Fahamu jinsi ya kuondoa write protection kwenye flash au memory card

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Maujanja ya kuondoa Write Protection kwenye flash au memory card

Neno write protection sio ngeni kulisikia ila kama bado basi ni hile hali ya flash / memory card kuweza kuwa protect na hivyo kushindikana kufutwa chochote kile kilichomo ndani yake Kazi yako inakua unasoma kilichopo ndani tu "read only"

hivyo huweza kukupa ugumu wewe wa kutoweza kuingiza chochote kwenye hiyo flash Wala kufuta

Leo nitawaambia njia ya kuondoa lakini Kuna njia mbili za kufuata

Ondoa Physical write protection
njia hii ni rahisi unachotakiwa kufanya ni kuweza kuangalia kama flash yako au memory card yako Ina lock pembeni sasa utakuta kwenye flash au card reader utakuta Kuna ki lock kidogo ambacho uweza kulinda data zako zisiweze kufutwa

Unaweza kusogeza picha hili kuona zaidi kama akuna ki lock na bado hiyo protect basi soma hii njia nyingine

Remove Write Protection kwa kutumia Window
kwa kutumia Window fanya hivi hakikisha kwanza account ya window ni administrator usingie kama guest . alafu fanta hivi

tafuta sehemu ya kusearch Kisha tafuta neno CMD kisha run as administrator au bonyeza button ya window na R kisha andika CMD run as administrator kwa kubonyeza shift + alter + enter.
andika diskpart kisha enter
andika list disk kisha enter
baada ya hapo chagua SD card Yako utakuta disk 0 ya window yako hivyo utaangalia flash au Sd card Yako namba hipi kisha utaandika select disk 1 au 2 kisha enter >> kisha andika hivi attributes disk clear readonly piga enter

baada ya hapo utaweza kuondoa Flash au memory card yako kwenye write protection kupitia kompyuta Yako

Ebu tuambie ulikua unafanyaje kuondoa Flash au memory card hiko write protected tuachie maoni sasa.

Jifunze matatizo mbalimbali ya simu kompyuta app games software pamoja na suluhisho zake pia maujanja ya teknolojia kwa ujumla karibu katika page yetu.
 
Nzuri sana
Mimi mkuu ni kila ninapoweka kitu kwenye Flash yangu vinakataa kusoma yaani Kama ni video basi zitagoma ku Play au Audio zitagoma nazo..

Nimejaribu ku fomart nako inarudi pale pale
Je nijaribu njia gani ikubali? Ukubwa ni 64 GB
 
Nzuri sana
Mimi mkuu ni kila ninapoweka kitu kwenye Flash yangu vinakataa kusoma yaani Kama ni video basi zitagoma ku Play au Audio zitagoma nazo..

Nimejaribu ku fomart nako inarudi pale pale
Je nijaribu njia gani ikubali? Ukubwa ni 64 GB
Je umejaribu ku format kwa njia gani tumia cmd ku format mkuu ikikataa basi flash Yako sio original ni fake na inakaribia kufa kabisa


Ukitaka kujua kha flash yako original au fake tembelea page ya Instagram

Login โ€ข Instagram utajifunza sasa
 
Je umejaribu ku format kwa njia gani tumia cmd ku format mkuu ikikataa basi flash Yako sio original ni fake na inakaribia kufa kabisa


Ukitaka kujua kha flash yako original au fake tembelea page ya Instagram

Login โ€ข Instagram utajifunza sasa
Nipe command za ku format kwa cmd from the scratch huenda ikapona ikishindikana hapo basi naitupa
Sijanunua leo mkuu ni ya zamani sana
 
Nipe command za ku format kwa cmd from the scratch huenda ikapona ikishindikana hapo basi naitupa
Sijanunua leo mkuu ni ya zamani sana
Run cmd as administrator
Kisha andika
Diskpart piga enter
List disk piga enter
Select disk utachagua disk Yako hapo mkuu kisha utapiga kama 1 2 au 3 na nk ki sha piga enter

Clean piga enter
Create partition primary piga enter
Active piga enter
Format fs= fat32 piga enter subir imalize mpaka 100

Baada ya hapo andika exit piga enter
Kisha exit tena piga enter tumia flash Yako
 
Back
Top Bottom