda mwingi sana kujifunza. AdSense hailipi sana ila ni ya kuanzia. Mtiti uko kwenye payment methods, tafuta nyuzi nyingi za website humu zipo ikibidi tag wale unaoona walitoa nondo.

Unatoa contents za lugha gani. Una viewers wangapi kwa mwezi
Mwanzoni nilikuwa natumia Kiswahili lakini nikajagundua kwamba post za kiswahili haziend kabsa views ni chache. Nikaamua kubadili lugha na kutumia English kwasabab contents zangu zinaweza kusomwa na yeyote duniani na akafaidika.

Wakati natumia Kiswahili nilikuwa napata views elfu 8,9,10 hadi 11 kwa mwezi lakini tangu nimeanza kuandika kwa kingereza kwa mwezi napata views elfu 55, 60, hadi 65
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,261
2,000
Mwanzoni nilikuwa natumia Kiswahili lakini nikajagundua kwamba post za kiswahili haziend kabsa views ni chache. Nikaamua kubadili lugha na kutumia English kwasabab contents zangu zinaweza kusomwa na yeyote duniani na akafaidika.

Wakati natumia Kiswahili nilikuwa napata views elfu 8,9,10 hadi 11 kwa mwezi lakini tangu nimeanza kuandika kwa kingereza kwa mwezi napata views elfu 55, 60, hadi 65
Sasa mzee kwa hiyo views 50k unatakiwa uwe na hela kabisa. Binafsi sina blog ila kwa ninaosoma shuhuda za waandishi wa nje kwa views 50k unaweza ingiza mpaka $500 ukizingatia na niche yako ni nini. Umechelewa sana kuanza monetization. Tatizo kubwa sisi hatuna PayPal ambayo ni rahisi zaidi

Bongo sio wasomaji ukiandika Kiswahili unajichosha labda uwe famous kama kina Bongo5 na uandike umbea. Ningependa kujua zaidi kutoka kwako
 
Nilipata wazo la kuweka AdSense hivi karibuni na tangu niweke AdSense leo ni siku ya 8 inasoma dola 9. Kutokana na kutofahamu huko mbele itakuaje kwenye malipo ndio maana nikaja kwenye jukwaa hili ili kufahamishwa processes zote.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom