jinsi ya kupambana na MFUMO DUME.

jinsi ya kupambana na MFUMO DUME.

notifeki

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2013
Posts
402
Reaction score
283
Kuna malalamiko mengi kuhusu mifumo ya kijamii katika nchi yetu inayoonekana kuwa kikwazo kwa maendeleo ya aina fulani ya wanajamii wetu. Example mifumo dume na mifumo kristo.

ntatoa dokezo dogo la namna ya kupambana na mojawapo ya mifumo unaorudisha nyuma maendeleo ya wanajamii wenzetu a.k.a mfumo dume. Next time ntaongelea mfumo kristo.

NAMNA YA KUPAMBANA NA MFUMO DUME:
1. Wanaume kuacha kutoa mahali, wanawake watoe mahali.
2. Wanaume waache kuhudumia familia zao. Wanawake wahudumie familia kifedha.
3. Wanaume waache kulipa bili za baa. Wanawake walipe bili za vinywaji na nyama choma baa.
4. Wanaume waache kuhonga wanawake magari, nyumba, simu, school fees. N.k. Wanawake wawahonge wanaume.
5. Wanaume waache kulipa matunzo ya watoto a.k.a child support.
6. Viti maalum kwa wanawake vifutwe.Wanawake wapewe haki ya kugombea kama wenzao wanaume.
7. Wanajeshi mstari wa mbele wawe wanawake.
8. Kama unapinga mfumo dume ongezea hoja.
 
Wanawake tunawapenda kama dada zetu, binti zetu, mama , shangazi zetu. Cha ajabu tumekuwa tukiwabagua kwa kuwaona tofauti na dhaifu kuliko sisi. Tubadilike tuwape haki kama wanaume wenzetu a.k.a usawa. To hell with mfumo dume. TAMWA mniunge mkono hapa.
 
hapo namba 1 , 2 na 4, mbona wanaume kibao siku hizi wameolewa?????? Wanawekwa mjini na wanawake??????? Wanawake ndo watunza familia....(idadi ya wanaume inazidi kupungua siku hadi siku, )

Anyway definition yako ya mfumo dume ni ipi?

halafu mfumo kristu ndo nini?
 
Wewe sema tu unataka kuhalalisha uhongwaji kwa wanaume na wasifanye kazi.
Sasa mimi nikihudumia familia,kulipia bills,fees&et al.
Hizo hela za mwanaume zina kazi gani???au ndo kuzipeleka nyumba ndogo??
Au yeye anakuwa hana kazi anakuwa mariyooo???
Njia pekee ni kujitambua sisi wanawake na kusimamia imara.
Hayo mengine naona unapigia debe umariyooo.
 
Hiyo namba sita tu ndo umepatia. Hizo zingine zote tutatengeneza mfumo jike na kuanza kupambana nao. Tunahitaji equal treatment. Namuhonga nae ananihonga pia. Tunahongana. Mara ngapi mwanamke anamhudumia mwanaume tena bila masengenyo wala nini?
 
Sidhani kama unaelewa maana ya mfumo dume. Haki ni tofauti ni majukumu. Vyote ulivoorodhesha si mambo ya haki, ni majukumu au tabia ambazo wanaume wanazo katika jamii yetu. Anyways labda unatania sababu hii topic haijakaa kisiriaz sana...:glasses-nerdy:

Back
Top Bottom