Jinsi ya ku bargain mshahara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya ku bargain mshahara

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by BLUE BALAA, Mar 17, 2011.

 1. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Huwa nashindwa kuelewa sisi watanzania huwa tunatumia vigezo gani wakati tunapatania mishahara. Mimi nafikiri kazi inatakiwa ikuhudumie mfanyakazi na siyo wewe uwe unaihudumia kazi. Kuna wafanyakazi wengi sana wanatumia resources zao wakati wakiwa kazini bila kupata malipo yoyoye yale ya ziada. Mfano mtu anatumia gari lake, mafuta yake, simu yake, PR yake etc. Na wakati ana ajiriwa anajua hayo matumizi yapo ila we never take into consideration. (Tuondoe kabisa mentality ya kupiga deal makazini.

  Ni vizuri wakati tuna bargain mishahara tuwe tuna consider yafuatayo.

  1. Nauli/Mafuta ya gari
  2. Wear & Tear ya gari
  3. Kodi ya nyumba hata kama una nyumba assume kwamba umepanga kwasababu hata nyumba yako inahitaji repair & maitanance
  4. Chakula, matibabu, ada za watoto na fedha ya dharura
  5. Markup at leat 25% ya gharama zote ili uweze ku save.

  Uzoefu unaonyesha mshahara wa kwanza ambao umepatana na mwajiri unaweza ukaongezeka baada ya miaka mitatu na siyo zaidi ya 15%. hivyo mapatano ya mwanzo yana maana sana.

  N.B NEVER EVER TRY TO BARGAIN CHEAP UKITEGEMEA KWAMBA UTAPIGA DEAL.
   
 2. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante sana Mkuu...! Tunaomba pia maelezo ya jinsi ya kuandika CV kama utakuwa na uzoefu..!
   
 3. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Karibu sana, CV sina uzoefu nayo sana ila najuwa hutakosa mtu hapa jamvi la wajanja
   
 4. NOT ENOUGH

  NOT ENOUGH JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 526
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huwezi kuishi bila ya deal makazini. Labda kwa sisi madada upate boss huko ofisni awe ana ku support
   
 5. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Binafsi sina uzoefu mkubwa saana katika hili lakini ninaweza nikashauri kutokana na general knowledge. Upo uandishi wa aina nyingi saana wa CV kutegemeana na wapi na nani unampelekea. Lakini kubwa zaidi ni content ya CV unayoiandika. CV haitakiwi iwe copy and paste. Inatakiwa iwe inaandika kutegemeana na kazi mtu anayotaka kuiomba na kuonyesha uwezo (strength) kulingana na hitajio la kazi. CV nyingi siku hizi huanza kwa kuandika jina na address on top then summary ya yule mtu kwa mistari michache saana juu ya uwezo wake. hapo ndio inabisi uzitaje zile uniqueness zako zinazoweza kukufanya uwe superior over others. Sema experience qulification na personal qualities kiasi tu hapo ila kwa maandishi ya kuvutia bila kuboronga lugha. Waombe watu waipitie CV yako ikiwezekana. Hapo hakikisha kabisa unaonyesha link ya kazi unayoiomba na uwezo/uzoefu wako. Baada ya hapo endelea na education background. Sema vitu relevant. Usihangaike na mpangilio wa primary sijui sekondari unless kazi unayoiomba inahitaji uonyeshe hiyo primary na sekondary. Anza na latest qualifiacations vivyo hivyo na job experience na awards zinazofanana na kazi ile au zinazoonyesha umahiri wako. Hayo ni baadhi, kuna issue za personal info na references nazo ni muhim pia huku na contact zikionekana kwa uwazi.
   
 6. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,644
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280

  mkuu hii ni kweli kabisa, wengi wetu tunakua desperate sana kwenye interview hata take home tunazoomba hazilingani kabisa na maisha ya sasa, inabidi tubadilike jamani tujue thamani yetu
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Unfortunately waajiri wetu (na hasa HR managers) hawajuo hayo mambo, wao wako bize kuanalia mwajiri atafaidi vipi huduma yako at the cheapest rate
   
 8. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Na mwajiri akishaona uko desparate ndo anakukandamiza kabisa. Sasa usikubali kuwa desparate kwani hapo una uza PRODUCT yako ambayo ni wewe mwenyewe who knows your qualities
   
 9. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  HR yuko kwa ajili ya ku maximize upande wa mwajiri hivyo usitegemee kwamba anaweza kukusaidia.
  You need to be YOURSELF when bargaining, bargain kile ambacho unaona kitakuwa na manufaa kwako. Dont be weak my friend utaishia kula 150,000 kwa mwezi pamoja na degree yako.
   
 10. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Well said, kuna kazi moja niliapply tena ilitangazwa hapa jamvini..walitaka kunitoa nilipo sasa for less than what i get now
  nikawaambia kwendeni kule..kisa tu working environment ya kwao ni nzuri kuliko nilipo.
  hawajui mi nimepiga mpaka gharama nilizotumia nikiwa chuo eboo.
  Waajiri nanyi muwe mnaangalia hili,msipende kulalia sana,mnajikuta mnakosa wafanyakazi wazuri kwa ubahili wenu
   
 11. B

  Bernardus New Member

  #11
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante ndugu, mtazamo wako unafaa tutaufanyia kazi.
   
 12. M

  MAKARONI New Member

  #12
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haya bwana na sisi waserikalini tutabargain na nani yetu nDO KAMA ILEEEEEEE
   
 13. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
   
 14. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2011
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,015
  Likes Received: 1,828
  Trophy Points: 280
  Pia tuangalie na Mazingira tunayoenda kufanyia kazi. kuna rafiki yangu alikimbilia kigoma kufanya kazi kisa mshahara mkubwa baada ya miezi mitatu ndo akaanza kujutia kukaa kigoma. alikua akirudi kutoka vijijini akifika geto anakuta geto limenuna inabidi aanze kutafuta mboga na kupika hapo kachoka balaa na nguo za kuvaa kesho kazini zote chafu na mambo mengine mengi tu ya kukela. kununua vitu vya ndani hakuweza kununua kwakua familia yake ipo mbali na yeye yaani aliishi maisha kama vile mwanafunzi wa shule ya boarding. baadae aliamua tu kutafuta kazi sehemu nyingine na kulipwa mshahara nusu ya ule aliokua akiupata kigoma
   
 15. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Yaani na wewe bado una mawazo ya kihivi?
  Pole sana.
   
 16. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
   
 17. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kuna ukweli hapo, ila kubagain mshahara pia hutegemea kazi unayoomba, nafasi yako ktk kazi hyo, uzoefu ulionao na uhusiano wake na kazi ynyewe, kiwango chako cha elimu na uhusiano wa elim hiyo na kazi yenyewe n.k ambavyo watataja wengine.

  Kwa mfano nilipomaliza chuo niliwah omba kazi ktk kampuni ya teleco, ilikua ni nafasi ya u catama care.nikaitwa kwa intaviu.
  kwa uelewa nilokua nao ile kazi hua ni full bize full day, na wakati mwingine hua kazin mtu unakwenda saa 6usiku(wanaofanya watashuhudia).
  haya na mengine mengi yakanifanya nikawataka wanilipe laki7.ila waniambia "yani we ni fresh from collage na unataka laki7??"
  "Nenda tutakwita" hadi leo hii.mwenzangu tuliekua ane akataka laki 4 na akapata ile kazi.
   
 18. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Deliverable za mwajiriwa zinaanza pale anapokuwa sehemu yake ya kazi, amefikaje toka huko anakolaza mbavu zake hata sheria ya kazi haitambui hilo. Ale nini watoto wasome wapi hilo atajipangia mwenyewe kulingana na anavyotaka kutumia mshahara alioomba. Hivi mnataka mwaajiri awafanyie haya yote kwa kutumia kipato kipi? Kama wewe unamchango mkubwa kwenye mapato ya mwajiri wako ni busara kurudi mezani ili mshahara upande juu badala ya kutegemea mwajiri akuhudumia kama House Girl
   
 19. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  pia tunatakiwa kuangalia kiwango cha mshahara cha hiyo proffesion kikoje kwa wakati huo.
  Mfano kama mshahara wa wahasibu kwa wakati huo laki 8- mil 1 inabidi na wewe mshahara utakaobargain uwe ndani ya hiyo range.
   
 20. Mutashobya

  Mutashobya New Member

  #20
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  People say dat wen luv comes knocking on ur door let it in.But sumtimes luv
  comes through a backdoor & by the time u notice its on its way out.
   
Loading...