Jinsi ya Kufadhili Wageni nyumbani kwako

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,338
51,859
JINSI YA KUFADHILI WAGENI WANAOKUJA NYUMBANI KWAKO.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Kwenye familia ni jambo la kawaida kutembelewa na wageni. Wageni huja kwa sababu mbalibali kma vile kusalimia, kuja kukupongeza kwa jambo fulani, kuja kukupa faraja au kukusaidia upatwapo na madhila ya dunia; Wapo wageni ambao huja ili uwape msaada au faraja, wengine uwape hifadhi kwa muda, wengine huja kama sehemu ya kudumisha undugu na urafiki.
Mgeni huweza kuwa Wazazi wako, Wakwe zako, ndugu zako, watoto wa ndugu zako, mashemeji, marafiki, jamaa n.k

Wazazi wengi hasa wa Kiafrika huwa na dhana potofu kuwa wanapoenda kutembelea familia za watoto wao hudhani kuwa wao ni sehemu ya familia ya watoto wao jambo ambalo sio kweli. Wazazi lazima tuelewe kuwa unapoenda kwa mtoto wako nyumbani kwake; jua kabisa wewe ni mgeni kwenye ile familia. Hata kama ni mzazi wa mume/mke wa hiyo familia haimaanishi kuwa wewe ni sehemu ya hiyo familia, isipokuwa wewe ni mgeni muhimu kwenye familia hiyo. Hivyo huna maamuzi yoyote yale katika familia ya mtoto wako isipokuwa ushauri tuu.

Kutembelewa na wageni ni jambo jema sana, kiimani inaaminika kuwa nyumba itembelewayo na wageni ndio yenye baraka. Lakini hii sio kweli, sio kila mgeni anayekuja au atakayekuja kwenye familia yako ni baraka, wageni wengine ni chanzo cha laana, mikosi na mmajanga; na ndio maana nimeona umuhimu wa kuandika andiko hili.

Usikaribishe wageni ikiwa nyumba yako haina utaratibu, kanuni au katika ya familia.
Familia isiyo na utaratibu, kanuni na katiba inayoongoza wanafamilia haifai kutembelewa na wageni kwani mgeni yoyote iwe mwema au mgeni muovu akija salimia kwenye familia hiyo lazima majanga yatokee.

Huwa nawaambiaga wanangu katika maandiko yangu kuwa; usitembelee familia yoyote ambayo haina utaratibu, kanuni au katiba. Hata kama ni ndugu yako wa damu, au rafiki yako, kamwe usimtembelee nyumbani kwake ikiwa umeshajua kuwa familia yake inaishi bila utaratibu, wala miongozo.

Ni kawaida kwa wageni wasio na utaratibu au sheria katika familia zao kukataa kuja kukutembelea kwenye familia yako ikiwa wewe unasheria na kanuni kwenye familia yako.

Usikubali kutembelewa na wageni wasiotaka kufuata sheria za nyumbani kwako, mgeni ajapo hapaswi kuleta mabadiliko yoyote ndani ya familia yako, yawe mabadiliko chanya au mabadiliko hasi. Ikiwa umeona jambo zuri kwa mgeni na ukataka kuliiga basi, usiwe mwepesi kuiga mambo ya wageni hata kama ni mazuri bila kuyafanyia tathmini kwa muda usiopungua miezi mitatu.

Wageni wengi wamevunja ndoa za watu, wageni wengi wamefanya uharibifu wa mai, wageni wengi wametumika kuingiza mikosi, uchawi, kuleta magonjwa ndani ya familia, kubadili tabia za mke au mume, kubadili tabia za watoto.

Kikawaida kwenye wageni kumi wanaokutembelea basi mgeni mmoja ndio huwa na manufaa kwenye familia, lakini tisa waliobaki hawana manufaa. Nane wanaweza kuhitaji msaada wako, na mmoja akawa adui yako au akatumiwa na maadui zako.

Hatuwezi kukataa wageni, wageni ni muhimu lakini umuhimu wao hauzidi umuhimu wa familia zetu, na umuhimu wa familia zetu unalindwa na sheria na taratibu tulizoziweka zinazoongoza familia zetu. Mgeni akaribishwe kwa wema na ukarimu mkuu lakini ukaribisho uambatane na utoaji wa sheria za familia.

AINA ZA WAGENI
Kuna aina tatu za wageni

1. Wageni Ndugu
2. Wageni wasio Ndugu
3. Wageni wasioonekana

WAGENI NDUGU
Wageni ndugu ni wale ambao wana uhusiano na wewe wa moja kwa moja wa damu. Kama vile Mama, Baba, Kaka, Dada, Mjomba, shangazi n.k
Wageni hawa kwa sehemu kubwa wana michango ya hapa na pale kwenye maisha yako, hivyo wajapo ndani ya familia yako huwa na nguvu(inaweza kuwa kubwa au ndogo kulingana na utakavyowaruhusu) nguvu hii hutokana na michango yao pindi ulipokuwa mdogo, au ulipokuwa huna kitu. Kutokana na michango yao kwako wageni hawa mara nyingi baadhi yao huweza kujifanya wanamaamuzi ndani ya nyuma yako kwa kisingizio cha michango waliyoitoa kwako. Michango inaanzia kwenye kukuzaa, kukulea, kukusomesha, na kukupa huduma zozote zile. Wageni hawa ni baraka kwa sehemu kubwa ikiwa watakuwa ni watu wenye akili na wachaji wa Mungu, lakini wageni hawa hugeuka mashetani wabaya kama hawana akili na hawamchi Mungu. Ni kawaida kulogwa, kurudishwa nyuma kimaendeleo, au ndoa yako kuvunjwa na kundi hili la wageni kwani hawa ni ndugu zako. Ndoa nyingi huvunjwa na kundi hili.

Uzuri wa kundi hili ni kuwa hawa ni ndugu zako, iwe iwavyo kama mwanzo ndio walikuleta na kukukaribisha duniani basi ni lazima hata mwisho wako wakusindikize kaburini. Kundi hili heshima yake imekaa hapo kwani ufanye utakavyofanya kundi hili ndilo litawajibika na wewe dakika za lalasalama ukiwa hujiwezi. Pia kundi hili kwa sehemu kubwa ndilo linauchungu halisi na wewe hasa Mama yako mzazi kwani yeye ndiye aliyekuleta na ndiye anajiona anajukumu la kuhakikisha yupo nawe mpaka mwisho. Shida ya kundi hili au wageni hawa ni ile kujichukulia mamlaka dhidi yako, yaani ni rahisi kukuingilia au kukupoka kabisa uhuru wako wa maamuzi.

WAGENI WASIO NDUGU
Hawa ni wale wageni ambao huna uhusiano nao wa kidamu kama vile marafiki, jamaa, majirani, washikaji, mashoga, na hata wafanyakazi unaowaajiri au ulioajiriwa nao sehemu ya kazi. Kundi hili ni kundi lisilo na nguvu ya moja kwa moja kwani linajifahamu fika kuwa halina nguvu ya kiushawishi, linajijua ni kundi la mpito kwani mmekutana njiani au ofisi basi ipo siku mtaachana
Kundi hili pia linahusu mashemeji, mawifi na wakwe ambao umeowaolea/kuolewa kwao. Kundi hili nguvu yake ni ya wastani pale linapotaka kukushambuiia au hata kukusaidia.

WAGENI WASIOONEKANA
Hawa ni wageni ambao wanakuja ndani ya nyumba yako pasipokuonekana kwa macho, wageni hawa hawaji kwa miguu( Physically) huja kwa namna mbalimbali ikiwemo Uchawi na ulozi, roho wa Mungu, Virusi au Bakteria, na teknolojia. Wageni virusi na Bakteri huleta athari ya magonjwa yanayotibika kisayansi, lakini wageni wajao kichawi na kiulozi huja kwa namna nyingi ikiwemo kwa kutumia wanyama kama paka, panya, n..k, huja kwa kupitia ndoto au kuja moja kwa moja na kuishi nyumbani kwako pasipo wewe kujua, pia wageni wajao na roho wa Mungu huja kwa mfano huo huo wa wachawi na ulozi, huja kwa njia ya wanyama, ndoto au hata ishara zingine.

Wageni wanaotembelea nyumba zetu siku hizi zaidi ni wageni wa kiteknolojia kupitia vifaa vya mawasiliano kama vile simu, luninga, radio na laptop n.k. Kupitia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, instagram, Jamii Forum, WhatsApp n.k nyumba yako inaweza kutembelewa na wageni wasioonekana zaidi ya kumi kila siku. Utashangaa umekaa na mkeo kumbe anachat na mgeni wake kwa siri huko mitandaoni, au umekaa na mumeo kumbe anachat na mgeni wake kwa siri.

Leo wengi humu ni mashahidi kuwa wageni wasioonekana hasa wa mitandao wa kijamii wamekuwa mwiba sana ndani ya ndoa zetu. Wake zetu wamerubuniwa na wageni hawa wengine mpaka kuchepuka wameshachepuka na wageni wa mtandaoni, halikadhalika na wanaume

Wageni huweza kuwa kama wapelelezi
Wageni huweza kuwa kama watafuta msaada
Wageni huweza kuwa kama sehemu ya timu yako ya mapambano ya maisha.

Mara nyingi nasemaga kuwa, mke au mume habadiliki from nowhere, mke/mume hubadilishwa kulingana na mgeni aliyekutana naye. Mawazo ya mtu hutegemea zaidi watu na mazingira yanayomzuka.

Kikawaida, watu wote wenye akili huwazuia wenza wao kuchangamana na watu wasio na tija kwenye familia. Ni kawaida kwa mume mwenye akili kumzuia mke wake baadhi ya marafiki au kuingia baadhi ya mitandao ya kijamii. Mwanaume mwenye akili lazima aweke sheria za kuchangamana na kuingiliana kwa wanafamilia wake akiwemo mke na watoto kwa ustawi wa familia.

SIKU ZA KUKAA MGENI NYUMBANI KWAKO
Suala la mgeni kukaa nyumbani kwako ni suala muhimu la kuzingatiwa.
Mgeni lazima ifahamike atakaa kwako kwa muda gani akiwa anafanya nini.

Kadiri mgeni akaavyo kwako ndivyo athari zake zinaongezeka, zinaweza kuwa athari hasi au chanya.
Ukaaji wa mgeni nyumbani kwako utategemea zaidi ukaribu wako na yeye, lakini ukaribu wako na mgeni usizidi ukaribu wako na familia, namaanisha kama mgeni ataonekana anathari hasi zaidi kwenye familia ni bora aondoke bila kujali ukaribu wake kwako.

Mgeni kama ndugu ambaye amekuja kukusalimu asimalize siku saba nyumbani kwako.
Mgeni kama ndugu ambaye amekuja kwa sababu ya shida ya maradhi, akae mpaka atakapopona, akishapona muongezee siku saba kisha aondoke nyumbani kwako.
Mgeni kama Mzazi wako anaweza kuwa Mama/ Baba au wakwe zao, akae siku zisizozidi siku ishirini na nane nyumbani kwako
Mgeni kama mzazi wako/ mkwe wako kama amekuja kwa shida ya maradhi basi akae mpaka atakapopona na akipona muongezee siku zisizozidi ishirini na nane.
Mgeni kama ndugu yako labda ni mdogo au shemeji aamemkimbia/amefukuzwa na mumewe/mkewe usimpokee asilale hata siku moja katika nyumba yako, akifika tuu mpe chakula kisha mpigie mume/mke wake kuwa mkewe/mumewe yupo kwako na umemrudisha kwake. Usikae na mtu aliyekimbia nyumba yake, ataharibu nyumba yako. Akikubembeleza mwambie akiende kwa wazazi/wakwe zake. Zingatia usimpokee mtu aliyekimbia nyumba yake, akapokelewe na wazazi/wakwe huko.

Mgeni kama rafiki yako ambaye amekuja kukusalimu asimalize siku tatu ndani ya nyumba yako
Mgeni kama rafiki yako kama amekuja kwa kufukuzwa na mumewake au kakimbia nyumba yake, huyu usimpokee, mwambie aende kwingine, akusamehe tuu.

Mgeni aliyekuja kukuuguza/kumuuguza mkeo, akae mpaka siku u/atakapopona kisha muongezee siku saba za kukaa hapo kupumzika kisha akiondoka umpe na zawdi kidogo kama Ahsante.

Usipokee mgeni yeyote aliyekuja bila taarifa isipokuwa Mzazi/mkwe wako tena atoe sababu za msingi. Asiifanye nyumba yako kama yake, ajue kuwa hapo kuna utawala mwingine.
Usipokee mgeni yeyote aliyekuja katikati ya usiku na asubuhi yaani saa sita za usiku bila taarifa, au hata akitoa taarifa iwe ni kabla ya masaa kumi na mbili.

Usimruhusu Mgeni hasa usiyemjua kuombea chochote kwenye familia yako, iwe ni kuombea chakula, iwe ni kuomba wakati wa kusali, mgeni usimpe kuendesha ibada labda ila kuchangia anaruhusiwa. Wanaoruhusiwa kuomba kwenye familia yako sheria za familia ziainishe kabisa kuwa ni wewe Baba, Mkeo, na watoto, na ndugu zako mlio na imani sawa, na mashemeji zako mlio na imani sawa, na wakwe zao mlio na imani sawa, na wazazi wako mlio na imani sawa. Yeyote aliyetofauti na wewe kiimani asihusike kwa vyovyote kuendesha ibada za familia yako.

Ukiwa kama Baba wa familia ukisaidiwa na mke wako, mchungaji usiyemjua kamwe asiombe ndani ya nyumba yako. Mgeni atakayeomba ndani ya nyumba yako kama nilivyowataja hapo juu usimruhusu amshike moja ya watoto wako kichwa au sehemu yoyote ya mwili, bali mtamwambia kuwa yeye aombe alafu ninyi wazazi(wewe na mkeo) mtawashika watoto wenu kichwani kama ishara ya baraka au ishara ya jambo lolote mlilonuia

Mgeni asiruhusiwe kupika chakula hasa mgeni asiye wa karibu sana. Uwekwe utaratibu maalumu wa jinsi ya kuandaa chakula lakini mgeni asihusishwe kwa vyovyote vile. Wageni watakaoruhusiwa kupika wawe wazazi/wakwe, ndugu/ mashemeji. Hata hivyo usalama uzingatiwe, kila kitu kiwe chini ya uangalizi pasipo wageni kujua hivyo.

Mgeni awe huru ili iwe rahisi kumtambua kwa urahisi tabia zilizojificha, hakikisha unakuwa mcheshi na mchangamfu ili kufanya ajisikie huru na ajiachie kwako, jizuie na hasira na ukali usio na tija, fanya ukali mahali kwenye tija ikiwa ni sehemu ya kutoa funzo kwa wahusika ndani ya nyumba.

Kama mgeni atakuwa hafuati taratibu za nyumba yako ikiwemo taratibu za kazi, ibada, mavazi, chakula, lugha na mawasiliano, mikao na mitembeo, mapumziko na burudani basi utampa onyo si zaidi ya mara mbili, akikaidi basi utamfukuza nyumbani.

Ikiwa mgeni atahatarisha usalama wa famiia yako, ikiwa ni pamoja na mkeo au mumeo kumtaka kimapenzi, au mgeni kumtaka mkeo au mumeo kimapenzi hutakuwa na haja ya kutoa onyo bali utamfukuza moja kwa moja siku hiyo hiyo. Asilale humo.
Ikiwa moja ya wanafamilia ataungana na mgeni kufanya uovu huo fukuza wote, iwe ni mkeo na mgeni, au huyo mtoto na huyo mgeni fukuza wote jicho lako lisiwe na huruma. Lakini ikiwa wewe(mume) ndiye umeungana na mgeni yaani unatoka naye kimapenzi basi itakulazimu wewe ndiye uiache familia kwa sababu wewe ndiye muovu

Ikiwa mgeni atabainika anadalili za uchawi, ulozi na ushirikina, au utamfumania na hayo, basi hautampa onyo hata moja bali utamfukuza siku hiyo hiyo, asilale ndani ya nyumba yako usiku huo. Mpe hela ya Nyumba za wageni akalale huko kisha utampa na pesa ya nauli ya kurudi alipotoka.

Mgeni asilale na mtoto wako, labda awe mgeni kama Mzazi wako/ mkwe wako, lakini ikiwa mzazi/mkwe wako anasemwa kwa uchawi basi asilale na mwanao.

Mkeo hataruhusiwa kufua nguo za wageni wowote wa kwako wa kiume, iwe ni Baba yako, au wadogo zako wakiume waliofikisha umri uzidio miaka 15.
Mkeo hatafanya yale akufanyiayo wewe kwa mgeni yeyote kama sehemu ya kuwakarimu wageni kama vile kumuwekea mgeni maji ya kuoga bafuni

Mkeo atakuwa na haki ya kutoa mashauri ya kumfukuza mgeni kwako ikiwa ataona yafaa, nawe utaangalia sababu za yeye kufikia maamuzi hayo. Zingatia ulioa mwanamke unayempenda na uliyeamini anaakili ya kuwa mke wako, ikiwa ndivyo msikiize.

Mume akitaka kumfukuza mgeni yoyote ndani ya nyumba hatategemea ushauri wa mtu, atafanya hivyo pasipo kuingiliwa na yeyote yule. Ikiwa ataona yafaa kuomba ushauri kwa mke wake au watoto hiyo itakuwa hiyari yake na wala sio lazima. Ila mke yeye hatakuwa na mamlaka ya kumfukuza mgeni yeyote ndani ya familia pasipo kuomba kibali kwa mume wake. Na akichukua mamlaka ya kumfukuza pasipo kuomba kibali kwa mumewe basi itahesabika ni ukosefu wa adabu kwa mumewe,.

Mke hataruhusiwa kuleta mgeni yeyote nyumbani pasipo kuomba ruhusa kwa mume wake. Akishapewa ruhusa ndipo huyo mgeni ataruhusiwa kuja nyumbanii. Taarifa ya kuja kwa mgeni sharti iwe ndani ya masaa arobaini na nane. Mume anayomamlaka ya kukataa mgeni yeyote atakayepewa taarifa na mke wake au atakayeletwa na mke wake pasipo kuingiliwa na yeyote.

Mume atatoa adhabu ya kumfukuza mke wake kwenda nyumbani kwao kwa muda atakaoona ikiwa mke ataleta Mgeni pasipo kupewa kibali na mumewe, Kama huyo mgeni wa wa mke wake atakuwa ni mwanaume basi adhabu inaweza kuwa kubwa zaidi. Mwanaume usikubali na wala usiwe na huruma katika mambo kama haya.

Mke hataruhiswa kumsindikiza mgeni zaidi ya kwenye geti. Mgeni labda awe Mzazi/ mkwe ndiye atasindikizwa zaidi ya getini kwa kadiri mume atakavyoona.

Mume hatatoa ruhusa kwa mkewe ikiwa ataomba kutoka out kwa ghafla kwenda kwa rafiki yake kutembelea, au ndugiu yake, au Mtu yeyote yule iwe kwenye sherehe au tukio la kuhuzunisha, bali mke atatoa taarifa kabla ya masaa arobaini na nane . Mume anayomamlaka ya kukataa kutoa ruhusa hata akipewa taarifa mwezi mzima.

Ikiwa mume utabaini mkeo anapenda Mgeni yeyote zaidi yako, na hapa ni Mama yake au Baba yake kushinda wewe, basi Mume kama kiongozi wa nyumba utampa talaka mkeo akaishi na huyo mama/Baba yake. Usiogope bali kuwa na moyo mkuu. Hivyo ndivyo familia inajengwa.

Kwa leo niishie hapa

Ulikuwa nami;

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Tandahimba
 
Ndefu sana. Mkuu uwe unaangalia namna ya kuandika thread zako kwa ufupi. Wengine hwajazoea kusoma habari ndefu
 
Na kweli kamati ya roho mbaya imekaa.hii...ni hivi maisha.yenyewe ndio.hayahaya tunaunga unga tunasaidiana mambo yanaenda...hakuna siku matatizo yanaisha..ndiyo.maisha ni kusali na kujitahidi kuheshimiana kufuata sana haya masharti ni gubu iliyopitiliza na ukoloni mavi...yaani upangiwe mpaka kusindikiza umsindikize MTU umbali.gan? Ulisikia wapi...kama mkeo ana uzinzi ataufanyia hata hapohapo kitandani kwako ulisikia wapi MTU mzima analindwa
 
Miaka mitano naona ndugu washapigwa makala, mwaka wa 6 ukiisha tutapifwa makala namna ya kuachana na watoto wetu waliofikisha umri wa miaka 18.
 
Andiko lako zuri kwa kiasi fulani, lakini kwa maisha yetu sisi Waafrika hii huwezi kuitumia moja kwa moja japo yapo baadhi ya mambo umeyaongelea yanaweza kufanyika.
 
Asante sana kwa somo zuri japokuwa kuna mambo mengine ukiyafuata utakuwa unabomoa badala ya kujenga...hebu fikiria rafiki wa mkeo amefiwa mzazi...na maziko ni baada ya siku 1, je akikuomba ruhusa utampa baada ya masaa 48?

Kuna baadhi ya jamii mgeni anaheshimika sana...mi kwetu kwa mfano...mke wa mdogo wangu lazima aniwekee maji bafuni.

Ni kautaratibu ambako tumekakuta kukaacha inahitaji muda...sema muingiliano na watu wa jamii zingine unatutoa kwenye haya mazoea...

All in all ROBERT HERIEL umetoa somo zuri sana.
 
Asilimia kubwa umeandika makala ya kikoloni japo yapo machache yakuchukua.
 
Back
Top Bottom