Kuna demu alikuwa ananiumiza kichwa kweli hapo mwanzo hasa ukizingatia mzee nimeoza zaidi ya kufa, kwa siku kama hajanipiga mizinga 7 basi mi5, nikiona namba yake naugulia haswa. Siku 1 nikasema mimi ujinga huu nitaenda nao hadi lini, basi nikapiga moyo konde kwamba KUANZIA SASA AKINIOMBA PESA JIBU NI MOJA TU SINA. Basi kuanzia siku hiyo kila akiniomba pesa jibu langu sina, kumbe mwenzangu kuomba kwake ni hobi yake maana pamoja na kila siku kumjibu sina bado anaendelea kuniomba na huu mwaka wa 6 natoka nae na kila tukikutana au nikimpigia au akipigia simu au hata sms ni lazima atanipiga mzinga,japo kwenye mizinga 80 atapata mzinga mmoja tu lakini hakomi.