Schengen sio Nchi, ila ni Mji mmoja wapo katika nchi ya Luxembourg, ambako mkataba wa kuondoa vikwazo mipakani kwa baadhi ya nchi za Ulaya ulisainiwa, mnamo mwaka 1985. Mkataba huu wa kuondoa vizuizi mipakani ulisainiwa na nchi tano kwanza, ambazo ni Ubelgiji, Ujerumani (enzi hizo ilikuwa Ujerumani Magharibi), Ufaransa, Luxembourg na Ubelgiji. Kwa sasa nchi zinahusika na mkataba huo zimeongezeka na kufikia 26, zikiwemo Sweden, Finland, Norway, Ugiriki, Italia nk. Uingereza haihusiki na mkabata huo.
Mkataba huu pia ni tofauti na ule wa EU, kwa sababu baadhi ya wanachama wa Schengen si wanachama wa EU, kama vile Uswisi na Norway.
Nadhani nimefafanua kidogo.