Mbwa dume
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 5,844
- 9,988
Heshima kwenu wadau wa jukwaa hili tukufu,
Ingawa mimi si mgeni humu ila nina muda kidogo sijaingia zaidi ya kupita tu japo nashangaa hawa jamaa wamebadilisha muonekano mzima wa JF tofauti na tulivyozoea mwanzo.
Nisiwachoshe niende kwenye jambo hasa lililonileta;
Kuna mtu niliwahi kutana naye kipindi cha nyuma sana nikiwa Dar huyu jamaa alisema anao uwezo wa kupanua ukubwa wa memory card yoyote ndogo kuwa kubwa! Sikuamini ila nilimpa memory ya simu yangu ilikuwa na 2 GB lakini alipoichomeka kwenye laptop yake akachukua kama dakika 3 akanipa memory nilipoweka kwenye simu yangu ikasoma 8GB! na mpaka leo naitumia.
Tatizo jamaa hakutaka kuweka wazi ni software gani anatumia nimejaribu ku-google nikakutana na software moja hivi inaitwa memory stick driver increaser nimeidownload lakini nimeitumia haikufanikiwa kupanua memory yoyote!
Najua humu jukwaani kuna watu wa kila aina kuna wataalamu wa hizi makitu naomba maujanja iwe ni link ya kudownload hizo software au hata Torrents.
Natanguliza shukrani