Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
1. Usimsahihishe mwenzi wako hadharani mbele ya umma au kundi la watu, Inamfanya aone aibu.

2. Usimfokee au kumkaripia mwenzi wako unaporekebisha.

3. Usitumie maneno kama "Hautawai...", au "Wewe kila mara...". Kufanya hivyo ni kuchochea visa. Tumia maneno kama "Sidhani kama ilikuwa sawa ulichofanya jana"

4. Usimsahihishe mwenzi wako kana kwamba ni mtoto ukisema "Tafadhali tenda sambamba na umri wako", "Wewe ni mtu mzima bwana", "Kua", "Wewe ni mtoto sana", "Una kuwa kama mtoto", "Una utoto mwingi" na kauli za namna hiyo. Hii haionyeshi heshima

5. Usimsahihishe mwenzi wako kuhusu jambo zito wakati nyinyi wawili hamna muda wa kutosha wa kulizungumzia. Fanya hivyo katika hali ya utulivu.

6. Unapomsahihisha mwenzi wako zungumza kwa sauti ya upendo na ukarimu.

7. Usimsahihishe mwenzi wako mbele ya watoto wako. Inaonyesha kutoheshimu.

8. Usimlinganishe mwenzi wako na wengine ukisema "Kwa nini usiwe kama wanawake/wanaume wengine?", "Kwa nini usiwe kama hivi na hivi?". Inamdhoofisha mwenzi wako na inaua kujiamini kwake.

9. Usikumbushie makosa ya zamani ya mwenzi wako, yaliyopita yamepita. Ukifanya hivyo utachanganya tu masuala

10. Msifu mwenzi wako kuliko unavyomkosoa.

11. Unapomrekebisha mwenzi wako, usiruhusu mwenzi wako kuwa na shaka na upendo wako. Unaweza kufanya hivyo kwa kusema "Unajua nakupenda. Mpenzi, niliona kwamba...."

12. Usiruhusu hisia zako zikushinde na kusema mambo yasiyo na maana.

13. Tarajia kubishiwa au mabishano kutoka kwa mwenzi wako au kukwepa uhalisia, watu wazima wengi hawachukulii kurekebishwa kama kitu kirahisi, kwa lugha nyingine hawapendi kurekebishwa au kuambiwa ukweli lakini ukiendelea kuwa mpole na kuwasilisha taarifa zako kwa staha, hatimaye mwenzi wako atakubali.

14. Ukishamsahihisha mwenzi wako, usimtie hatiani; hii itapunguza tu umoja wenu.

15. Thamini ukuaji wa mwenzi wako, pale anapopambana na kuonesha kubadilika katika nyanja mbalimbali za kitabia, kiuchumi na kimaisha basi thamini ukuaji wake.

16. Usichukulie maisha kwa uzito sana.

17. Kumbuka kwamba lengo la kumrekebisha mwenzi wako si kuthibitisha kuwa upo sahihi bali ni kumtia moyo mwenzi wako kuwa bora zaidi. Unapozingatia kuthibitisha kuwa uko sahihi, unaweza kushinda mabishano lakini ukapoteza ndoa yako au kufanya mambo kuwa magumu kati yenu wawili.
 
Yule mwanaume huwa anaongea na mimi kwa ustaarabu kama hivyo mpaka naona aibu sometimes!
Yani unakosea halafu unarekebishwa kwa upole na upendo, unakiri kosa na hakika huwezi kurudia.

Sio umekosea unakosolewa kama mko vitani, kejeli juu!
Huwezi kuliona kosa lako.
 
Mwenzi mwenye mapungufu piga chini
Kwa hiyo kwa Akili zako unahisi wewe hauna mapungufu, kwamba wewe ukoseagj, wewe ni mkamilifu... Angalia wewe ndio usije ukawa wa kupigwa chini 🤣

Hakuna mtu asiyekuwa na mapungufu Dunia hii, ukiona uambiwi mapungufu yako haimaanishi uwakwazi Watu, bali wengine wanaogopa kukuambia tu
 
Kuna kenge hata ukiwaeleza kustaarabu na faragha hawaelewi na wanakuja juu, sijui shida Nini? Au tutie gunia la mkaa?
 
kuna wengine unawaelekeza jambo mara elfu lakini ni vichwa maji, mpaka unajiuliza huyu mwalimu wake aliishi naye vipi?

unatumia kila aina ya pitch zote zinafeli. aisee mapenzi ni matamu ila sometime very boring.
 
Kwa hiyo kwa Akili zako unahisi wewe hauna mapungufu, kwamba wewe ukoseagj, wewe ni mkamilifu... Angalia wewe ndio usije ukawa wa kupigwa chini 🤣

Hakuna mtu asiyekuwa na mapungufu Dunia hii, ukiona uambiwi mapungufu yako haimaanishi uwakwazi Watu, bali wengine wanaogopa kukuambia tu
Akiona pungufu anipige chini
 
1. Usimsahihishe mwenzi wako hadharani mbele ya umma au kundi la watu, Inamfanya aone aibu.

2. Usimfokee au kumkaripia mwenzi wako unaporekebisha.

3. Usitumie maneno kama "Hautawai...", au "Wewe kila mara...". Kufanya hivyo ni kuchochea visa. Tumia maneno kama "Sidhani kama ilikuwa sawa ulichofanya jana"

4. Usimsahihishe mwenzi wako kana kwamba ni mtoto ukisema "Tafadhali tenda sambamba na umri wako", "Wewe ni mtu mzima bwana", "Kua", "Wewe ni mtoto sana", "Una kuwa kama mtoto", "Una utoto mwingi" na kauli za namna hiyo. Hii haionyeshi heshima

5. Usimsahihishe mwenzi wako kuhusu jambo zito wakati nyinyi wawili hamna muda wa kutosha wa kulizungumzia. Fanya hivyo katika hali ya utulivu.

6. Unapomsahihisha mwenzi wako zungumza kwa sauti ya upendo na ukarimu.

7. Usimsahihishe mwenzi wako mbele ya watoto wako. Inaonyesha kutoheshimu.

8. Usimlinganishe mwenzi wako na wengine ukisema "Kwa nini usiwe kama wanawake/wanaume wengine?", "Kwa nini usiwe kama hivi na hivi?". Inamdhoofisha mwenzi wako na inaua kujiamini kwake.

9. Usikumbushie makosa ya zamani ya mwenzi wako, yaliyopita yamepita. Ukifanya hivyo utachanganya tu masuala

10. Msifu mwenzi wako kuliko unavyomkosoa.

11. Unapomrekebisha mwenzi wako, usiruhusu mwenzi wako kuwa na shaka na upendo wako. Unaweza kufanya hivyo kwa kusema "Unajua nakupenda. Mpenzi, niliona kwamba...."

12. Usiruhusu hisia zako zikushinde na kusema mambo yasiyo na maana.

13. Tarajia kubishiwa au mabishano kutoka kwa mwenzi wako au kukwepa uhalisia, watu wazima wengi hawachukulii kurekebishwa kama kitu kirahisi, kwa lugha nyingine hawapendi kurekebishwa au kuambiwa ukweli lakini ukiendelea kuwa mpole na kuwasilisha taarifa zako kwa staha, hatimaye mwenzi wako atakubali.

14. Ukishamsahihisha mwenzi wako, usimtie hatiani; hii itapunguza tu umoja wenu.

15. Thamini ukuaji wa mwenzi wako, pale anapopambana na kuonesha kubadilika katika nyanja mbalimbali za kitabia, kiuchumi na kimaisha basi thamini ukuaji wake.

16. Usichukulie maisha kwa uzito sana.

17. Kumbuka kwamba lengo la kumrekebisha mwenzi wako si kuthibitisha kuwa upo sahihi bali ni kumtia moyo mwenzi wako kuwa bora zaidi. Unapozingatia kuthibitisha kuwa uko sahihi, unaweza kushinda mabishano lakini ukapoteza ndoa yako au kufanya mambo kuwa magumu kati yenu wawili.
Yes sure,
Mathalani kama hajaswaki vizuri mdomo unatema,
mueleze tu kiungwana na upendo, fulani, leo naona mdomo wako umechangamka umekula nini aise pekeyako au umekula vitunguu hebu njoo bafuni nikuswaki kwanza....

hata kama huko chini kuna smell the difference mueleze na ummbebe ukamuoshe kikamilifu
 
Wengine ukimwambia hata kwa lugha rafiki bado atakutafutia kisiriani tu ili na yeye akuongelee maneno ya kukukomoa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom