Invisible
Robot
- Feb 11, 2006
- 9,075
- 7,881
UFAFANUZI WA KINA NA MBINU ZA KUACHA UVUTAJI WA SIGARA
Mbinu Za Kuacha Uvutaji Wa Sigara
Miongoni mwa mambo magumu kabisa katika ufanikishaji wake ni mtu kuachana na uvutaji wa sigara. Watu wengi wamekuwa wakionywa kuachana na uvutaji wa sigara kwa sababu ya madhara yake, lakini wamekuwa wakishindwa kutokana na kukolewa na kiwango cha Nikotini inayopatikana katika tumbaku.
Vijana wengi wamekuwa wakijiingiza katika uvutaji kwa kufuata mkumbo, lakini baadaye wanapokuja kutambua kuwa wako katika hatari ya kuambukizwa au pengine wana ugonjwa wa kifua kikuu, wanakuwa katika wakati mgumu wa kuachana na uvutaji huo. Wengi wao wamekufa huku makundi kwa makundi wakitangatanga kutafuta suluhu ya kuchana na uvutaji, si tu kwa sababu ya kuhofia ugonjwa, bali hata kukosa uwezo wa kununua bidhaa hiyo.
Hata hivyo idadi kubwa ya wanaojaribu kuacha wamejikuta wakipata majibu ya kutoweza, kutokana na kusumbuliwa na hamu ya uvutaji, umbumbu wa mawazo pindi wanapokaa muda mrefu bila kuvuta, kuumwa na kichwa na hata udhaifu katika kukumbuka vitu au mambo waliyofanya au waliyopanga kuyatenda.
Pamoja na yote hayo watalaam na washauri wa masuala uvuaji wa sigara wanasema wanaopatwa na hayo wamekosa mbinu na muongozo wa kuwasaidia waachane na uvutaji wa sigara bila kupata madhara.
Kwa ufupi somo hili limehusisha uchunguzi wa kina pamoja na kumbukumbu za kitaalamu kutoka kwa washauri kama Anderson JE, Jorenby DE, Scott WJ, Fiore MC, Bailey WC, Cohen SJ, ambao wote kwa pamoja kupitia vituo vyao kikiwemo cha US Department of Health and Human Services na Public Health Service walishawahiwa kueleza mbinu salama za kuachana na uvuaji wa sigara.
Zifuatazo ni dondoo kadhaa za kufuata ili mvutaji aache sigara kwa usalama
- Mvutaji lazima afahamu ni muda gani ambao huwa anavuta sigara kwa wingi, je ni wakati akiwa amelewa au akiwa na mawazo mengi ya kimaisha? Akishafahamu hilo ajiulize ni kiwango gani cha sigara ambacho huwa unavuta kwa siku?
- Baada ya hapo achukua kitabu chake cha kumbukumbu na aandike muda huo ambao yeye huvuta sigara kwa wingi. Ajiulize kwa nini huwa unavuta, atathimini madhara ya uvutaji wa sigara kwake binafsi na kwa familia yako.
- Kaa chini upitie kwa makini kumbukumbu zako za muda na kiwango cha sigara unazovuta kwa nyakati hizo, kisha panga utaratibu mpya. Kwa mfano kama unavuta sana wakati ukiwa kwenye mawazo hakikisha kuwa unapoanza kufikiria juu ya jambo fulani uwe na kitu mbadala kitachukua nafasi ya sigara. Mfano kahawa au chai? Hakikisha kila penye hamu ya uvutaji unaweka kitu kingine mbadala cha kufanya zaidi ya kuvuta sigara.
- Ondoa masalio ya sigara katika sehemu ambazo unaishi, fua nguo zote na vitambaa ili kuondoa harufu ya sigara katika eneo unalokuwepo. Usikae karibu na mtu anayevuta, usikubali kuwa mshirika wa mvutaji na usiwe mtu wa kuendekeza sana msukumo wa mwili unaotaka uvute, bali kila unapowaza juu ya kuvuta fikiria madhara na nia yako ya kuacha.
- Wafahamishe rafiki zako kuwa umeamua kuachana na uvutaji, ili upate watu wa kuwaonea aibu pale utakapoanguka na kurudia uvutaji wa sigara. Panga tarehe ya kuacha na iwe kwenye kumbukumbu.
- Wakati ukiiendea tarehe hiyo ya kuacha hakikisha unapunguza kiwango cha uvutaji kadiri unavyoisogea siku hiyo. Jipangie muda mrefu zaidi ya kuvuta kulingana na kiwango chako cha uvutaji na kuendelea kuuongeza kila siku ili uzoee kukaa saa nyingi bila kuvuta.
- Fuata ratiba mbadala uliyojiwekea kuziba pengo la uvutaji, kama umepanga kutumia kahawa kila unapokuwa mpweke sebuleni hakikisha unajizoeza ili ikifika tarehe yako ya kuacha usiwe mtu wa kujiuliza cha kufanya nyakati ambazo utakuwa na hamu ya sigara.
- Lengo lako liwe ni kufanikiwa na usikate tamaa utakaposhindwa kufanikisha lengo lako kwa wakati uliojipangia. Mara kwa mara nenda kamuone daktari mshauri ili akupe muongozo zaidi wa kukusaidia na ikiwezekana akupe nafasi ya kuwatembelea wagonjwa waliopata ugonjwa wa kifua kwa sababu ya kuvuta sigara.
Kwa kifupi hizo ni dondoo chache tu za kukusaidia kuachana na uvutaji wa sigara, lakini mara nyingi kinachoweka nguvu za kufanikisha uachaji wa sigara ni utashi wa mtu ambao hutokana na tathimin ya kina ya muhusika na mtazamo wake juu ya sababu za kuacha. Mara nyingi wanaoshindwa ni wale ambao hawakuzitia nguvu sababu za kuacha kwao.
Siku zote mwanadamu anaongozwa na utashi na kila mwenye kutaka hufanikiwa. Hii ina maana kuwa kama mwanadamu atasema hawezi kuacha kitu fulani, haina maana kama hawezi kwa sababu ameshindwa kujizuia bali ameamua kutokutaka na kinachomshinda ni matokeo ya maamuzi yake. Kila anayetaka jambo hufanikiwa na hata wavutao sigara wanaweza kuacha kama wakitaka kufanya hivyo.
The purpose of this thread is to assist you to become tobacco-free forever, without the urge to start-up again. In just one week after starting to quit smoking, you can be free from smoking forever. Information in this Ebook is based on evidence from research on treatments and counseling that help people quit smoking.
If you are about to quit, do you know what to do to fight off that urge to smoke another cigarette? Do you know the reasons that cause you to light up that cigarette? If you are still smoking, you need to ask yourself, Am I ready to quit the smoking habit? Can I do it successfully?
There are two factors that will determine your success. They are;
1. You must have the desire to give up your habit.
2. You must have the confidence to know that you can do it.
Of course its possible to get motivated to quit, yet you fail for a variety of reasons. Quitting smoking can be an uncomfortable experience, and cigarettes have given you something to do for a long time. Consequently, it is only natural to think about the ups and downs of giving them up. Most who try to quit, fail to do so and have to try several times before they succeed. Should you have any doubts about giving up smoking, put it off until you are determined to do so.
===
Utafiti wa karibuni zaidi umeonesha kwamba njia bora zaidi ya kuacha uraibu wa kuvuta sigara ni kuacha mara moja. Utafiti ambao matokeo yake yamechapishwa katika jarida la kimatibabu la Annals of Internal Medicine unasema washiriki walioacha mara moja walikuwa na uwezekano mara 25% zaidi ya kutovuta sigara nusu mwaka baada ya kuachana na uraibu huo wakilinganishwa na walioacha uvutaji sigara taratibu taratibu.
Idara ya Afya ya Taifa Uingereza inasema njia bora zaidi ni kutenga siku fulani kuwa ya kuacha kuvuta sigara. Weka ahadi, tenga siku na uhakikishe umefanya hivyo siku hiyo, idara hiyo inashauri.
Utafiti huo wa karibuni uliofadhiliwa na Wakfu wa Moyo wa Uingereza ulihusisha washiriki 700 wa kujitolea. Waliwekwa kwenye makundi mawili, moja la kuacha kuvuta sigara mara moja na jingine la kuacha asteaste.
Baada ya miezi sita, ni 15.5% ya washiriki walioacha kuvuta sigara taratibu taratibu waliokuwa bado hawavuti sigara wakilinganishwa na 22% kwenye kundi la walioacha kuvuta sigara mara moja.
Kiongozi wa utafiti huo Dkt Nicola Lindson-Hawley, kutoka Chuo Kikuu cha Oxford alisema: "Tofauti inaonekana ni kama inatokana na kutatizika kwa watu katika kupunguza uvutaji sigara. Hili liliwapa jambo la ziada la kufanya, ambalo huenda liliwafanya kuacha kabisa mpango wao wa kuacha uvutaji sigara.”
Ingawa wengi wa washiriki walisema wangependelea sana kuacha uvutaji sigara, bado wale waliofanikiwa zaidi kuacha kabisa uvutaji sigara walikuwa wale walioacha Dkt Lindson-Hawley hata hivyo alisema ni heri kupunguza uvutaji sigara kuliko kutochukua hatua yoyote.
Washiriki wote walipewa ushauri pamoja na vitu vya kuwasaidia kukabiliana na makali ya kuacha uvutaji sigara.
MAONI NA USHAURI KUTOKA KWA WADAU WA JF
---Toa vitu vyote vitakavyokufanya utamani sigaraUkiashaujua kwamba kila kitu binadamu anachokifanya kinaanzia kweny mawazo yake bc ni rahisi kuacha sigara japo mwanzo arosto itakutesa. kwanza fanya hivi jaribu kila unapohisi unatamani kuvuta sigara jaribu kuyahamisha mawazo yako kufikiri vitu vingine (kujisahaulisha) au kucheki movie au kupiga story na marafiki wasiovuta sigara ili wa sikushawishi
Na kingine toa vitu vyote vitavyokufanya utamani kuvuta sigara kama viberiti ,vipisi vya sigara , vifungashio vyake na vinginevyo na kubwa zaid jitahidi kulaa pilipili nyingi kweny vyakula vyako hii itakusaidia kupunguza hamu ya kuvutaa sigara ukiwa umemaliza kulaa.
Ukijaribu kuzingatia hay naona inawez kukusaidia ndani ya wiki au wiki mbili ilaa hii ya kusema punguza kidogo watu wengi haiwasaidii .NAMALIZIA kuacha sigara ni vita kama vita vingine ila ni ni vita kati ya mawazo yako na tamaa za mwili usichukulie lelemama Amua leo na Utaacha
Sent using Jamii Forums mobile app
---Hatua za kuacha kuvuta sigaraSigara ina nicotine, a very addictive substance. Kuiacha inahitaji mkakati maalumu.Mimi nilifanikiwa kuacha kwa kujitrain mwenyewe.Fanya yafuatayo:
1. Punguza idadi ya sigara unazovuta kwa siku.Mfano kama ulikuwa unavuta packet moja kwa siku, puguza hadi sigara 15,10 hadi 5 kwa siku.
2. Jinyime kuvuta sigara usiku ,kama ulikuwa unaamka katkati ya usingizi na kuvuta,acha.
3. Jiepushe na marafiki wavutaji.Ukiwa nao watavuruga mpango wako
4. Endelea kupunguza idadi ya sigara hadi kufika moja kwa siku.
5. Unaweza sasa kuvuka siku nzima bila kuvuta.Ukifika hatua hii, jaribu kuruka hadi siku tatu bila kuvuta,lakini endeleakuhakikisha sigara ni moja tu kwa siku.Ukiweza kufikisha wiki bila kuvuta unaweza kuacha sasa.
Mpango huu niliubuni mwenyewe na ulinisaidia sana kuacha mpaka sasa sivuti.
Sent using Jamii Forums mobile app
---Mambo ya kufanya ili kuacha sigaraBro!kama una nia kweli kuacha sigara ni simple sana. Fanya hivi kila siku unapovuta sigara popote utakapokua majivu na kile kishungu vihifadhi sehemu safi may be kwenye mfuko au gazeti safi.Then ukirudi nyumbani andaa glass yako ya maji safi ya kunywa kisha weka vile vishungi na majivu ya sigara kisha funika.
Fanya zoezi hili kwa wiki moja,maji ni yale yale glass moja yafunike vizuri. Baada ya wiki moja chukua chujio yachuje yale maji vizuri kisha yanywe.Kitakachofuata baada ya muda utatapika sana. Baada ya kutapika hiyo ndio itakua tiba yako maana hata moshi wa sigara hutata kuipata tena ile harufu yake. Kila la heri kaka.
---Kuacha sigara kunaanzia mawazoni mwakoUkiashaujua kwamba kila kitu binadamu anachokifanya kinaanzia kwenye mawazo yake bc ni rahisi kuacha sigara japo mwanzo arosto itakutesa. kwanza fanya hivi jaribu kila unapohisi unatamani kuvuta sigara jaribu kuyahamisha mawazo yako kufikiri vitu vingine (kujisahaulisha) au kucheki movie au kupiga story na marafiki wasiovuta sigara ili wa sikushawishi
Na kingine toa vitu vyote vitavyokufanya utamani kuvuta sigara kama viberiti ,vipisi vya sigara , vifungashio vyake na vinginevyo na kubwa zaid jitahidi kulaa pilipili nyingi kweny vyakula vyako hii itakusaidia kupunguza hamu ya kuvutaa sigara ukiwa umemaliza kulaa.
Ukijaribu kuzingatia hay naona inawez kukusaidia ndani ya wiki au wiki mbili ilaa hii ya kusema punguza kidogo watu wengi haiwasaidii .NAMALIZIA kuacha sigara ni vita kama vita vingine ila ni ni vita kati ya mawazo yako na tamaa za mwili usichukulie lelemama Amua leo na Utaacha
Sent using Jamii Forums mobile app
---Fuata hatua hizi kuacha sigaraUnavuta ngapi kwa siku?.Tuanzie hapo kwanza
-Kama unavuta 10 anza kupunguza kidogokidogo,wiki hii vuta 8,wiki unayofuata vuta 6 kwa siku,hivyo hivyo mpaka utakuta umebaki na mbili kwa siku then moja.
-Usinunue pakti la sigara,nunua moja moja,na kama umeshaamua utavuta idadi kadhaa kwa siku nunua zote kwa pamoja uwe nazo.
-Unapovuta usiingize moshi mwingi ndani.
-space muda kati ya sigara moja na nyengine,mfano masaa manne manne ukivuta saa moja,usivute tena mpaka yapite masaa manne au zaidi.
Ps.ukiwa na stress usikimbilie pombe ama sigara,kula shada.
Sent using Jamii Forums mobile app
---Kuacha Sigara ni mind set tuSometimes ni mindset tu, nilianza kuvuta sigara 2012 nikiwa na wazungu maeneo ya baridiiiiii wenzangu wakawa wanavuta huku wapo poa tu huku mie nakufa na baridi ndio wakanishauri nivute kupunguza baridi.
Basi hadi kuja kurudi kwenye joto letu nikawa mvutaji mzuri tu na hakuna aliyekua anajua maana nilipokua navutiaga Mungu anajua tu yaaan kama mvutaji bangi kwa mashaka.
Usiku kifua kilikua kinabana kupumua shida na kukohoa hadi mama yenu (mke wangu) akahisi nimeukwaa.. Nikasema huu ni ujinga yaani nakufa nikijiona kisa kitu cha shilling 200? Basi nikaacha ghafla tu kama masikhara nikawa nafanya mazoezi ya kukimbia uwanja wa mpira kila usiku na kunywa sana maji.
Sasa hivi ushapita muda mrefu sana yaaani najihisi kama mtoto mdogo kifua kilainiiii... Ndugu zangu sigara zinazeesha na zinaua acheni masikhara kabisa
Sent using Jamii Forums mobile app
Ushuhuda kwa walioachaMimi nilikuwa mvutaji sigara tangu nikiwa shuleni miaka ya mwanzoni mwa 1960. kwa hiyo kwa karibu nusu karne, nilikuwa navuta sigara. mwaka jana mwezi juni, asubuhi nilikuwa nimebakiza sigara tatu. niliamua kwamba nikimaliza hizo tatu, basi sitavuta tena. tangu siku hiyo, baada ya kumaliza sigara zangu, sijavuta tena hadi leo.
ni kweli nilikuwa nimejaribu mara nyingi kuacha bila mafanikio. nilipatata hata kutumia patches za aina mbalimbali. na nilikuwa nawaudhi hata familia yangu nyumbani kwani nilikuwa navuta sana. lakini kusemwa hakukusaidia. sana sana iliongeza bidii yangu ya kuvuta.
kwa kuwa siku hiyo ya juni 26 niliamua bila hata kushauriana na mtu yeyote, wala sikumwambia mke wangu kwamba naacha, nimeweza kuacha. la msingi ni uamuzi wa nafsi yako bila shinikizo. inawezekana. vitabu au dawa hazisaidi kama mtu hajaamua.
macinkus
PIA UNASHAURIWA KUSOMA HAPA:
= > Sigara huharibu DNA mwilini na kuongeza hatari ya kupata kensa!