Jinsi ya kuepuka mizinga ya wadada

Jinsi ya kuepuka mizinga ya wadada

Dah...hiyo namba 4 imenichekesha haswa.

Hata hivyo tatizo mwanaume ukimhonga mwanamke atakutangaza haswa kwa wenzie kuwa wewe ni zoba anakuchuna tu.
 
Ukiona umemtumia mpenzi wako/mchumba wako/mchepuko wako/mke wako au hata rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu kwaajili ya kumsalimia lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo, tafadhali sana usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu.

KWA MFANO:
1. Ukimtumia sms ''Mambo mpenzi wangu?'' akikujibu ''mambo mabaya'', usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa ''sina hela dear''

2. Ukimtumia sms ''Maisha yanasemaje kipenzi changu'' akikujibu ''maisha magumu hubby wangu we acha tu'' usimuulize kwanini, ukimuuliza kwanini atakwambia ''nimefulia mwenzio kama nini sijui''

3. Ukimtumia sms ''Mbona kimya sana mchumba wangu, umenitupa kiasi hicho'' akikujibu ''sijakutupa wangu yaani mambo hata hayaendi'' usimuulize kwanini mambo hayaendi, ukimuuliza atakwambia kuwa ''yaani sina kitu mpenzi wangu, simu ilikuwa haina hata hela ya kubeep''

4. Au ukiona mwanamke anaanza kwa kukwambia nikwambie kitu? We mkatalie kiutani utani tu, mwambie usiniambie, hata akikomaa vipi akwambie mwambie sitaki uniambie huku unafanya kama utani lakini moyoni unakuwa upo serious.

5.Au ukiona katumia simu ya rafiki yake kukupigia au kutuma sms, usiulize kwa nin hukutumia simu yako. La sivyo simulizi za matatizo yake zitaanza
 
Hili ni janga kubwa,unaweza kuwa na nia nzuri na mpenzi lakini kila siku yeye ni mizinga tu hadi upendo unaisha,yeye ataishia kusema wanaume wanasumbua bila kujichunguza yeye kwanza
 
Honestly baadhi yenu,wanawake badilikeni Jaman....
Imenitokea hii Jana tu,nilionana na mdada ambaye tulisoma wote o level miaka hyo, baada ya yeye kuniomba tuonane Jana...yaliyonikuta nimeishiiiiia kucheka tu na kumsikitikia..
Yeye ameshaolewa na mim sijaoa, ila tulivyoonana Jana,basi alikuja na rafik yake maeneo flani hiv,wamekula wamekunywa weee bia , japo mi situmii kilev nikawa nawasomaa tu,mda ulipozid kwenda nikamuaga niondoke sababu nakaa mbali kidogo....
Hahaha et akaniuliza "Nikwambie kitu"?
Nikajua tu huu mznga.
"Eti naomba utupatie nauli"...
Sikulaza damu,nikamwambia hapa nimebakiza Mia 4 tuu,na aliziona wakat zimerudishwa na waitress, nikamwambia subili nikakutolee ATM ,maana sikua nimepangilia kuja kusastain gharama zake na best yake, au Nikutumie kwa Sim maana hapa had niende atm then niwatumie,akasema poaaa....nilipowasha gari na kusepa,sikupokea Sim yaake tena wala SMS,sabab nimemuona ni mswahil sanaaa.....Dah baadh ya madada badiliken msiwe Majipuu....

Sasa MTU hamna mahusiano yeyote then unataka unifanye ATM, thn sipend mwanamke tegemez yaan..

Halafu kaja Na team yake ili akukomoe.Hatareee
 
Hali ngumu watu wameamua kusema ya moyoni. Hatari sana
Kuna kadada ka chuo nilipanda nako bajaji. Kakatoa noti ya elf 10 kumpatia dereva ili akate elf 1, tena baada ya kumsikia dereva huyo akimlalamikia abiria mwingine aliyetoa elf 5 kuwa chenji zinasumbua. Kalipoona dereva anazidi kulalamika, kakaanza kuangalia kwenye kapochi kake huku akiniangalia kwa jicho la "NILIPIE BASI WEWE." Nikampotezea, nikatoa nauli yangu na kumpatia dereva. Kakabahatika kuipata 450, kakawa kanampa huku kamekomaa kunirembulia macho. Mi nikashuka zangu huyoooo kwenda kuweka vocha ya elf 10.
 
Back
Top Bottom