Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,425
Mwezi January maisha yalikuwa tofauti na yalivyo sasa. Covid-19 tuliisikia tu kama hadithi kutoka Wahuan. Nilialikwa kwenye tafrija moja. Nilikutana na mwanaume wa Kitanzania, ni Mhandisi kitaalauma.
Yule bwana anavutia sana, hana tumbo na kwa jinsi alivyopangilia mavazi yake, zaidi ya mvi kichwani huwezi kidhani ni 50+ alionekana kama kijana wa 30.
Tuliongea kwa takriban masaa matatu tukiwa pale kwenye tafrija. Nilimuuliza siri ya muinekano wake. Alisema kuanzia akiwa 35 ndiyo aliweka mazoezi kuwa sehemu ya maisha yake. 40 aliamua kuacha kunywa pombe. Alisema ni majukumu kwani wakati huo alikuwa anamalizia kujenga nyumba na pesa ilikuwa inahitajika. Aliamua kufanyia watu kazi za taaluma yake katika muda wa ziada. Baada ya kutokushika pombe kwa miezi sita aliamua kuachana nazo kabisa.
Sasa hivi ana nafasi ya juu sana kazini kwake. Anaishi kwenye nyumba yake hivyo hana changamoto za maisha baada ya kustaafu. Aliniambia asubuhi anakimbia kwa lisaa limoja. Akirudi nyumbani anaoga na kula matunda. Baada ya hapo mke wake au dada anakuwa amemfungia mayai mawili ya kuchemsha anakula kazini na maji anakunywa sana.
Jiioni akifika nyumani chochote kilichopikwa atakula lakini hata chakula kiwe kitamu haongezi sahani ya pili. Kabla ya kulala anakula bakuli la salad Lina matango, parqchichi, nyanya vitu kama hivyo.
Hajawahi kuwa na matatizo ya sukari wala moyo. Akiugua mara nyingi ni malaria.