Jinsi ya Kuongea na Ndugu Yako Aliyekufa

Abtali Mwerevu

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2013
Posts
796
Reaction score
707
Ndugu yako aliyekufa, anatamani kuongea na wewe, lakini wewe hufahamu njia ya kukuwezesha kuongea naye. Inawezekana mambo yamekuwa magumu na unaamini unahitaji ushauri wake, inawezekana umemkumbuka tu na ungependa uzungumze naye, na inawezekana alifariki mkiwa katika ugomvi sasa unataka mmalize tofauti zenu na pengine unataka ushauri kutoka kwake. Kwa sababu yoyote ile unaweza kuongea na ndugu yako aliyekufa!

Vifaa unavyohitaji ili kuwezesha kuongea naye

Mchele

Mchele ni zao pendwa katika nchi yetu. Ni mchele huu huleta chakula pendwa wali. Kwa hivyo mchele ni kifaa muhimu.

Pombe

Pombe itatumika katika kukuhamisha mawimbi (frequency).

Beseni lenye maji

Hii ipo kwa ajili ya kutuliza mawimbi na kufanya mtandao wa kiulimwengu ukamate vyema. Beseni la maji linafanya kazi sawa na dishi la kisimbuzi katika kuonesha channel za televisheni.

Boga la ukubwa wowote

Linasimama kama mtandao (Network).

Mziki wenye mapigo ya 520 Hz

Huu ni mahususi kwa kuondoa msongo wa mawazo na kuponya matatizo ya kisaikolojia. Ili kuweza kuongea na ndugu yako aliyekufa, unahitaji utulivu wa hali ya juu katika akili yako.

Ili kuweza kuupata muziki wa aina hii, utahitaji kukodi mpiga zeze mwenye uelewa, kama huwezi, utawasha muziki huu niliokuwekea.

View: https://www.youtube.com/watch?v=ZQkBmCJG9i8

Muziki wenye mapigo ya 852 Hz

Huu upo mahususi kwa ajili ya kuamsha jicho la tatu (pineal gland). huwezi kumuona aliyekufa bila kuamsha jicho la tatu. Ndiyo unalo jicho la tatu. Ni jicho hili ndilo hutambua mambo mengi yasiyoonekana kwa macho ya kawaida, kwa mfano, inapofika usiku, jicho la tatu, hufahamu hilo na kukutengenezea usingizi. Mwanga ukiingia hata kama umelala jicho la tatu hutambua hilo na kukufanya uamke.

View: https://www.youtube.com/watch?v=joXu1AMzzWg&t=19s

Zoezi lenyewe

Hakikisha unasababu ya muhimu ya kumuita ndugu yako ili uongee naye. Usimuite akaja halafu ukabaki huna neno, hawezi kukudhuru lakini atakutisha! Kwa hivyo kuwa na hoja za msingi umuitapo.

Siku tatu kabla hujafanya zoezi la kuzungumza naye, mfikirie yeye tu. Kila unapotembea, unapofanya kazi mfikirie. Kumbuka mambo aliyowahi kufanya na muwaze sana. Ukimaliza hatua hii, ingia katika zoezi rasmi.

Saa sita usiku

Mchele kilo moja, weka katika beseni.

Pombe ya asili majagi mawili. Kama huna au huifahamu, nunua bia nne.

Beseni lenye maji liwe pembeni.

Boga.

Mpiga zeze kama ulimpata, au tumia simu yako kucheza miziki iliyoelekezwa.

Mpangilio

Kaa katikati ya mchele, beseni, na boga. Yaani, mchele uwe kushoto, beseni la maji liwe kulia na boga liwe mbele yako. Mpiga zeze kama yupo atakaa mbele ya boga. Kama unatumia simu kucheza muziki wa mapigo tajwa, kaa nayo simu hiyo. Pombe zako uwe nazo hapo ulipokaa.

Dakika tatu

Tumia dakika tatu kumfikiria ndugu yako. Kisha fungua pombe ya kwanza ili uanze zoezi rasmi la kuhama mawimbi (frequency) kunywa pombe zako ukiwa unasikiliza ule mziki tajwa. Bia ya kwanza na ya pili, sikiliza 520 Hz, bia ya tatu na nne sikiliza 852 Hz.

Ukimaliza, pombe zako, anza kumuita ndugu yako taratibu,usiwaze kitu chochote. Kama ndugu yako ataona wewe si muoga, atakuja. Ongea naye shinda yako bila kuogopa.

Endapo utamuita kwa dakika 20 mfululizo naye asije, maana yake ni kwamba, ndugu yako ameona wewe ni muoga. Ameamini kwamba akikutokea utakimbia na hutafanya chochote. Basi ndugu yako huyu anasubiri ulale ili akutokee ndotoni.

Kama ndugu yako hakutokea, kaa saa moja, kisha nenda msalani kutoa haja ndogo, halafu rudi kulala. Unapolala, mfikirie ndugu yako, fikiria umuhimu wa wewe kuongea naye.

Basi utakapokuwa umelala, saa la kwanza utakuwa katika usingizi mwepesi, saa la pili utazama kidogo, saa la tatu utakuwa ndani kabisa usingizini, nalo saa la nne, utakuwa katika ndoto, utamuona ndugu yako katika ndoto, mweleze shida yako, mweleze jambo lako.

Nakutakia kila la heri.

Kama Una Swali, Uliza Nitajibu, au Wasiliana Nami Moja Kwa Moja Kwa Kugusa Hapa.
 
Kama hutumii pombe inakuaje sasa?
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
download (3).jpeg
 
Hivi ndivyo asemavyo Bwana kuhusu wafu na Mungu si mwanadamu aseme uongo

AYU. :7:9
Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa.

MHU. :9:5
kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.

MHU. :9:6
Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.

Huyo atakayekuja/atakayetokea ni jini lililochukua sura ya ndugu yako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom