Jinsi ya kuishi bila kukopa kopa pesa

Jinsi ya kuishi bila kukopa kopa pesa

Kwa mara ya kwanza umeandika jambo la muhimu sana kwa weledi mkubwa. Ninaunga mkono yote uliyoandika. Watu wakope mikopo kuboresha biashara na sio mambo mengine yasiyozalisha. Hata kwenye biashara kukopa ni kwa tahadhari sana..... kwa mkristo kama unaweza kufanya mambo yako bila kukopa ni bora zaidi.
 
26 Life kwanza nikusahihishe, ningekuwa na hali ngumu ya maisha nisingeshinda hapa naandika mada za kuwasaidia wengine.

Hoja yako kuhusu kutumia pesa za wengine (leverage) huku zako binafsi zikiendelea kuzaa faida kwenye compound interest ni mbinu ya kifedha inayotambulika, na kwa mtu mwenye maarifa ya juu ya fedha, inaweza kuwa na manufaa.

Hata hivyo, changamoto ni hii: mbinu hiyo inahitaji nidhamu ya hali ya juu, uelewa wa hatari za kifedha, na uwezo wa kurejesha mkopo kwa wakati hata kama mambo hayaendi vizuri. Ni wachache sana wanaoweza kuitumia mbinu hiyo kwa mafanikio.

Wengi wanaokopa, katika nchi zinazoendelea, hawakopi kwa ajili ya uwekezaji, bali kwa matumizi ya kila siku kama chakula, kodi, mavazi, au sherehe. Kwa hiyo, hawazalishi chochote kutoka kwenye mkopo.

Katika mazingira kama hayo, hata kama mtu ana pesa zake benki zinazopata compound interest, bado hatakuwa na faida ya kweli kwa sababu anaingiza faida ndogo sana benki (labda 10% kwa mwaka), lakini anatumia mkopo wa riba kubwa (labda 15% au zaidi), halafu fedha hiyo inakwenda kwenye matumizi yasiyo na marejesho.

Matokeo yake ni kwamba faida ndogo inayopatikana kwenye compound interest inafutwa kabisa na mzigo wa mkopo wa matumizi. Mwisho wa siku, mtu huyo atazama kwenye madeni ingawa anaonekana ana akili ya kifedha.

Kwa hiyo, siwashauri watu wa kawaida waanze na mkakati wa “leverage” kabla hawajajenga msingi wa nidhamu ya matumizi, akiba, na uelewa wa mikopo yenye tija. Ni bora kuwa huru kifedha kuliko kuishi kwa kutegemea mikopo kila siku.

Hekima ya Mithali 22:7 bado inabaki kuwa ya kweli: "Akopaye ni mtumwa wa akopeshaye."

Na bado sote tunahitaji Mungu atutimizie ahadi yake kwamba tukifuata kanuni zake, atatufikisha kwenye level ambayo: “Tutawakopesha mataifa, wala hatutakopa.” (Kumb. 28:12)

cc: DeepPond Soulja boy Mvinyo mpya
Maelezo meengi yaani nimesoma mpaka baadaye nimeanza kuona kama sauti ya Nanauka ikiimba....

Pointi itabakia palepale kama unaona mikopo ni ujinga ni kwasababu huna Financial Intelligence.
Labda kama unawashauri wajinga ambao huwa wanakopa kwaajili ya Starehe na Matumizi.
Kwasisi wawekezaji hatuwezi kuichukua hiyo advice.
 
Umetoa elimu nzuri Sana dada, japo Huwa nakupiga Spana, Ila hapa nakuona kongole😊👍
26 Life kwanza nikusahihishe, ningekuwa na hali ngumu ya maisha nisingeshinda hapa naandika mada za kuwasaidia wengine.

Hoja yako kuhusu kutumia pesa za wengine (leverage) huku zako binafsi zikiendelea kuzaa faida kwenye compound interest ni mbinu ya kifedha inayotambulika, na kwa mtu mwenye maarifa ya juu ya fedha, inaweza kuwa na manufaa.

Hata hivyo, changamoto ni hii: mbinu hiyo inahitaji nidhamu ya hali ya juu, uelewa wa hatari za kifedha, na uwezo wa kurejesha mkopo kwa wakati hata kama mambo hayaendi vizuri. Ni wachache sana wanaoweza kuitumia mbinu hiyo kwa mafanikio.

Wengi wanaokopa, katika nchi zinazoendelea, hawakopi kwa ajili ya uwekezaji, bali kwa matumizi ya kila siku kama chakula, kodi, mavazi, au sherehe. Kwa hiyo, hawazalishi chochote kutoka kwenye mkopo.

Katika mazingira kama hayo, hata kama mtu ana pesa zake benki zinazopata compound interest, bado hatakuwa na faida ya kweli kwa sababu anaingiza faida ndogo sana benki (labda 10% kwa mwaka), lakini anatumia mkopo wa riba kubwa (labda 15% au zaidi), halafu fedha hiyo inakwenda kwenye matumizi yasiyo na marejesho.

Matokeo yake ni kwamba faida ndogo inayopatikana kwenye compound interest inafutwa kabisa na mzigo wa mkopo wa matumizi. Mwisho wa siku, mtu huyo atazama kwenye madeni ingawa anaonekana ana akili ya kifedha.

Kwa hiyo, siwashauri watu wa kawaida waanze na mkakati wa “leverage” kabla hawajajenga msingi wa nidhamu ya matumizi, akiba, na uelewa wa mikopo yenye tija. Ni bora kuwa huru kifedha kuliko kuishi kwa kutegemea mikopo kila siku.

Hekima ya Mithali 22:7 bado inabaki kuwa ya kweli: "Akopaye ni mtumwa wa akopeshaye."

Na bado sote tunahitaji Mungu atutimizie ahadi yake kwamba tukifuata kanuni zake, atatufikisha kwenye level ambayo: “Tutawakopesha mataifa, wala hatutakopa.” (Kumb. 28:12)

cc: DeepPond Soulja boy Mvinyo mpya
 
Naomba nitoe ushuhuda kidgo,

Nina mikopo ya biashara Kama benki 4 hivi, tangu 2010 mpaka Sasa naendelea nayo. Nailipa vizuri TU.

Mwendo wangu ni Huwa nakopa miez 6 maximum mwaka 1 TU, mwaka Jana tu ndo nmechukua mkopo mmoja TU WA miaka 2.

Ila principle zangu Huwa ni mbili TU,

1. Huwa sikopi kuanzisha mradi mpya,ukiona nmekopea mradi mpya, uwa sikopi zaidi ya 25% ya mtaji nilionao.
Mrejesho Huwa halisubiri uanze KUTAFTA wateja.

2. Pesa ya mkopo inaendakwenye malengo ya mkopo Moja Kwa Moja bila kupunguza Hata mia mbovu.

Ukinikuta nna pesa ya mkopo, aisee Hata itokee emergency ya namna gani, ntakuacha ujifie zako tu, Ila sio kupunguza Hata senti moja ya mkopo niliochukua.
 
Taifa linakopa, bilionea wanakopa, mimi ni nani hata nisikope?
 
Panga bajeti ya mapato na matumizi.
– Bajeti inakusaidia kujua unachopata na kutumia bila kupitiliza.

Tumia pesa kwa vipaumbele, si kwa mazoea au tamaa.
– Tofautisha kati ya mahitaji ya lazima na anasa au starehe.

Epuka maisha ya kushindana na watu wengine.
– Kuiga maisha ya wengine hupelekea matumizi ya kupita uwezo wako. Ukiona jirani yako amenunua Rolls-Royce Spectre, usikope pesa ili ununue Bugatti Tourbillon.

Jifunze kusema “hapana” kwa matumizi yasiyo ya lazima.
– Nidhamu ya kusema hapana ni silaha muhimu dhidi ya madeni.

Tenga akiba kila mwezi, hata kama ni kidogo.
– Akiba ni kinga dhidi ya dharura zinazoweza kukulazimisha kukopa.

Ridhika na kile Mungu alichokupa kwa sasa.
– Kuridhika huzalisha amani ya moyo na huzuia tamaa ya kupita kiasi.

Fanya kazi kwa bidii na ubunifu. Usiridhike na chanzo kimoja cha pesa. Panua wigo.
– Mapato yako yataongezeka ukiongeza bidii ya kazi na vyanzo vingine vya mapato halali.

Usitumie mikopo kuendeshea maisha ya kila siku.
– Mikopo inafaa zaidi kwa ajili ya uwekezaji. Usikope kwa ajili ya kununua chakula au mavazi.

Epuka mikopo ya haraka, yenye riba kubwa.
– Mikopo hiyo inaumiza zaidi kuliko kusaidia; inawaingiza watu wengi kwenye mateso.

Mshirikishe Mungu katika mipango yako ya kifedha.
– Mungu huwapa hekima wale wanaomtumaini, hata katika masuala ya pesa.
Nilikaa mwaka mzima bila kununua nguo zilizopo zimechakaa sana. Je niigata pesa sinunue kwa kuwa nguo ni anasa?
 
Umetoa elimu nzuri Sana dada, japo Huwa nakupiga Spana, Ila hapa nakuona kongole😊👍
Asante kwa kongole. Nakuombea, Mungu akufunulie, utambue kuwa hata zile mada zangu unazozitwanga spana zina elimu nzuri ya kukusaidia kupata faida ya milele kuliko hizo compound interests
 
Taifa linakopa, bilionea wanakopa, mimi ni nani hata nisikope?
Mabilionea na mataifa makubwa hukopa kwa madhumuni ya kuwekeza au kukuza biashara zao. Na wanapokopa wanahakikisha kwamba mikopo hiyo inaleta faida na si mzigo.

Wengi wetu tunakopa kwa matumizi ya kawaida au anasa bila mpango wa marejesho, na hapo ndipo tunapoingia kwenye hatari ya kuishi kama watumwa wa mikopo sawasawa na andiko hilo "akopaye ni mtumwa wa akopeshaye" (Methali 22:7).

Mimi hapa nahamasisha kuishi bila kutegemea mikopo. Sijasema kwamba usikope kabisa. Ni bora kujifunza namna ya kutumia fedha kwa busara, na kuendelea kujenga uhuru wa kifedha kwa kuzingatia hekima ya Biblia.
 
Matumizi ya kawaida ni yapi?
Mzazi wako mgonjwa anatakiwa pesa ya matibabu baada ya vipimo vikubwa na huna pesa unafanyaje?
Familia inakuwa kwa ongezeko la watoto, je usikope ujenge kanyumba na maisha mengine yaendelee?
 
wanakopa hadi siisiiemu na ufisadi wao wote wee ni nani hata usikope, unaandika usivyovijua yani wana kila kitu lakini bado wanakopa ili wakope tena.
 
Soma tena vizuri mada. Sijasema kukopa ni dhambi
 
whatever the case huwezi kuishi bila kukopa hasa kwa nchi zetu masikini hizo , anakopa hadi trump hizo namna ulizosema ni ma theory tu hamna kitu.
 
Kumbe Kiswahili kigumu?! Mada yangu ina-discourage kukopa kopa, sio kukopa
 
Back
Top Bottom