Jinsi ya kuishi bila kukopa kopa pesa

Jinsi ya kuishi bila kukopa kopa pesa

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Panga bajeti ya mapato na matumizi.
– Bajeti inakusaidia kujua unachopata na kutumia bila kupitiliza.

Tumia pesa kwa vipaumbele, si kwa mazoea au tamaa.
– Tofautisha kati ya mahitaji ya lazima na anasa au starehe.

Epuka maisha ya kushindana na watu wengine.
– Kuiga maisha ya wengine hupelekea matumizi ya kupita uwezo wako. Ukiona jirani yako amenunua Rolls-Royce Spectre, usikope pesa ili ununue Bugatti Tourbillon.

Jifunze kusema “hapana” kwa matumizi yasiyo ya lazima.
– Nidhamu ya kusema hapana ni silaha muhimu dhidi ya madeni.

Tenga akiba kila mwezi, hata kama ni kidogo.
– Akiba ni kinga dhidi ya dharura zinazoweza kukulazimisha kukopa.

Ridhika na kile Mungu alichokupa kwa sasa.
– Kuridhika huzalisha amani ya moyo na huzuia tamaa ya kupita kiasi.

Fanya kazi kwa bidii na ubunifu. Usiridhike na chanzo kimoja cha pesa. Panua wigo.
– Mapato yako yataongezeka ukiongeza bidii ya kazi na vyanzo vingine vya mapato halali.

Usitumie mikopo kuendeshea maisha ya kila siku.
– Mikopo inafaa zaidi kwa ajili ya uwekezaji. Usikope kwa ajili ya kununua chakula au mavazi.

Epuka mikopo ya haraka, yenye riba kubwa.
– Mikopo hiyo inaumiza zaidi kuliko kusaidia; inawaingiza watu wengi kwenye mateso.

Mshirikishe Mungu katika mipango yako ya kifedha.
– Mungu huwapa hekima wale wanaomtumaini, hata katika masuala ya pesa.
 
Kukopa sio jambo la kujivunia. Maandiko yanatuambia: akopaye pesa ni mtumwa wa akopeshaye: “Tajiri humtawala maskini, naye akopaye ni mtumwa wa akopeshaye.” (Mithali 22:7)

Kauli hii inagusa hali ya kiroho, kisaikolojia, na kijamii anayopitia mtu anayekopa. Kukopa pesa sio dhambi, lakini ni jambo linalomfanya mtu awe tegemezi kama mtumwa.

Mtu anayekopa hujikuta kwenye hali zifuatazo za utumwa:
Utumwa wa Kiakili: Fikira zake nyingi hujikita kwenye deni. Anakosa amani ya moyo, usingizi wake huvurugika kwa sababu ya mawazo ya kulipa deni.

Utumwa wa Maamuzi: Anakosa uhuru wa kufanya maamuzi ya kifedha, kwa sababu mapato yake mengi huenda moja kwa moja kwa mkopeshaji.

Utumwa wa aibu: Mara nyingi anakosa ujasiri mbele ya watu au kujisikia aibu kuonana na mkopeshaji. Mkopo unaweza kuharibu sifa na mahusiano.

Utumwa wa Kiroho: Imani na tegemeo la akopaye linaweza kuhamia kwa binadamu badala ya kumtumaini Mungu. Kwa sababu hiyo anaweza hata kujihusisha na mikataba isiyo ya ki-Mungu.

Waswahili wnasema "kukopa arusi, kulipa matanga(msiba).

Hapo ndipo penye mtego. Kwa sababu ya kukopa kopa, kuna watu wana madeni makubwa kiasi kwamba wanaamua kutokulipa kabisa madeni. Hii mbele za Mungu ni dhambi. Unahesabika miongoni mwa wasiofanya haki (Zaburi 37:21). Mtu mwaminifu lazima arudishe kile alichoazima. Mtu anayekopa kwa nia ya kutolipa, au anakataa kulipa kwa ulegevu au ujanja, ni mkosaji mbele za Mungu. Ni sawa na mwizi.

Katika Warumi 13:8 tunakumbushwa kwamba tusidaiwe chochote isipokuwa kupendana.

Deni la pekee tunalopaswa kuwa nalo ni upendo, sio fedha za watu wengine. Kukopa bila kulipa ni kinyume cha agizo hilo.

Tukiishi kwa kumtumaini Mungu, tunaweza kuwa mbali na kukopa kopa. Badala yake tunaweza kuwa watu wa kuwakopesha wengine. Katika Kumbukumbu la Torati 28:1-12, Mungu amesema tukiisikia sauti yake na kufanya maagizo yake, atabariki kazi za mikono yetu, kiasi kwamba tutakuwa watu wa kukopesha mataifa mengi na sisi hatutakopa.

Hii ni ahadi ya Mungu kwa watu wake wanaoishi kwa uaminifu na kutii maagizo yake. Ni ahadi ya kuinuliwa kutoka hali ya utegemezi hadi hali ya kuwa msaada kwa wengine.

Mungu hataki watoto wake waishi katika utumwa wa madeni. Anapenda tuwe huru kiuchumi ili tuweze kuwasaidia wengine, na kuonyesha utukufu wake kwa dunia. Ukimwamini Mungu, ukafanya kazi kwa bidii, na ukaishi kwa nidhamu ya fedha, Mungu atakuinua kwa viwango vya kuwakopesha na kuwasaidia wengine. Barikiwa.
 
Huyu bado anahali ngumu ya maisha kiasi kwamba hajajua bado faida za mkopo.

Yaani bado hujaijua ladha ya kuwa na pesa ila unazituliza tu kwenye Compound Interest halafu unatumia pesa za mwingine kupigia pesa.
 
Japo hili andiko lako ni C&P lakini angalau leo umeongelea mada ambayo ina manufaa kwa Taifa na Wananchi wake
 
Umesema ukweli unaotokana na uhalisia wa maisha ya wengi wetu — pesa haitoshi hata kama tukipanga bajeti. Lakini je, hiyo haitoshi iwe sababu ya kuhalalisha maisha ya mikopo isiyokuwa na mwisho?

Kukopa si dhambi, ila ni dawa yenye madhara ikiwa haitatumika kwa nidhamu. Ukijikopesha kila wakati kwa sababu tu "hela haitoshi", unajiweka kwenye mtego wa utegemezi wa kudumu. Hilo halibadilishi hali, bali linaiimarisha kwa kifungo kisichoonekana.

Bajeti, nidhamu, na ridhiko havifanyi pesa iongezeke ghafla, lakini ni misingi inayokuweka kwenye nafasi ya kukua — hata kwa hatua ndogo ndogo.

Ni kweli kwamba hali ni ngumu. Lakini pia ni kweli kwamba kuna watu waliotoka kwenye hali kama hiyo hiyo kwa kuamua kuishi chini ya uwezo wao, kufanya kazi ya ziada, na kuvumilia kwa muda. Ukianza leo kujifunza kuacha mikopo midogo midogo, kesho hutaogopa mikopo mikubwa ya uwekezaji.

Sio wote tutaweza kuishi bila kukopa — lakini tusikubali mikopo iwe mtindo wa maisha.

Kama tunakopa, tuhakikishe ni kwa kusudi sahihi — si kwa starehe, si kwa kushindana, na si kwa kujificha nyuma ya ugumu wa maisha.

Baraka huja kwa bidii, nidhamu, na maamuzi sahihi, hata kama ni magumu.
 
Japo hili andiko lako ni C&P lakini angalau leo umeongelea mada ambayo ina manufaa kwa Taifa na Wananchi wake
We hujui tu, mada za kiroho zina manufaa sana kwa jamii yote. Mada zenye mafundisho ya Neno la Mungu zinabadili roho za watu. Watu wakiokoka kwelikweli wanaacha wizi, ujambazi, chuki, mauaji. Wakiokoka wanakuwa waaminifu kazini, hawadanganyi katika biashara, hawatoi ahadi za uongo, hawadhulumu watu...
Bado tu hujaona faida za mada za kiroho?
 
Kwahiyo ukimwangalia mwamposa haliishi Hilo bundle??
Ukilitumia bando lako kumsikiliza mhubiri wa kweli, utapata ufunuo zaidi wa jinsi ya kufanikiwa hata kiuchumi. Lakini kama bando lako unalitumia kuwasikiliza manabii wa mchongo, watakuibia hata kidogo ulicho nacho. Ndio sababu tunakazana kuandika mada za kiroho ili kuwatahadharisha watu kuwa nyakati hizi ni za mwisho. Kuna manabii wengi wa uongo. Mada za namna hii ni faida kwa jamii kwa sababu wataepuka kupoteza pesa zao kununua chumvi na mafuta feki ya upako.
 
Nshakuomba uniombee hutaki
 
Umasikini ndiyo chanzo cha uovu wote. Ukikomboka kiuchumi hata nafsi huwa na utulivu na uhalifi kwenye jamii unapungua pakubwa.
Ndiyo maana tajiri hapandishi mashetani
We hujui tu, mada za kiroho zina manufaa sana kwa jamii yote. Mada zenye mafundisho ya Neno la Mungu zinabadili roho za watu. Watu wakiokoka kwelikweli wanaacha wizi, ujambazi, chuki, mauaji. Wakiokoka wanakuwa waaminifu kazini, hawadanganyi katika biashara, hawatoi ahadi za uongo, hawadhulumu watu...
Bado tu hujaona faida za mada za kiroho?
 
Huyu bado anahali ngumu ya maisha kiasi kwamba hajajua bado faida za mkopo.

Yaani bado hujaijua ladha ya kuwa na pesa ila unazituliza tu kwenye Compound Interest halafu unatumia pesa za mwingine kupigia pesa.
26 Life kwanza nikusahihishe, ningekuwa na hali ngumu ya maisha nisingeshinda hapa naandika mada za kuwasaidia wengine.

Hoja yako kuhusu kutumia pesa za wengine (leverage) huku zako binafsi zikiendelea kuzaa faida kwenye compound interest ni mbinu ya kifedha inayotambulika, na kwa mtu mwenye maarifa ya juu ya fedha, inaweza kuwa na manufaa.

Hata hivyo, changamoto ni hii: mbinu hiyo inahitaji nidhamu ya hali ya juu, uelewa wa hatari za kifedha, na uwezo wa kurejesha mkopo kwa wakati hata kama mambo hayaendi vizuri. Ni wachache sana wanaoweza kuitumia mbinu hiyo kwa mafanikio.

Wengi wanaokopa, katika nchi zinazoendelea, hawakopi kwa ajili ya uwekezaji, bali kwa matumizi ya kila siku kama chakula, kodi, mavazi, au sherehe. Kwa hiyo, hawazalishi chochote kutoka kwenye mkopo.

Katika mazingira kama hayo, hata kama mtu ana pesa zake benki zinazopata compound interest, bado hatakuwa na faida ya kweli kwa sababu anaingiza faida ndogo sana benki (labda 10% kwa mwaka), lakini anatumia mkopo wa riba kubwa (labda 15% au zaidi), halafu fedha hiyo inakwenda kwenye matumizi yasiyo na marejesho.

Matokeo yake ni kwamba faida ndogo inayopatikana kwenye compound interest inafutwa kabisa na mzigo wa mkopo wa matumizi. Mwisho wa siku, mtu huyo atazama kwenye madeni ingawa anaonekana ana akili ya kifedha.

Kwa hiyo, siwashauri watu wa kawaida waanze na mkakati wa “leverage” kabla hawajajenga msingi wa nidhamu ya matumizi, akiba, na uelewa wa mikopo yenye tija. Ni bora kuwa huru kifedha kuliko kuishi kwa kutegemea mikopo kila siku.

Hekima ya Mithali 22:7 bado inabaki kuwa ya kweli: "Akopaye ni mtumwa wa akopeshaye."

Na bado sote tunahitaji Mungu atutimizie ahadi yake kwamba tukifuata kanuni zake, atatufikisha kwenye level ambayo: “Tutawakopesha mataifa, wala hatutakopa.” (Kumb. 28:12)

cc: DeepPond Soulja boy Mvinyo mpya
 
Panga bajeti ya mapato na matumizi.
– Bajeti inakusaidia kujua unachopata na kutumia bila kupitiliza.

Tumia pesa kwa vipaumbele, si kwa mazoea au tamaa.
– Tofautisha kati ya mahitaji ya lazima na anasa au starehe.

Epuka maisha ya kushindana na watu wengine.
– Kuiga maisha ya wengine hupelekea matumizi ya kupita uwezo wako. Ukiona jirani yako amenunua Rolls-Royce Spectre, usikope pesa ili ununue Bugatti Tourbillon.

Jifunze kusema “hapana” kwa matumizi yasiyo ya lazima.
– Nidhamu ya kusema hapana ni silaha muhimu dhidi ya madeni.

Tenga akiba kila mwezi, hata kama ni kidogo.
– Akiba ni kinga dhidi ya dharura zinazoweza kukulazimisha kukopa.

Ridhika na kile Mungu alichokupa kwa sasa.
– Kuridhika huzalisha amani ya moyo na huzuia tamaa ya kupita kiasi.

Fanya kazi kwa bidii na ubunifu. Usiridhike na chanzo kimoja cha pesa. Panua wigo.
– Mapato yako yataongezeka ukiongeza bidii ya kazi na vyanzo vingine vya mapato halali.

Usitumie mikopo kuendeshea maisha ya kila siku.
– Mikopo inafaa zaidi kwa ajili ya uwekezaji. Usikope kwa ajili ya kununua chakula au mavazi.

Epuka mikopo ya haraka, yenye riba kubwa.
– Mikopo hiyo inaumiza zaidi kuliko kusaidia; inawaingiza watu wengi kwenye mateso.

Mshirikishe Mungu katika mipango yako ya kifedha.
– Mungu huwapa hekima wale wanaomtumaini, hata katika masuala ya pesa.
Great
 
26 Life kwanza nikusahihishe, ningekuwa na hali ngumu ya maisha nisingeshinda hapa naandika mada za kuwasaidia wengine.

Hoja yako kuhusu kutumia pesa za wengine (leverage) huku zako binafsi zikiendelea kuzaa faida kwenye compound interest ni mbinu ya kifedha inayotambulika, na kwa mtu mwenye maarifa ya juu ya fedha, inaweza kuwa na manufaa.

Hata hivyo, changamoto ni hii: mbinu hiyo inahitaji nidhamu ya hali ya juu, uelewa wa hatari za kifedha, na uwezo wa kurejesha mkopo kwa wakati hata kama mambo hayaendi vizuri. Ni wachache sana wanaoweza kuitumia mbinu hiyo kwa mafanikio.

Wengi wanaokopa, katika nchi zinazoendelea, hawakopi kwa ajili ya uwekezaji, bali kwa matumizi ya kila siku kama chakula, kodi, mavazi, au sherehe. Kwa hiyo, hawazalishi chochote kutoka kwenye mkopo.

Katika mazingira kama hayo, hata kama mtu ana pesa zake benki zinazopata compound interest, bado hatakuwa na faida ya kweli kwa sababu anaingiza faida ndogo sana benki (labda 10% kwa mwaka), lakini anatumia mkopo wa riba kubwa (labda 15% au zaidi), halafu fedha hiyo inakwenda kwenye matumizi yasiyo na marejesho.

Matokeo yake ni kwamba faida ndogo inayopatikana kwenye compound interest inafutwa kabisa na mzigo wa mkopo wa matumizi. Mwisho wa siku, mtu huyo atazama kwenye madeni ingawa anaonekana ana akili ya kifedha.

Kwa hiyo, siwashauri watu wa kawaida waanze na mkakati wa “leverage” kabla hawajajenga msingi wa nidhamu ya matumizi, akiba, na uelewa wa mikopo yenye tija. Ni bora kuwa huru kifedha kuliko kuishi kwa kutegemea mikopo kila siku.

Hekima ya Mithali 22:7 bado inabaki kuwa ya kweli: "Akopaye ni mtumwa wa akopeshaye."

Na bado sote tunahitaji Mungu atutimizie ahadi yake kwamba tukifuata kanuni zake, atatufikisha kwenye level ambayo: “Tutawakopesha mataifa, wala hatutakopa.” (Kumb. 28:12)

cc: DeepPond Soulja boy Mvinyo mpya
Safi sana. Umeandika point muhimu. Kimsingi sio mpango wa Mungu watu wake waishi kwa mikopo...
 
Back
Top Bottom